Wabongo acheni kukariri maisha

Wabongo acheni kukariri maisha

Si wanasemaga ukifa kama haukufunga ndoa hawakisalii,

Unaanza ukumiwa kabla ya kushindiliwa kifusi
 
Funga Ndoa acha maneno mengi, ipo siku utajua nini maana ya kushiriki mambo ya Kanisa bado hujapatwa na changamoto.
 
Mimi nmeishi na mwanamke miaka mitatu bila ndoa na sahv naona afadhali sijafunga ndoa maana mwanamke kawa jeuri hatare, na nmezaa nae ila namtaftia namna ya kuachana nae, maana mwanamke hataki kujishusha afu tukikosana kidogo basi anatoa matusi ambayo Mimi kama mwanamme siwezi kuyatamka namimi naona inapofikia nitampiga kitu ambacho nishaapishwa na mama yangu kamwe nisije kumpiga mwanamke ni heri kuachana nae
pigaaa domoo lakeee akili zimkaeee
 
Kama unaishi na mwenza wako na hutaki ndoa unaogopa majukumu.

Hapo ulipo unauwezo wa kumfukuza huyo mtoto wa watu muda wowote.,na hakuna wa kukuuliza sababu huna ndoa nae.
Lakini ukishapiga pingu ya maisha huwezi kufukuza mke kiholela.

Sheria zitakubana..

Pia hapo ulipo hutambuliki ukweni zaidi ya watu wawili watatu wanaokutambuwa.
Hata baba mkwe na mama mkwe kuja kwako pia haiwezekani...

Kama kidume oa basi,,uone cha mtema kuni.

Hapo ndy vijana wa hovyo mnapaogopa..
Unaweza kufunga ndoa lakini usimfukuze bali ukamwacha
 
Hakuna sheria inayokulazimisha kubaki ndoani hata moja.
Ukiamua kuvunja ndoa unavunja muda wowote na hakuna yeyote atafanya chochote zaidi ya kujaribu kukushauri tuu.

Hakuna kitu kinachoitwa pingu za maisha. Ni maneno ya uongo. Watu wanavunja ndoa hata mwezi haujaisha tangu wafanye harusi.

Ndoa ni makubaliano ya Hiyari ya Watu Wawili. Na inahusisha Majukumu ya wanandoa tuu bila kuhusisha Watu wa nje. Wengi wanaotaka ndoa zifungwe ni kutaka kujiingiza kwenye familia za Watu kwa kuomba misaada.


N
Ni kweli ndoa ni makubaliano ya hiyari,

Lakini yanampa mwanandoa kujiamini zaidi na mwenza wake kuliko kuishi bila ndoa.

Mwanamke akiwa na ndoa huwezi kufukuza kiholela,
Kama hawara.
 
Mimi naishi na mwanamke ambae HATUJAFUNGA NDOA, ila Sasa cha kushangaza ni watu huko kanisani mwanamke anapoenda kutwa kumshauri eti tufunge ndoa, majirani wale wenye ndoa kutwa kumshauri shauri tuu, Mimi naishiaga kuwaambia tuu NDOA SIFUNGI

ni kama ishu ya kipaimara/kubarikiwa Mimi tokea Niko darasa la saba nilishakimbia hayo mambo, na Leo hii wale waliobarikiwa 90% nnaowajua ni wavuta bangi,walevi na wamechoka mbaya (kipindi tukiwa shule ya secondary walinitabiria Mimi eti nitakua na maisha magumu kwakua sijabarikiwa/sijapata kipaimara, lakini kwasasa wao wamechoka sana Mimi Niko vzuri.

Hawa wanaonishauri Mimi nifunge ndoa unakuta mtu ana miezi SITA kwenye ndoa, wengine ndoa zimevinjika zimewashinda Mimi watanishauri Nini???

Nyie mnaoenda kanisani mnajiona sana Yani mnaona kama yesu sijui ni mjomba wenu au ndio mnamjua mungu sana! ACHENI KUKARIRI MAISHA

Mambo ya kufunga ndoa Kwa Sasa minaona kama ni JANJA JANJA TUU, kama nataka kuishi na mwanamke naishi nae sio lazima ndoa.

Eti utakuta mtu kwakua alikua haendi kanisani huko KKKT siku anataka kufunga ndoa mchungaji anamkataa anasema hamtambui kwakua sio mshirika! Halafu utakuta mtu anapaniki kabisa Kwa kukataliwa kufungishwa ndoa kanisani unapaniki Nini wewe ACHENI upumbavu
Ukishaenda kanisani ambako watu wanakulazimisha kufunga ndoa kinyume na maoni yako tu unakosa haki ya kuwaambia watu wasikariri maisha.

Kwa sababu hata wewe itaonekana unakwenda kanisani kwa kukariri maisha.

Kanisani kama ni sehemu ambako watu wanaamini katika kufunga ndoa, na wewe huamini katika hilo, kwa nini bado unakwenda na kuwaharibia watu imani zao?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom