Fikra potofu kuhusu watu weusi (Afrika) ambazo sisi wenyewe tunaziamini bila kutafakari kwa kina

Your Friendly Narcissist

JF-Expert Member
Sep 16, 2023
1,302
3,243
Habari wadau wote wa JF

Hakuna kitu kibaya kama kumwacha mtu akufafanue au kukuelezea kama vile ww mwenyew hujijui.
Don't let anyone define you and don't let anyone define your beliefs.

Kuna baadhi ya mambo waafrika tunakua tunajiaminisha na kujilaumu bila kutafakari kama "je haya mambo tunaambiana/tunayoambiwa ni kweli" na hayo mambo tunapenda kusema kuwa ndo chanzo cha maendeleo yetu kuwa hafifu, kweny hii thread ntajaribu kuorodhesha mambo hayo kadri niwezavyo;

Fikra namba moja;
Fikra ya kwamba dini aliyotuletea mzungu ndo inatufanya tuwe hv, kwamba tuwe wavivu, tuwe wanyonge na wengine wanasema watu weusi(waafrika) tunashindwa kugundua vitu kwa sababu tukijiuliza maswali ambayo hatuna majibu tunaishia kusema "mungu anajua".

Je hizi fikra ni za kweli? HAPANA.

Kwanza kabisa unatakiwa kujua kwamba wazungu(wakoloni) hawakuleta dini africa, dini ilikuwepo africa hata kabla ya ukoloni.

Ndio religious beliefs za maeneo mengi hapa africa before colonialism zilikuwa ni imani za ancestor worship(kuomba kwa mizimu ya Babu zetu) na kuamini katika mizimu but kulikuwa kuna maeneo kama Ethiopia walikuwa wanamjua mungu.

Ethiopian Bible ni ya zamani kuliko hata King James Version, Ethiopian Bible ilikuwepo miaka 800 kabla hata ya King James Version na ni moja kati ya biblia za zamani sana(zile za kwanza kwanza kuandikwa) ukiachana na zile za mwanzoni kabisa zilizoandikwa kwa lugha ya kiebrania(agano la kale) na kigiriki(agano jipya).

Hio biblia ilikuwepo Afrika huko Ethiopia na watu walikuwa wanaisoma na kufatisha yaliyoandikwa humo, walimjua mungu na amri zake na jinsi ya kuishi maisha yanayompendeza mungu, sababu iliyofanya waikubali hii dini ni kwa sababu baadhi ya mafundisho yake yalikuwa yakiendana na tamaduni na mila zao.

images - 2023-09-29T171009.713.jpeg

images - 2023-09-29T171055.835.jpeg

Wakoloni hawakuleta dini africa bali walileta madhehebu(ukatoliki, Lutheran, usabato) pia walisaidia kuisambaza sehemu ambazo dini haikufika ila sio kwamba walivokuja africa ndo ilikuwa mara ya kwanza watu wa africa kusikia habari za mungu, HAPANA, Tena kuna baadhi ya maeneo wamisionari walipofikia(ukiachana na Ethiopia) walikutana na watu wanaomjua mungu, ni jambo la kushangaza kwamba walidhani watakuta watu waabudu miti but kulikuwa kuna watu wanamjua mungu na wana practice amri za mungu, ninacho eleza hapa ni mambo ambayo wamisionari wenyew waliokuja africa walikutana nayo na wakastaajabu na kuandika vitabu.

Fikra ya kwamba dini inatufanya tuwe wavivu na wanyonge ni fikra potofu, dini haifundishi hivo ni uelewa tofauti tuu wa mtu na mtu.

Dini inasema plainly kwamba uvivu ni mbaya na uvivu ni dhambi, dini inasisitiza watu kufanya kazi kwa bidii, soma kitabu cha mithali vizurI.

Dini haifundishi unyonge, dini inafundisha tusichochee ugomvi na inafundisha tuwe "wapatanishaji" bali sio kuwa mnyonge, lakini inapokuja situation ambayo inabidi utumue violence ili kujilinda ama kumlinda umpendaye dini inaruhusu, dini inasema muwe "wapole kwa kiasi" haisemi tuwe wanyonge, unapotakuwa kutumia violence kutetea haki zako dini haina kipingamizi katika hilo. DINI SIO FACTOR INAYOSABABISHA UMASKINI WA AFRICA, tuiondoe hii dhana kichwani.

Fikra namba mbili;
Fikra za kwamba watu weusi tuna akili pungufu, hatuna akili ya uvumbuzi, hatuna ubunifu kama wazungu na kwamba wazungu wametuzidi talanta, hizi zote ni fikra potofu sana.

Watu weusi tuna akili nzuri sana hatujazaliwa na RAM ndogo kama wengi tunavofikiria, hizo ni sababu za uongo tunazotafuta ili kujifariji.

