Waalimu wa siku hizi hadi muambiwe kuwa hali za maisha yenu sio nzuri!? Juzi tu hapo serikali imekuja na kikokotoo cha pensheni za watumishi mkiwemo nyie waalimu. Watu mnakatwa pensheni yenu na mpo kimya tu?!
Pensheni ni mali yenu na sio msaada kutoka serikalini, mnapaswa kuelewa kuwa mmechangia pensheni hiyo kwa kukatwa kigogo kidogo kila mwezi na hivyo mnapostaafu mnapaswa kupewa hela yenu yoote na sio sehemu tu au kulipwa kidogo kidogo hadi mtakapokufa na inaishia hapo!
Na viongozi wetu pia muwe na weledi wa kutosha. Hivi kweli mnawekeza kwenye vifo vya watumishi wenu! Kwanini kutokumpa mtumishi pensheni yake yote anapostaafu? Mnakuja na mpango wa kumpa mtumishi kidogo kidogo hadi atakapokufa na malipo yanaishia hapo. Hamjui kuwa pensheni ni akiba waliyojiwekea watumishi wakati wakiwa wanafanya kazi na kwamba ni haki yao na wanapaswa kulipwa pensheni yao yote?
Mpango wa pensheni kwa kikokotoo ni serikali kukosa ubunifu wa kukusanya mapato na hivyo kuingilia pensheni za watumishi; hili ni kosa dhidi ya ubinadamu!
Lakini na nyie watumishi wa serikali mpo wapi? Au mnafikiri maandamo ni kwa ajili ya vyama vya upinzani tu?! Hivi waalimu wa siku hizi mnaweza kweli kuwafunza wanafunzi ujasiri, kupigania haki au upeo wowote kweli?!