The man with the whip asks, ΒWhatΒs your name?Β The answer comes back, ΒKunte Kinte.Β Down comes the whip. And again the question is asked, ΒWhatΒs your name?Β Defiantly, the answer once more is, ΒKunte Kinte.Β Over and over the same thing happens, WhatΒs your name? WhatΒs your name? My name is Kunte Kinte. My name is Kunte Kinte.
The lash keeps falling, and Kunte Kinte keeps proclaiming his name, until, bloodied and crying with pain, he whispers, ΒMy name is Toby.Β The lash comes down again, ΒI didnΒt hear you. WhatΒs your name?Β Kunte Kinte raises his voice and says, ΒMy name is Toby.Β
SIVYO TULIVYO!, tumekubali kuambiwa ndivyo tulivyo hadi tumeamini kuwa ndivyo tulivyo! Na ni kwa sababu hii mgongano wa kifikra umetokea na ni mgongano huu unaothibitisha kuwa si wote wako hivyo.
Wale wenye mawazo ya "ndivyo tulivyo" ndio ambao wanashindwa kufikiri kuwa kuondokana na jembe la mkono hakuhitaji mtaalamu toka Japan ambaye tayari alikuwa nchini kwa shughuli nyingine! Ni wale wenye mawazo ya "ndivyo tulivyo" ndio ambao wanajikuta hawako tayari kusimama na kusema "mkataba huu siwezi kuusaini kwa sababu hauna maslahi kwa nchi yangu". Ni wale wenye mawazo ya "ndivyo tulivyo" ambao wakitumwa na nchi yao kufanya kitu wao hukifanya kwa kuboronga kwani wakifanya vizuri wataonekana tofauti!
Hii inanikumbusha mawazo ya baadhi ya vijana wamarekani weusi ambao wanalazimika ku"conform" na maisha yanayowazunguka ili wasionekane tofauti. Wasiposikiliza hip hop wanaonekana "sivyo walivyo"; wasipoitana the "n" word wanaonekana kuwa "sivyo walivyo" na wengine wamefikia mahali kuwa hata darasani wakionekana wanapasua basi wanaonekana sivyo walivyo! Vijana hawa kutokana na udhaifu wa uamuzi wanajikuta wanaanza kukubali kuwa "ndivyo walivyo".
Hivyo utamkuta kijana/binti aliyekuwwa mzuri katika tabia na masomo anapoanza kuact up na kuwa kama "ghetto booties' na "niggers" on the street! Hawa wanakubali kuishi kwa kuikubali stereotype kuwa watu weusi wako hivi au wako vile.
Ndio maana anapotokea mtu kama Dr. Bill Cosby na kuwaambia "you don't have to be the stereotype" watu wanadhani kawatukana; akisema watu weusi wanaweza kuwa tofauti anaonekana anaishushia hadhi nasaba yake!
Ni kwa sababu hiyo basi nakataa, napinga, sikubali, na sikutayari kuambiwa kuwa mtu mweusi "ndivyo alivyo"! Ninayakataa mawazo haya si kwa maneno tu bali pia kwa vitendo. Kwamba nikipata nafasi ya kuwa walipo hawa sitofanywa madudu waliyofanya wao! Lakini si mimi tu na wengine wengi ambao wanafahamu kuwa wanaweza kufanya tofauti!
Sasa aliyekubali kusalimu amri kwenye mawazo hayo ambayo msingi wake ni hisia duni za kitumwa ndiye ambaye hafai kukasimiwa madaraka au hata kupewa madaraka au nafasi yoyote ile kwani hawezi kubadilika.
Ndio maana haya nimeyaita mapambano ya kifikra! fikra dhaifu za kitumwa na zenye chembe ya mabaki ya ukoloni lazima zipingwe na kuoneshwa kuwa ni fikra dhaifu ni fikra za kitumwa na ni fikra zenye lengo la kuondoa utu na uthamani wetu kama wanadamu. Tukikubali kuwa "ndivyo tulivyo" tunakubali kuwa sisi si binadamu kamili na ya kuwa ndani yetu katika nasaba na mbari za wazazi wetu kuna makosa fulani yanayotufanya tuwe duni! Tukikubali kuwa "ndivyo tulivyo" tunakiri kwamba kuchukuliwa kwetu utumwa, kutawaliwa na kunyanyaswa kunakoendelea kufanyika leo hii ni kwa haki kabisa!
Ni lazima tuoneshe kwa vitendo vyetu kuwa "sivyo tulivyo". Hata hivyo endapo madudu yanayoendelea kufanyika katika bara la Afrika yatakuwa ni yale yale; kama matukio ya Kenya, Rwanda, Darfur, Somalia yataendelea kufanyika ni wazi kuwa tunawapa haki watu kutunyoshea vidole na kusema "waafrika ndivyo walivyo".
Kwa hili namshukuru Nyani Ngabu kwa sababu siyo tu amechochea mawazo lakini kwa hakika anatulazimisha tuchague upande. Kwamba tunakubali kuwa sisi ni duni (akiwamo yeye mwenyewe) na ya kuwa hatuwezi, na hatustahili kuweza au tunakataa stereotype hiyo na kuamua kwa dhati kuwa tofauti na bora zaidi. Si kwa sababu ya kuwaiga wengine bali kwa sababu sisi wenyewe kutambua thamani ya tofauti hiyo. Yaani, tusibadilike ili tufanane nao, bali tubadilike ili tushindane nao katika kila kitu kilicho bora!
Vinginevyo, kama vile manong'onezo ya usiku na mguso ambao ni mwiko; tutaanza kuamini maneno hayo kwamba ndivyo tulivyo. Na mwisho baada ya kuchapwa sana tukakubali kuitwa "Toby" na hivyo kukubali kuwa sisi ni mali ya mtu mwingine, na mtu huyo anaweza kuamua hatima yetu!
BINAFSI, SIKO HIVYO! NA SIKO KATIKA KUNDI LA WAAMINIO "NDIVYO TULIVYO".