Watu weusi tuna akili nzuri tuu ya uvumbuzi na anayesema hatuna mchango wowote kweny science ni muongo, hawa ni waafrica waliofanya major scientific discoveries lakini hawafahamiki;

1. ERASTO MPEMBA-(PHYSICS, TANZANIA)
2. MAMOUN BEHEIRY-(MATHEMATICS, SUDAN)
3. MULALO DOYOYO-(CEMENT, SOUTH AFRICA)
4. PELKINS AJANOAH-(SELFDRIVING CARS, CAMEROON)
5. KWATSI ALABURUHO-(NASA, UGANDA)
6. PAULA KAHUMBU-(CONSERVATION, KENYA)
7. CHEIKH ANTA DIOP-(PHYSICS, SENEGAL)
8. THOMAS ODIAMBO-(ENTOMOLOGY, KENYA)
9. HAILE DEBAS-(MEDICINE, ERITREA)
10. JEAN-JACQUES MUYEMBE-TUMFUM (MEDICINE, CONGO)
11. AHMED MUMIN WARFA-(BOTANY, SOMALIA )
12. ALI SAID FAQI-(TOXICOLOGY, SOMALIA)
13. OSMAN ADEN ABDULLE-(GENETICS, SOMALIA)
14. REDIET ADEBE-(COMPUTER SCIENCE, ETHIOPIA)
15. GIDAY WODE GABRIEL-(ARCHAEOLOGY, ETHIOPIA)
16. SOSINA HAILE-(CHEMISTRY, ETHIOPIA)
17. BENNET OMALU-(NEUROLOGY, NIGERIA)
18. BISI EZERIOHA-(ENGINEERING, NIGERIA
19. DAVIDSON NICOL-(MEDICINE, SIERRA LEONE)
20. CHEICK MODIBO DIARRA-(ASTRONOMY, MALI)

Waafrica tunajipotosha kwa kusema wazungu wametuzidi akili, wengine wanasema wazungu wana majini, wengine wanasema wazungu wanasaidiwa na shetani kugundua mambo vya technology, tusitafute sababu za kujifariji ili kupunguza maumivu ya umaskini.

Fikra kwamba wazungu wametuzidi watu weusi ubunifu kweny sanaa na tumezidiwa talanta na wazungu ni dhana nyingine potofu, tuna watu weusi wengi tuu duniani kote very inspirational people kweny sanaa na wamefanikiwa kupitia talanta zao kama kweny muziki kuna wakina Michael Jackson, Jay-Z, P Diddy, Kanye West, Rihanna, Beyoncé(wengine hapo kama Jay-Z na Rihanna wanashika namba za juu kwa utajiri) ukija kweny basketball(NBA) ndo usiseme watu weusi tumetawala pale all big stars wa NBA are blacks from the past to present day.

Kweny masuala ya ubunifu wa utengenezaji(craftsmanship) tulikuwa tunafanya haya mambo kabla hata ya ukoloni, wakoloni walipokuja walikuta kuna viwanda vidogodogo vya kufua vyuma(uhunzi), walikuta tayar tunafanya mambo kama kutengeneza sculpture, paintings, pottery, ceremonial and religious headgear and dressings.

Africa has a rich tradition of arts and crafts, asije Mtu akakudanganya akasema watu weusi hatuna kitu kichwani, mtu asiyejikubali yeye mwenyew na utamaduni wake ananishangaza sana aisee.

Fikra namba tatu;
Fikra ya kwamba watu weusi tumelaaniwa na kwamba wazungu ni watu special(wao sio kama sisi) nayo ni fikra potofu sana.

Hii fikra inatokana na story ya kweny biblia(mwanzo sura ya 9), soma picha za hapo chini;

Screenshot_20230929_161134_Biblia.jpg

Screenshot_20230929_161206_Biblia.jpg

kwaio sisi ndo uzao wake bhana huyo alielaaniwa, watu weusi tuliolaaniwa tunaotembea na laana za Hamu mtoto wake nuhu, aisee tusijitengenzee viji story vya kutufajiri kwamba umaskini wetu ulisababishwa na malaaniwa ya kipindi hicho ya nuhu na watoto zake.

Hata kama ni kweli huyo Hamu na mtoto wake waliilaaniwa na sisi ndio uzao wake, biblia hiohio inasema laana hazirithishwi, laana ya baba ni ya baba, haiwez kumdhuru mtoto endapo mtoto hataenenda katika njia za baba ake, kitabu cha "kumbukumbu la torati" linaelezea haya mambo vizurI.

Watu weusi HATUJALAANIWA(tungekuwa tuna laana hao wakina LeBron James, Jay-Z na Rihanna wasingekuwa wanafanikiwa hata kama hawapo africa kwa sababu laana inakufata kokote ulipo, but wamefanikiwa na wanaendelea kufanikiwa na ni watu weusi), hii dhana pia ni chanzo cha inferiority complex tuliokuwa nayo, tunawaona wazungu wa maana sana wakati wezi tuu hao wanakuja kuiba vitu africa wanapeleka nchini kwao alaf tunawaona watu wa maana wakati hawana hata malighafi za maana za kuzidi africa, tuiondoe hii dhana vichwani mwetu, tufanye kazi kwa bidii na tupandane.

