Wabongo acheni kukariri maisha

Wabongo acheni kukariri maisha

Kuna jamaa yang alikaa na mwanamke miaka 11 bila kufunga ndoa,, wakajaaliwa watoto, walijenga nyumba, mambo flesh kabisa,, sijui nn kimewakuta,,

Hivi sasa mwanamke anataka nyumba iuzwe wagawane,, mwanamke anadai hakuolewa na hana ndoa 🤣 kapigilia msumari na kusema watoto si wa jamaa yetu,

Haya mambo yasikie tu,

Huyu mtoa mada anaonekana ana magoma mengi anayachakata🤣
Akifunga ndoa sheria itambana😁
 
SIFUNGI, SADAKA NATOA KWA WASIOJIWEZA NA WAHITAJI HATA MITAANI WAPO SIO LAZIMA NIMPELEKEE 10% MCHUNGAJI
Genius Punguza maarifa basi kidog uelewe. Mambo ya imani hayapo ivyo kama unavyo fikili ki kawaida ina kupaswa uamini kwanza ndo uongee hiicho unacho kiongea bila hivyo usijadili maswala ya imani kama wew uamini uwezi kuwa na hoja za kuwambia wanao amini hasa katika kweli.
 
Mimi naishi na mwanamke ambae HATUJAFUNGA NDOA, ila Sasa cha kushangaza ni watu huko kanisani mwanamke anapoenda kutwa kumshauri eti tufunge ndoa, majirani wale wenye ndoa kutwa kumshauri shauri tuu, Mimi naishiaga kuwaambia tuu NDOA SIFUNGI

ni kama ishu ya kipaimara/kubarikiwa Mimi tokea Niko darasa la saba nilishakimbia hayo mambo, na Leo hii wale waliobarikiwa 90% nnaowajua ni wavuta bangi,walevi na wamechoka mbaya (kipindi tukiwa shule ya secondary walinitabiria Mimi eti nitakua na maisha magumu kwakua sijabarikiwa/sijapata kipaimara, lakini kwasasa wao wamechoka sana Mimi Niko vzuri.

Hawa wanaonishauri Mimi nifunge ndoa unakuta mtu ana miezi SITA kwenye ndoa, wengine ndoa zimevinjika zimewashinda Mimi watanishauri Nini???

Nyie mnaoenda kanisani mnajiona sana Yani mnaona kama yesu sijui ni mjomba wenu au ndio mnamjua mungu sana! ACHENI KUKARIRI MAISHA

Mambo ya kufunga ndoa Kwa Sasa minaona kama ni JANJA JANJA TUU, kama nataka kuishi na mwanamke naishi nae sio lazima ndoa.

Eti utakuta mtu kwakua alikua haendi kanisani huko KKKT siku anataka kufunga ndoa mchungaji anamkataa anasema hamtambui kwakua sio mshirika! Halafu utakuta mtu anapaniki kabisa Kwa kukataliwa kufungishwa ndoa kanisani unapaniki Nini wewe ACHENI upumbavu
Acha ngonjera wewe,funga ndoa watu tule cha mtume

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Kosa halirekebishwi kwa kufanya kosa Mkuu, ni haki na uhuru wako kuishi utakavyo as far as huvunji sheria.

Ila hiyo haiondoi maana na msingi wa issue kama ndoa na kipaimara kwa waumini wa dhehebu husika

Ie we ishi utakavyo ila jua taratibu zipo tu, kuna siku utajikuta umenasa unahitaji huduma ya imani yako hapo utaona umuhimu wa kutii bila shuruti.
Safi.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Kuna jamaa yang alikaa na mwanamke miaka 11 bila kufunga ndoa,, wakajaaliwa watoto, walijenga nyumba, mambo flesh kabisa,, sijui nn kimewakuta,,

Hivi sasa mwanamke anataka nyumba iuzwe wagawane,, mwanamke anadai hakuolewa na hana ndoa kapigilia msumari na kusema watoto si wa jamaa yetu,

Haya mambo yasikie tu,

Huyu mtoa mada anaonekana ana magoma mengi anayachakata
Akifunga ndoa sheria itambana
MIMI NDOA SIFUNGI, FUNGENI NYIE
 
Muda ndio utakaoamua. Mambo yote ya uongo yatazidi kuondoka na kupitwa na wakati na dunia itabaki kwenye Ukweli kama Zamani.

Mwanadamu ni mnyama anayejikosha tuu.

Wanaotaka kufunga ndoa wafanye hivyo ili waende sawasawa na mila, desturi na imani zao na kuwafurahisha wazazi na wazee wao ikiwa ndio hivyo. Lakini ujinga wao unajitokeza pale ambapo wanawapigia kelele wale wasiofanya kama wao ilhali ya kwao yenyewe yalishawashinda.

Angalia wengi wanaosema ndoa ndoano asilimia 90% wamefuata hizo taratibu. Afu angalia wanaoenjoy maisha ya ndoa asilimia 90% hawajafunga ndoa (hawajafuta taratibu).

Ambao hawajafunga ndoa kuachana ni dakika sifuri kwa sababu hawapo chini ya yeyote, na hakuna unafiki.
Lakini waliofunga ndoa ni kama watoto wadogo ambao kila kitu ni mpaka waombe ruhusa na mpaka wapewe ruhusa
Kuna jamaa yangu ndoa ina miezi mitatu tuu kutwa kwenda kusuluhisha Kwa wazee, mpaka anasema isingekua hii ndoa ningeachana nae, ndio ishakula hiyo
 
Unaweza ukajiona uko sahihi kumbe hauko sasa naanza kukuonyesha namna gani hauko sahihi:-

1. Kila jambo lina utaratibu, na utaratibu ndio unaotengeneza ustaarabu, kanisa lina utaratibu kwamba mwanamke na mwanaume hawawezi ishi pamoja bila kufunga ndoa, kwa hiyo wewe uko nje ya utaratibu, kwa sababu mke wako anasali kanisani na ndiko wanakomwambia akuhimize mfunge ndoa maana ndio utaratibu wa kanisa.

2. Kufunga ndoa hakuna maana kwamba ndani ya ndoa hakutakuwa na migogoro au kupishana kauli huko uwe umefunga au haujafunga lazima mtapishana kauli na kukwaruzana tu.

3. Ili mtazamo na msimamo wako uwe sawa mwambie mkeo asiende kanisani ili wote msisali na kwa hapo hakuna imani itakayokuwa inawaongoza zaidi yenu wenyewe.

4. Kubatizwa, kupata kipaimara hakuna maana kwamba ndio umekuwa mtakatifu na mbinguni utaenda la hasha, ni takwa la kiimani kulingana na utaratibu wa kanisa na bibilia na Yesu anasema lolote lililokubalika duniani na mbinguni limeekubalika, kama una mpango wa kwenda mbinguni basi kubatizwa ni lazima lakini kama hauna mpango sio lazima
Mkuu, umesema kwa busara, na umeeleweka, vema Sana, ilaa pia kipimo upicho mpimia mleta mada , utumie kupimia kanisa ,

je wanalo fanya kanisa ni njia iliyo nyoofu kwa kufuata msingi wa maandiko ya kitabu Cha Imani? (Biblia).
Kama tuta mhukumu ,kwa muktadha wa serikali , na kanisa Kama watakavyo , Basi tutamuona ana makosa Sana.
Ila Kama Ni Kumpima pia kwa muktadha wa kijamii na Imani (Kuwa na hakika na bayana kwa yasio onekana) ,mwamba yupo vizuri na Hana kosa.
Na yupo kwenye ndoa ilio kamili Wala Hain mawaa na Mungu ameikubali (Maana pande zote mbili zimeridhia kwa maana ya wazazi, na mahari watu wamekula).

Kwa Watu wa Kanisani huko, Kazi ya utumishi wa Mungu ni kuwaatoa , gizani na kuwaleta kwenye Nuru kwa njia ya Imani. Si kutoa hukumu na kufanyia ugumu watu kumkaribia Mungu , kwa kigezo Cha Ubatizo, Kipaimara na Ndoa.
Hivi inawezekanaa vipi mtu, anyimwe kufungishwa ndoa ya kanisa , Kisa Hajitokezi Kanisani , Hajapata Ubatzo wala Kipaimara ? Lengo ni Nini ?
Hivi wewe, mchungaji na Baraza lako,mliotunga tunga sheria sijui ni taratibu kumzia mtu kufunga ndoa na mwanamke ampendae , kwa kigezo Cha kutokufungama na kanisa , Je unahakika ndivyo Mungu anavyo taka kuwa ? Je Kama kanisa, Jambo hili , linatofauti gani na lilee la kupokea msamaha wa dhambi ,kwa malipo ya Cheti ndio uonekane umesamehewa ? (Historia ya kanisa).
Upande wa pili kule , wakikuona tu ,umepenyeza hata kwa bahati mbayaa unapigwa Cha mkeka kuhalalisha ,
Nivipi huku kwa Yesu wangu Mambo Ni mazito Sana kwenye Jambo la maana Kama hili , kwa vigezo vya bahasha za ahadi ,sadaka,jumuia,kipaimara, ubatizo nk ...?
Huu je ni mpango wa Mungu ?

