Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,552
Africans have about 5000 years of evolution to catch up with the rest of the world. Lives of many (I dare say most) Africans today are comparable or worse in quality to the lives of Asians or Europeans 5000 years ago. Of course by quality I am not referring to intangible aspects of life such as happiness but more like general health, diet, life span, material possessions of the general population. The biggest obstacle in overcoming chronic African problems is the low average IQ among Africans (approximately 70 points). Average IQ of 70 points makes it almost impossible to function and compete in the modern world.
Important: It is also good to note that average of 70 IQ points also means that there are many Africans who score well above 70 points and some even fall into the genius category. This is what Dr. James Watson was referring to in his controversial statements.
Ulemhola nkwingwa?
Nalimhola Nkoi.
nobhese ku detroit huku tulimhola! tuliko tukulyaga mbuta; bhasukuma twitanagaka chengu menule!
" Mimi ni mzabibu wa kweli, tawi langu lisilozaa nitaliondoa na kulitupa"Yesu Kristo
Je sisi ambao "ndivyo tulivyo" ni tawi lile lisilozaa?
Napenda niukuu ile slogan ya Nyani Ngabu na kuurudisha mjadala ambao ulishafungwa na labda tukipata wakti kuuangalia upya tunaweza kubadili fikira zetu na kuulizana jee sisi ndivyo tulivyo? matendo yetu, tabia zetu, fikira zetu, hulza zetu, utamaduni wetu, kufanya kazi kwetu, kuridhika kwetu, kulalamika kwetu, utegemezi wetu, uvivu wetu?
Jambo lililonisukuma kuanza jiuliza swali hili tena ingawa sikushiriki mjadala uliopita au kupitia kitabu cha Bundala kama kilivyoletwa na Zanaki wa Radio Butiama ni mambo kadhaa na tabia za "kawaida" katika jamii yetu na hata hapa kijiweni.
Wenzetu wazungu, ugumu wa maisha kutokana na hali yeyote, milele umekuwa ni kichocheo cha wao kuwa wachapa kazi, wavumbuzi, watafiti na kuendelea kutafuta suluhisho la matatizo yao au kuongeza ufanisi kupunguza ugumu na makali ya maisha au uchapa kazi. Mafanikio yao si kabisa au kamili (absolute/perfect), lakini husaidia sana kuleta mabadiliko na maendleo katika maisha na jamii zao na hivyo kuendelea kuwa na hali nzuri za maendeleo mpaka tunawanyeyekea na kuwaita "Nchi Matajiri".
Sisi tumedumaa, je ndivyo tulivyo?
Sasa hivi tumeletewa Mjapani yupo Ikulu kutushauri na kutufundisha jinsi ya kuachana na jembe la mkono, je Aisco, UFi, Ushirika, SUA, TFA, Kilimo wako wapi? je hawaoni umuhimu wa kuleta maendeleo na kuleta zana mpya za kuongeza ufanisi na uzalishaji mali mpaka tuletemwe taarishi kutoka Ajemi au Mashariki ya mbali? je sisi ni wavivu wa ubunifu na hatuna wataalamu wa kutosha au ndivyo tulivyo twashukuru kusaidiwa mpaka Chandarua?
Hujuma; ATC, BOT, Richmond, TISCAN na sehemu nyingine, jami tunapiga kelele na kushindana kutoa mapovu, lakini hakuna hata mmoja wetu ambaye yupo tayari kusema ngoja niende mahakamani na kudai haki kama Katiba inavyosema. Tumeachia Serikali "ifanye kazi huku tukiendelea kufaidi kupiga kelele na kutoa matusi na kashfa, "Chenge fisadi, Lowassa mhujumu, Screw Muungwana, Riziwani, Manji, Rostam, Othman, Bangusilo" na majina kibao kulia hujuma, ufisadi, Sisiemu, je hii ndio tabia yetu kuishia kulalama na kuendelea kunyanyaswa? je ni hali yetu ya ndivyo tulivyo inayofanya tuendelee kuhujumiwa?
Wakati wa sakata la maji Chuo Kikuu, niliuliza kwa nini Idara ya Uhandisi pale Chuo isiwe ya kimapinduzi na kufanya utafiti wa kina (utumike kama somo kwa wanafunzi na wapeme maksi kwa kushiriki) na kutafuta suluhisho la uhaba wa maji ambalo limetawala Chuo Kikuu kwa miaka mingi? Majibu yakaja Sisiemu, UDSM sio chuo tafiti, ooh Msola na lawama kibao! Je ndivyo tulivyo?
I would have thought kwamba Idara na wanafunzi wa Uhandisi wangekutana na Chuo cha maji, chuo cha ardhi na idara ya Jiolojia pale UDMS na kusema, jamani tutumie "talanta" (kama in Maryam anavyosema) tutafute mbinu za kuleta maji, iwe ni kuchimba visima, kuweka mabomba ya kiwango fulani, kutengeneza pampu au hata kutumia nyezno zote kutafuta namna ya kutumia lita 10 kupata mafanikio ya kutumia lita 30 za maji(efficiency)! Lakini kama Tulivyo, tunailaumu Dawasco, Azimio, CCM na Mafisadi!
NI lini basi tutaacha kuwa "ndivyo tulivyo"? Je tuna hata nia ya kuachana na dhana na fikira hizo za "Ndivyo Tulivyo"? maana ni mentality ya namna hii imetufanya tuendeleel kuwa tegemezi, kuhitimu katika uvivu, kuendelea kunyonywa na kupunjwa na mwishowe tumeanza kudhulumiana na kutafuna njia panya na za haraka kujipatia marudufu.
Huu Ufisadi, Uhujumu, Uzembe na Kunyonywa kungeendelea kutoea kama tungeamka na kusema "hivi sivyo tulivyo" na kuanza kufanya mambo kwa njia za maendeleo kama Wazungu, Waasia na Wamarekani kusini?
"Ndivyo Tulivyo" wikiendi njema kwenye kupata Kilauri, nyama choma, Ikibinda nkoi na Poozeo la kugombea baa (bamedi kama si changudoa)! Ndivyo tulivyo!
Nyani.
Ulimpinga na kumdhibiti sana Raj Patel enzi hizo kwa ku-advocate huu usemi, lakini naona mwishowe umekuwa muumini wake. Ukiondoa lugha mbaya ya Raj, na badala yake kuangalia substance na arguments za maneno yake, itabidi ukubaliane naye kuwa kuna kitu si sahihi kuhusu sisi watu weusi.
Mzee mwanakijiji,
Mkuu maelezo mazito sana na umegusia sehemu nyingi zinazozungumzia Sivyo tulivyo ktk fikra na pengine matendo ya wale wachache ktk kundi la kondoo. Lakini ktk utawala wa leo utakuta wameajiriwa mbwa maalum kwa kazi ya kuhakikisha kondoo hao wachache pia huishia zizini. Mwisho wa yote sote huingia ktk zizi moja pamoja na jitihada zote ambazo wengi huwa hawaelewi kwa nini Mwanakijiji hapendi kwenda zizini baada ya malisho. Na kwamtazamaji nje ya juhudi zote humwona Mwanakijiji pia akiwa zizini kundi moja na kondoo wengine kiasi kwamba hawezi kuona tofauti.
Jitihada hizi zote hapa JF ni ktk mapinduzi ya Kifikra na ndivyo changamoto analolitoa Nyani Ngabu ktk hatua nyingine, bila shaka ni muhimu ikienda sambamba na fikra za mapinduzi. Pengine yawezekana ndio mwanzo unaotakiwa tukubali kwanza Ndivyo tulivyo ili tuweze sote kupata tiba kwani kuukataa ugonjwa tukiwa ndani ya zizi kwa sababu kuna baadhi kati yetu wana ugonjwa huo wa kuambukiza itakuwa nje ya kutafuta solution. Hapa JF hatupo nje ya zizi mkuu wangu tumo ndani.