Fikra namba nne;
Fikra za kwamba africa ni bara maskini ni dhana nyingine potofu. Hakuna bara zuri kama africa, we have a very big good land our land is very intact, but europe hata ukiangalia kweny atlas utaona jinsi lilivyo, bara lao vinatengenezwa na visiwa vingi ndio kuna sehemu ya ardhi ipo intact but sio kama africa, ardhi yao sio intact kama ya kwetu.
Map_of_the_African_Union.svg.png

images - 2023-09-29T163350.830.jpeg

Africa ni bara lililojaa resources nyingi sana. Tuna malighafi za kutosha, tuna madini, tuna wanyama wa kutosha wa kila namna wakufugwa na wa mwituni(hadi wazungu wanatoka huko wanakuja kuwaonea huku) kinachoshangaza sisi wenyew hata hatuwajali tunawapakiza kweny ndege tuu wanapelekwa huko europe sisi hatuna habari.

Dhana ya kwamba africa ni bara masikini naomba tuliondoe vichwani mwetu, bara hili ni tajiri tuache visingizio tufanye kazi na tupendane.

Shida zetu watu weusi;
Shida yetu ya kwanza watu weusi tunajidharau sana, we dont respect ourselves, hatudhamini qualities zetu, tamaduni zetu, ardhi yetu, utu wetu yaan tunajiona kama watu tusiokuwa na dhamani kama wazungu, mwafrika mwenzako anaweza kukudharau kuliko hata mzungu, ni jambo la kuuzunisha sana unategemea support kutoka kwa mwenzako anakuangusha.

Shida yetu nyingine africa hatupendani na tuna unafiki, haya mambo yanaturudisha.
Kama unapenda astronomy na unapenda kufatilia celestial things utagundua kuna mambo mazuri na yakushangaza ambayo mungu ameumba, things like stars, nebulas(a place where stars are born), galaxies and there different forms, black holes, the whole universe is filled with magnificent things utakuja kugundua earth is just a just a very small fraction of the universe, kwaio mambo kama chuki, ubinafsi na roho mbaya ni mambo very minor ukilinganisha na ukuu uliopo ulimwenguni.

Obama na Biden walipokuwa wanafanya kampeni za uraisi walisema hawa support ushoga, cha kushangaza walivoingia madarakani Obama na mwenzake Biden wakabadilika wakawa wana support.

Hawakuishiwa hapo tuu they came to africa, they influenced some africans countries wakubali ndoa ya jinsia moja, mataifa ya africa yakakataa yakasema hamna sisi huku hatuna hayo mambo, those African countries were threatened to be sanctioned(kukata misaada) under Obama's watch, haya ndo matatizo ya watu weusi sasa, Obama ni mtu mweusi his ancestors ni waafrika but anawafanyia hivo ndugu zake waafrika.
Why men fucking other men mean so much to America, that when they refuse to accept same sex marriage you, threaten to sanction them, starve them, that you would your power to starve a baby, starve a woman, just because they want to uphold God's law.

Huu ni ushetani na Obama ndo alikuwa president, angekuwa Biden ningeeelewa kwa sababu hana roots africa, but imetokea under Obama's watch na yeye ana roots africa.

Watu weusi tupendane, tufanye kazi kwa bidii na tupunguze chuki.
Don't let anyone define you and don't let anyone insult your qualities.

Jikubali na usimwamini mtu yeyote akwambia una matatizo au race yako ina matatizo au ancestry yako ina matatizo just because you are African.

Nimeongea vya kutosha, sasa nakaribisha mawazo yenu, pia nakaribisha wale wakosoaji, kila opinion ni muhimu hata iwe negative nitaipokea.

Ni mm Your Friendly Narcissist

Karibuni.....
 
Unajichanganya mwenyewe!

Dini zipi unazungumzi mkuu. Za kushinda kanisani kupata mke, kazi, pesa na miujiza? Zile za mwamposa, mzee wa upako, zamadali zile za kuhubiriana kwenye maeneo ya shughuri za kazi , kwenye magari sokoni.🤣🤣. Kwa mantiki hiyo kwanini dini isiwe chanzo cha umasiki.


Uafrika hauna ustarabu kabisa.
Tazama choo za umma utaelewa kwanini sisi tupo hivi.
Tazama mtu akipewa madaraka akipata pesa, akisoma, kwa ufupi waafrika tuna urimbukeni mwingi, hatufai kwa jamii iliyostarabika.

Hata misaada tunayopewa kwa lengo la kuleta maendeleo bado misaada inapigwa.ubinafsi kwa sana.

Mkopeshe pesa mwafrika uone kila rangi. Sio waaminifu kabisa kwa vitu au Muda.

HOJA YA KUMTETEA MWAFRIKA SIIONI..
 
Waafrika ni wala rushwa wakubwa sana.

Waafrika hawajitambui.

Wabinafsi.

Kuna mla rushwa na mwizi mmoja atakuja kunipinga hapa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom