Jasusi,
1. Tulitawaliwa:- Hii ilitufanya sisi tuwe dependent![...]
Hebu tujadili kidogo hapa. Afrika, Asia, Amerika, hata Ulaya wenyewe kwa wenyewe walitawalana. Na kuna nchi za kiafrika inasemekana wakoloni walishindwa kuwatawala wakalala mbele (Ethiopia, Somalia),lakini na zenyewe hali ndio inatisha zaidi
Au by kutawaliwa, kwa tanganyika km. tunaongelea hata kabla ya 1884? Enzi za wafanyabiashara wa kigeni?
Vilevile, kama ni kutawaliwa kwa Utumwa, waafrika tunalia kila siku na utumwa lakini sio peke yetu tuliofanywa watumwa. Hata race nyingine pia zilichukuana utumwa.
So, Why Africans should be dependent just because of being colonized? Mchango wangu hapa ni kuwa kama kutawaliwa/utumwa kumetuathiri, basi ni kwa sababu ya rangi: watawala na slavemaster wetu hawakuwa weusi kama sisi. Nakumbuka hata kwa wamisionary waliotumwa na papa wakaeneze injili na kubatiza kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu:
- Walioenda Amerika, badala ya kufanya kazi iliyowapeleka, yaani kubatiza, wao wakaanza kwanza na kazi ya kueneza upendo, wakatengeneza watoto na hao wenyeji wa amerika, ndo tunaiona latin amerika ya leo
- Waliokuja Afrika, walifanya tu ile kazi waliyotumwa na papa, yaani kubatiza, wao walisahau upendo; hawakutengeneza watoto na vigoli wakiafrika
Kama colour ilifanya watawala wasieneze 'upendo', basi huenda ni hii colour pia ndio inayotufanya tuwe too much dependent, bila kusahau pia matatizo ya mtu mweusi yanafanana popote alipo, kutoka USA, Brazil, hadi Kimanzichana