Binafsi namwelewa sana Rev. Kishoka na nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sana na kama utakumbuka niliwahi sema solution ktk swala la Siasa ni kuwepo kwa Chama kimoja tu - CCM kisha sote tubanane humo humo. Mfumo wa kumchagua rais uwe kama wanavyofanya Marekani leo hii ktk vyama kumpata mgombea sisi iwe ndio imetoka hiyo. Nina hakika kina Salim, JK, Mbowe, Lipumba, Lowassa wote watapata nafasi sawa chini ya mwavuli mmoja kuliko huu utaratibu wa vyama vingi hali kimoja kati yao kimejengwa na Taifa zima.
Ndivyo tulivyo ni utamaduni ambao hutumia scare tactic na hakika mwafrika hasa Mdanganyika anavyoogopa kufa njaa hawezi kuona Chadema ama CUf inaweza vipi kuondoa adha hiyo ikiwa wao kupewa mlo wa siku moja tu imekuwa nongwa, itakuwaje mwaka mzima!
Kumbuka una deal na watu wenye njaa, hayo maswala ya kwenda kulima tumbo halina kitu mkuu wangu watu wengi hawafahamu. Harusi iliyofana husifiwa kwa chakula kilichokuwepo mengine yote ya hotuba na kadhalika (helikopta) ni majivuno ya mwenye nacho kwa Mdanganyika. Huongeza chuki na maseng'enyo kwani ndvyo tulivyo hatupendi maendeleo ya mtu kama yatapitia gharama ama maamuzi yetu hata kama ni kwa faida yetu sisi.
Tukiwa tunazungumzia watu binafsi basi hata mimi nitaangukia kwenye kundi la Sivyo Nilivyo. Lakini mimi nazungumzia picha kubwa. Swali lingine la kujiuliza, hivi wengi wetu humu tusingekuwa ughaibuni tungekuwa tunafikiria kama tunavyofikiria sasa hivi?
Ninaelewa vizuri kinachojaribu kusemwa na pole pole kwa mbali mmeanza kukipata ninachosema. Nitajaribu kukileta karibu zaidi.
Je Watanzania wote "ndivyo walivyo"? je weusi wote "ndivyo walivyo". Mada hii inasema "Watanzania ndivyo tulivyo" na imedokezea kidogo kuwa "waafrika" ndivyo tulivyo. Ina maana wote? Hili ninalikataa kwani hata wakati wa utumwa si wazungu wote walishughulika na utumwa na si wazungu wote waliamini watumwa siyo binadamu. Wapo katika fikra zao walipinga. Hata kina Jefferson wenyewe waliona ubaya wa utumwa kifikra ingawa na wenyewe walikuwa nao.
Sasa wale ambao wako kwenye kundi la "ndivyo tulivyo" hawawezi kutoka humo na kuanza kutenda na kuleta mabadiliko bila ya kubadilisha fikra zao. Kuna baadhi ya timu huendelea kufungwa na timu nyingi kwa sababu kwenye fikra zao wamekubali kuwa wa ni medebweda! Wachezaji wa timu hiyo licha ya mazoezi na utaalamu wa viungo hawawezi kusonga mbele kwa sababu hawajiamini na wamekubali kuwa wao ndivyo walivyo.
Mwenye macho haambiwi kodoa! Je, watanzania wote wamekubali utawala dhaifu, usio na mwelekeo wa CCM? Je Watanzania wote kwa kukubali "ndivyo tulivyo" wameshindwa kuonesha kupinga kwao hali ilivyo na kuchagua tofauti? Tukisikiliza mawazo ya wateteo "ndivyo tulivyo" tunaweza kushawishika kuamini kuwa hakuna Watanzania wenye kwenda kinyume na status quo.
Niwape mfano; uchaguzi wa 2005 Kigoma Kaskazini chama cha Demokrasia ambacho kilimsimamisha mgombea kijana Bw. Zitto Kabwe kilishinda jimbo hilo kwa Zitto kupata kura 28,198 na mgombea wa CCM kupata kura 21,822. Zitto akashinda kwa kura 6376. Kwa maneno mengine karibu watu thelathin elfu walikataa "ndivyo tulivyo" na leo hii tunakubaliana kuwa walifanya uchaguzi sahihi! Hili hamlioni?
Niwape mfano mwingine; Jimbo la Ubungo mgombea wake ambaye nusura abwagwe na bwana mdogo mwingine Bw. Charles Keenja alishinda jimbo hilo kwa kupata kura 98,473 na mpinzani wake bwana mdogo John Mnyika kupata kura 45,164. Leo hii wangapi mmelisikia jina la Mnyika zaidi kuliko Keenja? Leo sitoshangaa wakazi wengine wa Ubungo ambao walimpigia Keenja wanajuta kufanya uchaguzi huo kwa sababu walikubali mawazo ya "ndivyo tulivyo". Lakini hata kama hakushinda tuna ushahidi wa wazi kuwa watu 45,000 jijini Dar walikataa status quo, walikataa ndivyo tulivyo! kweli hawa hamuwaoni? mnaona wale walioshinda tu?
Hebu tuangalie Moshi Mjini. Mgombea wa Chadema Moshi Mjini mzee Phillemon Ndesamburo alishinda kwa kupata kura 32,025 na yule wa CCM Bi. Elizabeth Minde alipata kura 23,773. Mzee Ndesa alimbwaga kwa kura 8252. Mtu wa kawaida hawezi kuona hilo kwa sababu haamini kuwa wakazi wa Moshi wamekataa "ndivyo tulivyo" na wakaamua kuonesha bila chembe ya shaka kuwa wao sivyo walivyo! Hatuwaoni hawa kwa sababu tunaamini kuwa "ndivyo tulivyo".
Twende Kiteto kwenye uchaguzi huu uliopita. Mgombea wa CCM Bw. Benedict Nangoro alishinda kwa kupata kura 21,506 na mpinzani wake (niliyempigia debe kwa mbali) Bw. Victor Kimesera alipata kura 12,561. Kwa yule anayeamini kuwa "ndivyo tulivyo" yeye anaangalia zile kura 21,506 na kuona watu wamekubali status quo na kwa haraka atasema unaona "mbona Kiteto wameichagua tena CCM". Ingawa anachosema ni kweli lakini anashindwa kuona (a.k.a hataki kuona) kuwa kuna wana Kiteto elfu kumi na mbili hivi ambao wakionesha uhuru wa fikra zao na maamuzi ya kukataa hali "ilivyo" wakaamua kupiga kura kinyume na status quo! Kwanini hawa hamuwaoni kuwa wanaonesha kwa vitendo vyao kuwa "sivyo tulivyo".
Katika mifano hiyo minne utaona kuwa watanzania wenzetu zaidi ya laki moja na kumi na saba elfu wamekataa kuwekwa kwenye kundi la "ndivyo tulivyo". Hawakusema, hawakuimba, na hawakutangazwa magazetini bali kwa vitendo vyao wameonesha kuwa wanaweza kuwa tofauti!
Lakini tuachane na mambo ya kura kwa sekunde chache; Hapa JF tumepata bahati ya kupata taarifa ambazo vyanzo vyake ni ndani ya serikali. Kuna watu serikalini amba wamekataa kabisa kuwa "ndivyo tulivyo" na kutokana na wanayoyaona wameanza pole pole kupinga kwa kuonesha uozi na uchafu serikali. Ripoti zilizokwisha bandikwa na ile itakayobandikwa Jumatatu (kama mipango yao haitabadilika kwa kuamini ndivyo tulivyo) ni ushahidi wa wazi kuwa hata kwenye utumishi wa umma watu wameanza kukataa kwa vitendo "ndivyo tulivyo".
Hawa sitaki kuwakatisha tamaa kuwa "jamani ndivyo tulivyo, kwanini mnafunua mambo haya wakati hakuna lolote litakalobadilika?". Kwanini watu hawa warisk kazi zao, majina yao, na hadhi zao in a loosing battle? Kwanini, tuwatie moyo kufanya na kusimamia mambo ambayo tunajua hayatabadilisha lolote? Kama ndivyo tulivyo, kwanini tunapoteza muda kujadiliana na kukosoa wakati tumeshaamini kuwa "watanzania ndivyo tulivyo"?
If we were to agree to your proposition, we would have fundamentally, agreed to inferiority of mind and purpose. Tutaonekana tumekubali kuwa siyo tu Watanzania hatuwezi kubadilisha, bali pia hatustahili kubadilisha kwa sababu hakuna kati yetu mwenye uwezo wa kubadilisha kitu kwani "wote" ndivyo tulivyo.