Ndugu mleta mada, kula matunda mema ya ndoa yako halali kabisaa.
Ni ndio ambayo haina mashaka ndani yake hata kidogo.
Husihuzunishwe Wala kuyumbishwa na vyeti vyeti , vyenye mlengo nje na Imani ya kweli ya kristo Yesu na Mungu baba na Roho wake.
Chapa kazi , tunza familia, baraka Ni nyingi mnoo.
 
Nashukuru mkuu naomba nikujibu kama ulivyouliza, Kwanza lazima tukubali kuwa ndoa ni mpango wa Mungu, na Mungu aliweka makuhani yeye mwenyewe ili wawe wapatanishi kwahiyo ndoa ni mpango wa Mungu, lakini utaratibu ni mpango wa wanadamu, na huo utaratibu unakubalika kwa Mungu maana maandiko yanasema lolote mnalolipanga duniani na mbinguni limepangwa, hapo unaweza kuelewa.

Sasa mtu kuishi na mwanamke bila ndoa inaweza ikawa sahihi lakini iko kinyume na imani ya kikristo, naona wengi wanazungumza kutokana na madhaifu ya hao wachungaji na wainjilisti pamoja na hayo haiondoi kuwa kuishi na mwanamke bila ndoa kwa imani ya kikristo sio sawa, pengine inaweza kuwa sawa kwa imani zingine huko sijui. Yaani ni sawa na mtu kuishi na mtoto wa watu bila kumtolea mali au kujitambulisha kwao hilo kitamaduni na kimila haliko sawa hata kama tunaona watu wanafanya ila halijakaa sawa naamini hapo umenielewa

Kuhusu ubatizo yes ni lazima muumini mkristo abatizwe hiyo ndio maana ya kuwa mkristo kama hautaki kuwa mkristo sawa kubatizwa sio muhimu mbona Waislam hawabatizwi lakini ninaamini wanautaratibu wao, kuhusu sijui bahasha na sadaka bado ni utaratibu wa kanisa husika
 
Mkuu, umesema kwa busara, na umeeleweka, vema Sana, ilaa pia kipimo upicho mpimia mleta mada , utumie kupimia kanisa ,

je wanalo fanya kanisa ni njia iliyo nyoofu kwa kufuata msingi wa maandiko ya kitabu Cha Imani? (Biblia).
Kama tuta mhukumu ,kwa muktadha wa serikali , na kanisa Kama watakavyo , Basi tutamuona ana makosa Sana.
Ila Kama Ni Kumpima pia kwa muktadha wa kijamii na Imani (Kuwa na hakika na bayana kwa yasio onekana) ,mwamba yupo vizuri na Hana kosa.
Na yupo kwenye ndoa ilio kamili Wala Hain mawaa na Mungu ameikubali (Maana pande zote mbili zimeridhia kwa maana ya wazazi, na mahari watu wamekula).

Kwa Watu wa Kanisani huko, Kazi ya utumishi wa Mungu ni kuwaatoa , gizani na kuwaleta kwenye Nuru kwa njia ya Imani. Si kutoa hukumu na kufanyia ugumu watu kumkaribia Mungu , kwa kigezo Cha Ubatizo, Kipaimara na Ndoa.
Hivi inawezekanaa vipi mtu, anyimwe kufungishwa ndoa ya kanisa , Kisa Hajitokezi Kanisani , Hajapata Ubatzo wala Kipaimara ? Lengo ni Nini ?
Hivi wewe, mchungaji na Baraza lako,mliotunga tunga sheria sijui ni taratibu kumzia mtu kufunga ndoa na mwanamke ampendae , kwa kigezo Cha kutokufungama na kanisa , Je unahakika ndivyo Mungu anavyo taka kuwa ? Je Kama kanisa, Jambo hili , linatofauti gani na lilee la kupokea msamaha wa dhambi ,kwa malipo ya Cheti ndio uonekane umesamehewa ? (Historia ya kanisa).
Upande wa pili kule , wakikuona tu ,umepenyeza hata kwa bahati mbayaa unapigwa Cha mkeka kuhalalisha ,
Nivipi huku kwa Yesu wangu Mambo Ni mazito Sana kwenye Jambo la maana Kama hili , kwa vigezo vya bahasha za ahadi ,sadaka,jumuia,kipaimara, ubatizo nk ...?
Huu je ni mpango wa Mungu ?

Ndugu mleta mada, kula matunda mema ya ndoa yako halali kabisaa.
Ni ndio ambayo haina mashaka ndani yake hata kidogo.
Husihuzunishwe Wala kuyumbishwa na vyeti vyeti , vyenye mlengo nje na Imani ya kweli ya kristo Yesu na Mungu baba na Roho wake.
Chapa kazi , tunza familia, baraka Ni nyingi mnoo.
Wanachokifanya ni kuwatenga wasioenda kanisani, badala ya kuwatengenezea mazingira ya kurudi kundini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom