Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara MTPC wapewa mafunzo ya Usalama Mtandaoni

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
View attachment JF-1-35.jpg
JF-1-24.jpg
JF-1-22.jpg

JamiiForums imeendesha mafunzo ya Usalama Mtandaoni kwa Waandishi wa Habari 25 wanaowakilisha Vyombo mbalimbali vya Habari Mkoani Mtwara kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara MTPC

Mafunzo hayo yanalenga kuongeza ufanisi kwa Waandishi katika kazi zao kwa kuzingatia Mabadiliko na kasi ya ukuaji wa Teknolojia Duniani ambayo ambayo huambatana na changamoto mbalimbali ikiwe Usalama wa Kimtandao

=============

Waandishi wa habari 25 wanaowakilisha vyombo mbalimbali vya habari Mkoani Mtwara, wameshiriki mafunzo ya kujengewa uwezo usalama wa kijitali yaliyoendeshwa na Taasisi ya JamiiForums ya Jijini Dar es salaam ikishirikiana na Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara MTPC.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Tarehe 07 Septemba 2023 Afisa Programu – Uwajibikaji Bi. Nancy Minja, ameeleza kuwa mafunzo hayo yamelenga kuongeza ufanisi kwa waandishi wa habari katika kazi zao.

Nancy amesema kuwa ukuaji wa teknolojia Duniani umeambatana na changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili sekta ya habari na waandishi wa habari, hivyo ni vema kukumbushana na kuelekezana mambo muhimu kuhusu usalama wa kimtandao.

Kwa upande wake Ofisa programu wa vyombo vya habari vya mtandaoni kutoka Taasisi ya JamiiForums Zawadi Mkweru, amewashuri waandishi wa habari kuhakikisha vifaa vyao vya kazi zikiwamo simu na kumpyuta vinakuwa na Nywila (Password) imara, kama sehemu ya kujilinda katika kazi zao.

“Password ni sehemu muhimu sana kwa Mwanahabari kuwa nayo kwa sababu tunafahamu hata kisheria pia ukikamatwa na Polisi yani simu yako ikikutwa kwamba ilikuwa haina Password ni kosa.”

“Simu yako ikiibiwa sasaivi kama Mwanahabari kuna watu wangapi nyuma yako wataathirika, kuna mashahidi wangapi wa stori ambazo umeziandika watakuwa wameanikwa halafu watu watajua kumbe yule ndio alituchoma kumbe yule ndio alitufanya hivi.” Amesema Zawadi.

Naye Afisa Programu – Maudhui kutoka JamiiForums Bw Juma Hulwe aliyewasilisha mada ya Usalama Mtandaoni aliwakumbusha waandishi wa habari kuhakiki vifaa vyao vya kazi hususana simu na Kompyuta ili kuvikinga na mashambuli ya mtandaoni.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) Grace Kasembe, amesema mafunzo hayo yaliyoshirikisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya mtandaoni na visivyo vya mtandaoni, yamelenga kuwasaidia waandishi kwenda na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.

Miongoni mwa waandishi wa habari waliopata mafunzo hayo ni pamoja na Gregory Millanzi kutoka Jamii Fm, ambaye amekiri kuelewa umuhimu wa kuhakiki taarifa kabla ya kuichapisha mtandaoni pamoja na kuzingatia usalama kwa wanahabari.

Mafunzo hayo yamefanyika siku Moja huku yakiwezeshwa na taasisi ya JamiiForums kwa kishirikiana na MTPC.
 

Attachments

  • JF-1-34.jpg
    1 MB · Views: 3
  • JF-100.jpg
    1.1 MB · Views: 3
  • JF-1-24 (1).jpg
    JF-1-24 (1).jpg
    660.2 KB · Views: 1
  • JF-1-19.jpg
    1,012.8 KB · Views: 3
  • JF-1-8 (1).jpg
    690.7 KB · Views: 3
Back
Top Bottom