Kama hujui maana ya walk out huna haja ya kutoa pumba hapa, ina maana wote tulioangalia kwenye tv tuliingia bungeni au wewe ukimsikiliza Osama kwenye tv ina maana umekubaliana naye acha ujuha wako.na walioangalizia hotuba kwenye ukumbi mdogo wa wabunge watachukuliwa hatua gani? upuuzi mtupu na unafiki. Unakataa kumuona live, kisha unaenda kumtazama kwenye kioo.
Inahitajika akili kujua...
iko sababu, bora ambao hawakwenda maana hawakushiriki unafiki ule :embarrassed:
Hii ni sehemu ya habari iliyoandikwa na Mwananchi Newspaper ikiwataja wabunge hao:
"Wabunge hao kuwa ni Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Said Arfi (Mpanda Mjini) ambaye ni Naibu Mwenyekiti Taifa wa chama hicho, Mhonga Luhwanya (Viti Maalum), Jonh Shibuda (Maswa Magharibi), Maulida Komu (Viti Maalum).
Wengine ni Profesa Kulikoyele Kahingi,(Bukombe), Rachel Mashishanga(Viti Maalum), Raya Ibrahimu(Viti Maalum), Lucy Owenya (Viti Maalum) na Suzan Lyimo(Viti Maalum).
Lakini wabunge John Mnyika (Ubungo) na Halima Mdee (Kawe), walitoa udhuru kwamba walikuwa wanaumwa na Philemon Ndesamburo (Moshi Vijijini) alikuwa safarini. Hawa hawatapewa barua ya kujieleza, alisema Lissu.