Hivyo katika mifano hiyo tunaweza kuhitimisha mambo machache. Kwanza si wote "ndivyo walivyo" kwa sababu tuna ushahidi wa kiimpiriko kuwa kuna zaidi ya watanzania laki moja ambao wamekataa kuichagua CCM. Na pili kama kuna Mtanzania zaidi ya mmoja ambaye ameonesha kuwa hayuko kwenye kundi la "ndivyo tulivyo" basi kauli kuwa "Watanzania ndivyo tulivyo" inadondoka kifudifudi na kuvunja pua!
Kitu ambacho kinanifanya nitangaze pasipo shaka. Bado binafsi niko upande wa wale wote wanaokataa status quo na ambao hawakubali kupiga magoti kwenye altare ya washindwao na ambao wamenyosha mikono ya kusalimu mbele ya wale watubezao kama kina watson!
I categorically and singularly as an individual and part of a movement deny, despise, disagree, reject, unequivocally and perpertually the thoughts, ideas, sentiments, and everything else that says directly or indirectly that I, a black man, born of a black parents or of mixed race in a country called Tanzania that I'm inferior to anybody in the world or in any shape, manner, or form that I'm unequal in dignity, abilities, possibilities and opportunities just because I'm of a difference race or geographic origin. This I denounce without hesitation and unambiguously!
To this, I sign!
M. M. Mwanakijiji on this date of the year of Our Lord March 8th, 2008
And that is my final thought on the subject. Thank your friends!!
Nakuunga mkono kwa kuyaweka wazi mawazo yako Mkjj, ila kuna moja nitakuja nalo ambalo ni more holistic kwani linajumisha baadhi ya binadamu wa asili nyingine pia, katika hilo naomba uchangie maana naona umeanza kuweka ultimatums za kiaina.. lol
Hii dhana ya kwa vile Ndivyo Tulivyo basi sisi ni inferior sijui mmeitoa wapi. Haina maana hata kidogo kama wewe ndivyo ulivyo basi uko chini zaidi ya watu wengine kwenye mambo ya msingi. Ndivyo Tulivyo kwangu mimi ni dhana inayoelezea uwezo wa jamii nzima kutawala mazingira yake na si watu binafsi au watu wachache ktk jamii na mafanikio yao kimaisha.
Halafu hii mifano ya kisiasa wala haileti maana yoyote. Hao watu waliowachagua wagombea wa CCM na wenyewe wanaweza wakawanyooshea vidole watu wa upinzani na kusema wapinzani ndivyo walivyo na hawaelewi nini kinachoendelea.
Maisha ya jamii za kiafrika au watu weusi kwa kweli bado yako nyuma kiujumla ukilinganisha na jamii zingine bila sababu yoyote ile ya msingi kwa mtazamo wangu. Hivi mmejiuliza ni kwa nini? Niwape mfano mmoja au miwili. Nianze na usafi. Pale Kipawa kuna magenge na mama ntilie kibao. Katika eneo hilo hilo kuna majalala na mitaro ya maji machafu iliyoziba na kusababisha harufu mbaya. Iwe asubuhi, mchana au jioni utakuta watu kibao wamefunga kwa hao mama ntilie wakipata msosi. Hivi ni kwa nini watu wale chakula ktk mazingira kama hayo? Yaani watu kwa umoja na ujumla wanashindwa kuhakikisha angalau mazingira ya panapopikwa chakula ni masafi? Jamani hivi ni mimi tu nionaye kwamba kwenye jambo kama hili hatuhitaji chama chochote cha kisiasa kuja kutusafishia?
Aisee nina mambo kibao ninayoweza kuyataja hapa lakini ngoja ninyamaze tu maana anayetaka kukubali na akubali atayekataa na akatae. Ukweli uko palepale.
Kwa hiyo kimsingi dhana yako ya "ndivyo tulivyo" doesn't carry or imply any negative connotation? Kwa hiyo inaweza kuwa ni positive trait siyo?
Could be both...
If I say Africans are more gregarious than whites because that is just the way they are....is that a good or bad thing?
that is such a blanket statement..