Faiza,Waarabu wa zamani hapa Tanzania walikuwa na biashara za maduka ya rejareja, karibu yote Dar.
Wamepand kidogo kidogo mpaka sasa wana hayo makampuni makubwa makubwa, sasa wewe unataka uanze kukimbia hata kutambaa hujaanza?
Wachaga ni mfano mzuri wa biashara (wana ila moja tu, ambayo waarabu hawana), wanaanza kibanda cha sigara, mara viwili, mara vitatu, mara wanaenda Dubai mara wanashindana na AM.
Umenichekesha sana. Nilipokuwa mdogo kuna huyu Mwarabu akiitwa mshiiri. Yeye alikuwa anauza kanga, nguo za akina mama, etc. etc. Sasa kitu cha ajabu, akikuta hauna hela, mathalani kaja kule kwetu bara mwezi April, atakuuzia nguo bila kukutoza kitu. Anajua kuwa mwezi wa saba nane ni wakati wa kuvuna pamba maeneo ya kwetu na watu wana hela. Utamkuta anapita kila nyumba aliyotoa nguo na kanga za mkopo kukusanya hela zake. Hii ilikuwa inatokea karibu kila msimu wa pamba. Na alikuwa hasahau!