Wabeba mabegi mgongoni wanavyosumbua ndani ya daladala

Wabeba mabegi mgongoni wanavyosumbua ndani ya daladala

Halafu kuna akina dada nao wanabeba mapochi makuuuubwa kama wanahama vile. Unakuta kaning'iniza vizuri tu kwapani hilo pochi lake halafu kaliweka kichwani kwa abiria aliyekaa sasa anahangaika kulikwepa muda wote wa safari, hlf yanakuaga na ncha kali sasa likikugonga ni lazima usikilizie maumivu.
Wanatembea na pochi mbili !!!
 
Jirani yangu kaja nalo kalivaa ila kalipakata
 
[emoji23][emoji23][emoji23] jamani sio kwa kutukandia huku, mimi siku hizi nimesahau kubeba pochi ni mwendo wa begi tu
Mnasahau kuwa mmeongeza kitu kwenye mwili wenu kwahio mkipita sehemu lazima muache maumivu
 
Nimecheka sana hapo mwisho ulivyomaliza mkuu.
Wakuu poleni na kazi. Niende kwenye mada, kuna jamii kubwa kwa sasa, wake kwa waume wamekuwa wakibeba mabegi migongoni, siyo shida wala hakuna neno, ni vizuri pia.

Ila, baadhi yao, wanapoingia ndani ya daladala hawayakulii namna ya kuyabeba, bado wanakuwa nayo migongoni na mbaya zaidi, konda anataka kusimama wawili wawili, hapo ndipo shida hutokea.

Wawili waliosimama halafu wamepeana migongo yenye mabegi, kivumbi chake si cha kitoto. Hali hiyo huwafanya kuinamia mpaka kwa abiria waliokaa kwenye siti ambao nao hunesa mpaka kulaliana.

Nashauri, tukiingia ndani ya daladala mabegi tuyashikie kwa chini ili kuondoa kero kwa wengine.

Na kama hoja ni ile kauli ya 'ndiyo usafiri wetu ilivyo' basi sawa, acha tuteseke tu.
 
Halafu kuna akina dada nao wanabeba mapochi makuuuubwa kama wanahama vile. Unakuta kaning'iniza vizuri tu kwapani hilo pochi lake halafu kaliweka kichwani kwa abiria aliyekaa sasa anahangaika kulikwepa muda wote wa safari, hlf yanakuaga na ncha kali sasa likikugonga ni lazima usikilizie maumivu.
Ha ha aisee hatari sana comment nzuri na wahusika wame elewa.
 
inategemea na nimeweka nini ndani ya begi,na nyie msiotaka tubebe mabegi

mnataka tuende na vikapu mlimani city? yani naena nunua earphone na simu nibebe kapu ndo mnavyotaka?

ebuuuuuu nipisheni....
 
Tubebe nini sasa
Bebeni hata masanduku, ila mnapopita sehemu mkumbuke mmebeba mabegi yanayowagonga watu na vitu vingine. Imagine mtu anapita na begi lake yeye kapita ila begi lake mgongoni linagonga side mirror hadi inageukia mbele!

Ni kama dereva wa bodaboda amebeba gunia la mkaa ila anapenya katikati ya magari anakadiria upana wa usukani wake mbele anasahau upana wa gunia la mkaa nyuma
 
Sawa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom