Wabunge 10 wa chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge 10 wa chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchonga, Dec 2, 2010.

 1. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wabunge 10 wa chadema waliokataa kuingia bungeni ni akina nani?
   
 2. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145

  Hii ni sehemu ya habari iliyoandikwa na Mwananchi Newspaper ikiwataja wabunge hao:

  "Wabunge hao kuwa ni Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Said Arfi (Mpanda Mjini) ambaye ni Naibu Mwenyekiti Taifa wa chama hicho, Mhonga Luhwanya (Viti Maalum), Jonh Shibuda (Maswa Magharibi), Maulida Komu (Viti Maalum).

  Wengine ni Profesa Kulikoyele Kahingi,(Bukombe), Rachel Mashishanga(Viti Maalum), Raya Ibrahimu(Viti Maalum), Lucy Owenya (Viti Maalum) na Suzan Lyimo(Viti Maalum).

  "Lakini wabunge John Mnyika (Ubungo) na Halima Mdee (Kawe), walitoa udhuru kwamba walikuwa wanaumwa na Philemon Ndesamburo (Moshi Vijijini) alikuwa safarini. Hawa hawatapewa barua ya kujieleza, '' alisema Lissu.
   
 3. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Thanks DEODAT
   
 4. K

  Kishili JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 293
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Na kama kuwatosa na watoswe maana wanafurahi sana kuvunja daraja letu pekee(CHADEMA) kuvuka kulekea kuiondoa CCM
  ikulu. hasa mwepesi asipewe hata uwaziri kivuli maana hatutakuwa na uhakika kama atafanya kazi ya CHADEMA au ya CCM
   
 5. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  sasa jamani hii ni akili au hao wabunge wa viti maalumu waliogoma kwenda kumuonyesha jk kuwa wewe na wateuliwa wako ( nec) wamemuibia dr slaa kura wanajua kuwa nafasi zao za viti maalumu zimepatikana kutoka kwa dr slaaa. so wakati dr analalamika kuibiwa kura wenyewe wanagoma kumsupport kwa kuonyesha umoja katika chama!!!!!!! aingii akilini mtu aliye kusaidia mpaka ukafika mjengoni analalamika na asilimia kubwa ya watanzania wanajua ana haki aliyony'ang'anywa na hao wachakachuaji the wewe unagoma kuto support yako... shame on u all traitors...
   
 6. D

  Deo JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kati ya hawa ni wepi walifanya kikao kisicho rasmi kuwa hawatahudhuria?
   
 7. D

  DENYO JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Chadema wanashugulikia hili tunataka zitto avuliwe madaraka yake na aombe radhi kubaki na uanachama kigeugeu mkubwa na njaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa zake
   
 8. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mbona wote majina yanaonekana kulandana ? Au ndo walitaka wamsapoti jeykey mwenye asili yao? Mbona wana mambo ya ajabu! Zitto adai udini unasumbua ,ana akili timamu kweli? Ivi kugomea jk udini uko wapi? Zitto ondoka chadema haraka,naapa siingii chadema mpaka msaliti aondoke!
   
 9. 1

  1954 JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 4,282
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  CHADEMA hilo mnalo. Mkiwafukuza tu kutakuwa na uchaguzi mdogo ambapo CHADEMA lazima itapoteza. Huo ndio utakuwa mwisho wa CHADEMA kutamba kuwa kiongozi wa upinzani Bungeni. CUF watakuja kula kuku kwa raha zao.
   
 10. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  wavuliwe nafasi za uongozi chamani na bungeni itakuwa somo kwa wasaliti wengine
   
 11. m

  mbezibeach Senior Member

  #11
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni huyu mtoto anayeendekeza njaa itakuwa alifanya kampeni za chinichini kushawishi wenzake wasije bungeni.....maana kama huyo wa viti maalum Kigoma hakutokea itakuwa yeye ana mkono wake hapo.Halafu jana nimekiona tena TBC eti kinasema bado hakijapata barua..halafu eti nchi ina matatizo ya umeme.....maji....kwa hiyo tu-concentrate huko kwenya matatizo ya nchi...Kinafikiri kitaharibu chama halafu tukiache salama?
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  Wabunge CHADEMA wamshtaki Zitto


  *Waitaka Kamati Kuu imuhoji kwa kukiuka maamuzi
  *Wamo pia wengine 9 waliokacha ufunguzi bunge


  Na Edmund Mihale

  WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameiandikia barua Kamati Kuu ya chama hicho kuiomba imuite Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe na wabunge wengine tisa ili wajieleze kwa nini walikiuka maamuzi halali ya
  vikao.

  Hatua hiyo imetokana na kitendo cha Bw. Kabwe na wenzake kutoingia bungeni Novemba 18, mwaka huu ambapo wabunge hao walikuwa wameafikiana kwa kura, kuwa watoke nje ya ukumbi wa bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akizindua bunge.Pamoja na makubaliano hayo, Bw. Zitto ambaye ni Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni na wabunge hao hawakuingia bungeni.

  Wengine ambao hawakuonekana siku hiyo ni Bw. Said Arfi (Mpanda Mjini) ambaye ni Makamu Mwenyekiti Taifa wa chama hicho, Mhonga Luhwanya (Viti Maalum), Bw. John Shibuda (Maswa Magharibi), Bi. Maulida Komu (Viti Maalum), Profesa Kulikoyele Kahingi,(Bukombe), Bi. Rachel Mashishanga (Viti Maalum), Bi. Raya Ibrahimu (Viti Maalum), Bi. Lucy Owenya (Viti Maalum) na Bi. Suzan Lyimo(Viti Maalum).

  Akizungumza na Majira kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Mnadhimu wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani bungeni, Bw Tundu Lisu alisema kuwa Bw. Zitto amendikiwa barua mbili tofauti na wabunge wengine kutokana na kitendo hicho.

  "Zitto kama Zitto ameandikiwa barua mbili, moja ikiwa ya kitendo cha kushindwa kuingia bungeni jambo ambalo tuliamua katika kikao ambacho hata yeye alikuwepo."Barua hiyo iko tayari lakini ninachojua kuwa yuko Ughaibuni na sijui kama amerudi kwa kuwa alinitumia ujumbe mfupi wa simu kuwa anakwenda Malaysia lakini hajaniambia kuwa amerudi. Kusema kuwa yuko hapa nchini ndiyo sasa unaniambia," alisema Bw. Lissu.

  Alisema kuwa barua ya pili imeandikwa kwenda Kamati Kuu na wataitwa na kutoa maelezo mbele ya kamati hiyo. "Kwa kanuni za Katiba ya CHADEMA, Kamati Kuu ndiyo yenye uamuzi wa mwisho ama kumpuuza kama itaona jambo hilo halina uzito, au kama lina uzito itaunda tume kuchunguza tuhuma hizo na iwapo itabainika itachukua hatua," alisema Bw. Lissu.

  Alisema kosa lingine la Bw. Zitto ni kitendo cha kuwapigia simu baadhi ya wabunge kuwataka kutoka nje ya kikao kilichoitishwa na chama hicho baada ya kutoka bungeni, akiwataka kutoka katika kikao hicho na kumfuata aliko, jambo lililokera wabunge hao, hivyo kutoa taarifa katika kikao.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw Zitto alisema hadi sasa hajapata barua yoyote, na kuwa hizo ni habari za mitaani kwa kuwa hakukuwa na kikao chochote klichoketi ili kujadili suala hilo.

  Alisema yeye ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Naibu Katibu Mkuu na pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, hivyo alipaswa kujua hayo yote."Hizi ni habari za mitaani, mimi sijapata barua yoyotem niliyoandikiwa na CHADEMA," alisema Bw. Zitto.
   
 13. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  Chama kinaendesha kikao, Zitto anawapigia baadhi ya wajumbe wa kikao hicho waachane na kikao na kwenda kwake.Kama yaliyoandikwa ni kweli, hii haijakaa vizuri.
   
 14. Mathias

  Mathias Senior Member

  #14
  Dec 3, 2010
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jamani tuache majungu, hii habari ya Zitto kutoonekana bungeni haina tija yoyote. Kama adhima ya chama ilifikiwa (kwa asilimia 90) na watanzania wengi wanakubaliana na msimamo wa chama, aya mengine sidhani kama ni tatizo. Kwenye mkusanyiko wowote lazima utegemee watu wengine kufikiria au kutenda tofauti na maadhimio ya wengi. Maadam Zitto akubakia ndani ya Bunge (hasingeweza kubakia kwa sababu hakuwepo), na kutokufika kwake bungeni inatosha kuonyesha kuwa anakubaliana na msimamo wa wabunge wenzake wa chama kwa kutokumsikiliza JK.
  Pili, lazima tujenge utamaduni wa kuheshimu mawazo ya watu wengine na kuamini kwamba sio lazima wote tuwe na wazo moja. Mwenzetu anapowaza tofauti na sisi, tukubaliane nae na tumsikilize. Inawezakana akawa sahihi zaidi yetu, ndo demokrasia hii. Tukianza hii habari ya kukubali kila kitu na kufikiri kama mwenyekiti tutakuwa tunarudi nyuma na kuukaribisha umwinyi ulioko huko ccm, ambako kuhoji mawazo ya mwenyekiti ni uhaini.
   
 15. m

  mbezibeach Senior Member

  #15
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha upumbavu tunazungumzia kutotii maazimio ya kikao halali cha wabunge wa chama.....lazima chadema iwe na kauli moja.....acha kueneza kansa....akili zako ziko sawa?
   
 16. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwani huwa mnapewa barua za kujieleza kwa nini mnaandika lugha safi? Lugha chafu huongeza malumbano na kuamsha hasira. Pia inaonyesha kuwa heshima kwa mawazo ya wengine haipo, hivyo misingi ya demokrasia pia haisimamiwi.
   
 17. T

  Tovu Member

  #17
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mskaji mimi nakukubali sana kuhusu wabunge wa Chadema kutoka nje ya bunge najua ukiizungumzia hii hoja inaonekana umechelewa lakini ngoja. Unajua hawa wabunge wengine wa chadema hawaoni mbali kuwa kupata kura nyingi Dr. Silaa kungesaidia wabunge viti maarum kuongezeka upande wa Chadema na baada ya kuchakachua nafasi hizo zimekwenda CCM na kuongeza nafasi za ubunge kwenye chama chao kwa hiyo Dr. Slaa halii na yeye kuwa Rais tu na pia anaona nafasi ya Chadema bungeni haikupashwa kuwa hivi kama ilivyo walitakiwa wawe hata 50% kwa 50% na CCM ili malengo ya kuchukua nchi na kuingoza kwa haki na kweli yatimie na si ubabaishaji sasa wengine waliochaguliwa kwa viti maarum nao wanakimbia majukumu Upuuzi hatuja lizika kupata wabunge tu tunataka Rais pia atoke Chadema lakini naona wabunge wengine wa Chadema mawazo yamefika mwisho baada ya kupita kwenye majimbo yao sasa wanachuchnganya. ni hayo tu
   
 18. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #18
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  na walioangalizia hotuba kwenye ukumbi mdogo wa wabunge watachukuliwa hatua gani? upuuzi mtupu na unafiki. Unakataa kumuona live, kisha unaenda kumtazama kwenye kioo.

  Inahitajika akili kujua...

  iko sababu, bora ambao hawakwenda maana hawakushiriki unafiki ule :embarrassed:
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  crap
   
 20. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #20
  Dec 3, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  msitishie kufa wakati kuzimia hamuwezi
   
Loading...