Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,705
- 36,154
Hii naileta bila salamu!
Karne ya 17 na 18 wazungu ndipo walipogundua teknolojia nyingi.
Vitu ambavyo wazungu walivumbua Karne ya 17 -18 mpaka sasa Waafrika hatujagundua mithili ya hivyo. Tunapeleka watoto shule Ili waweze kutumia vitu ambavyo wazungu walivumbua miaka zaidi ya 300 nyuma .
Teknolojia ya kamera na picha mgando Wazungu waliigundua miaka karibu mia 4 iliyopita , imeboreshwa na kuboreshwa zaidi na itazidi kuboreshwa lakini sisi kazi yetu ni kuanzisha vyuo vya kufundishana namna ya kutumia.
Ingini za magari/mitambo ziligundulika miaka mingi imepita sisi kazi yetu ni kufungua vyuo vya kufundishana namna ya kuzitumia au kubadilisha kifaa kilichokufa kwenye hiyo engine.
Sasa Waafrika tuwe na kalenda yetu ambayo itatupa mwongozo wa wapi tuanzie.
Leo hii kuna vyuo vya kufundishana namna ya kutengeneza ingini za ndege, kiuhalisia sio kutengeneza bali ni kufanya service na kubadilisha vifaa vidogo vidogo.
Sasa ni vurugu mechi , tumepokea mambo ya Karne ya 21 ambayo kwa uhalisia sisi tuko huko Karne ya 15-16.