Wabeba mabegi mgongoni wanavyosumbua ndani ya daladala

Wabeba mabegi mgongoni wanavyosumbua ndani ya daladala

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
430
Reaction score
727
Wakuu poleni na kazi. Niende kwenye mada, kuna jamii kubwa kwa sasa, wake kwa waume wamekuwa wakibeba mabegi migongoni, siyo shida wala hakuna neno, ni vizuri pia.

Ila, baadhi yao, wanapoingia ndani ya daladala hawayakulii namna ya kuyabeba, bado wanakuwa nayo migongoni na mbaya zaidi, konda anataka kusimama wawili wawili, hapo ndipo shida hutokea.

Wawili waliosimama halafu wamepeana migongo yenye mabegi, kivumbi chake si cha kitoto. Hali hiyo huwafanya kuinamia mpaka kwa abiria waliokaa kwenye siti ambao nao hunesa mpaka kulaliana.

Nashauri, tukiingia ndani ya daladala mabegi tuyashikie kwa chini ili kuondoa kero kwa wengine.

Na kama hoja ni ile kauli ya 'ndiyo usafiri wetu ilivyo' basi sawa, acha tuteseke tu.
 
Halafu kuna akina dada nao wanabeba mapochi makuuuubwa kama wanahama vile. Unakuta kaning'iniza vizuri tu kwapani hilo pochi lake halafu kaliweka kichwani kwa abiria aliyekaa sasa anahangaika kulikwepa muda wote wa safari, hlf yanakuaga na ncha kali sasa likikugonga ni lazima usikilizie maumivu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom