Sisi watanzania bado tuko nyuma sana ya muda

Kinumbo

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
3,189
Reaction score
5,819
Sio jambo la kufurahisha wala kufurahia kwa hali tuliyo kuwa nayo kiujumla, kuanzia namna ya tunavyo ishi kila siku. Dunia ya sana iko mbali na kwa haraka sana ila sisi watanzania tunaonekana bado sana ama hatuko tayari kwenda vile dunia iliko fika ama inako elekea. Inashangaza sana

Napenda tujadili kuhusu teknolojia, teknolojia inaonekana kwetu sisi bado tuko nyuma sana tofauti na mataifa mengine.

Staili ya maisha tunayo ishi imetufanya tudumae kimawazo hasa katika kutatua matatizo. Leo hii hapa Tanzania asilimia kubwa ya wananchi mitaani mpaka maofisini wanazungumza ama kujadili mambo yasio na mantiki yoyote ile katika dunia ya sasa.

Unakuta asilimia kubwa ya wananchi kuanzia asubuhi mpka muda wa kulala ni kupigizana kelele na mambo ya usimba na uyanga, siasa, wanawake na umbea tu.

Kweli kwa dunia tunayoilekea bado tunajadili ujinga kama huo? Yaani tunakaa na kupoteza muda wakati wenzetu huko wanafanya makubwa kila uchwao sisi tumebaki na kejeli za kijinga huko mitandaoni.

Wapo watano sema Serikali ndio imetufikisha hapa, naam kwa asilimia kubwa ni wao na hii ni kutokana kuwepo kwa sera mbovu hasa katika sekta ya elimu.

Hawa jamaa wanajiita viongozi hawana huruma kabisa na sisi wao wanajiangalia wenyewe tu, tuachane na hao jamaa maana hawana msaada wowote kwetu.

Nauliza sisi kama sisi tumechukua hatua ipi?

Duniani kumetokea mapinduzi makubwa mno ya teknolojia ila sisi hatujui tuko wapi na tunaelekea wapi. Leo hii huko China wana barabara inapita chini ya maji ila sisi kurusha tu satellite tumeshindwa wakati Kenya na Rwanda wamemeza.

Wapo watakao sema usilinganishe China na Tanzania, naam ni sahihi kabisa ila huoni taifa lako lina rasilimali nyingi kuliko hiyo China, sasa jiulize wamefanya nn mpaka wakupite. Akili mtu wangu

Leo hii kuna ishu ya Cryptocurrency, hii kitu nadhani kwa asilimia kubwa wengi wameisikia ama kuifahamu kabisa.

Cryptocurrency hii itakuja kuwa mapinduzi makubwa kwenye masuala ya kifedha hapo baadaye, je ni wangapi wana ufahamu kuhusu hii kitu na wako tayari?

Sisi Watanzania tumekalia mambo ya kipumbavu na kuacha mambo ya msingi, hatujifunzi vitu vipya wala ata kusoma vitabu hatutaki tupo tupo tu yaani inauma sana.

Sisi watanzania tunaelewa kwamba ukimaliza kidato cha nne ama ukifika chuo kikuu baasi umemaliza kila kitu hatutaki tena kujifunza ama kupanua mawazo yetu.

Sipo hapa kuongelea habari za Cryptocurrency ila nitatolea mfano tu. Wapo wadau mbalimbali wameleta mada kuhusu hii kitu lakini matokeo yake wakaitwa matapeli hii inaonyesha ni kiasi gani baadhi ya sisi watanzania hatuko tayari kujifunza, kujifanya tunajua na kupinga kumbe ujinga tu.

Niliwahi kutana na maneno mazuri sana katika moja ya kitabu cha mwandishi Robert Kiyosaki nanukuu "The most successful people in the world are the most rejected people in the world". Sisi watanzania tumekalia kupinga, kejeli na kuto kutaka kujifunza.

Unapinga Cryptocurrency wakati huo huo unatumia internet kwa miaka ya nyuma ilikuwa ngumu kuelewa ama kuamini ishu ya internet leo hii tunaitumia.

Nini kinakufanya usiamini Cryptocurrency wakati hayo ni matokeo ya teknolojia, vipo vingi vitakuja kwenye masuala ya teknolojia.

Mwenyezi Mungu ametujalia akili ili itumike kutatua matatizo yetu sio kupinga na kujadili masuala yasio na manufaa kwetu sisi kwa sasa na hapo baadaye.

Yapo mengi ya kuyaandika ila nisiwachoshe ila tujitahidi kuwa tayari kwa mabadiliko ya dunia. Tutumie akili zetu kutatua changamoto zinazotukabili na pia tuwe tayari kujifunza sio kila kitu ni ubishi tu, asanteni.
 
Sio jambo la kufurahisha wala kufurahia kwa hali tuliyo kuwa nayo kiujumla, kuanzia namna ya tunavyo ishi kila siku. Dunia ya sana iko mbali na kwa haraka sana ila sisi watanzania tunaonekana bado sana ama hatuko tayari kwenda vile dunia iliko fika ama inako elekea. Inashangaza sana

Napenda tujadili kuhusu teknolojia, teknolojia inaonekana kwetu sisi bado tuko nyuma sana tofauti na mataifa mengine.

Staili ya maisha tunayo ishi imetufanya tudumae kimawazo hasa katika kutatua matatizo. Leo hii hapa Tanzania asilimia kubwa ya wananchi mitaani mpaka maofisini wanazungumza ama kujadili mambo yasio na mantiki yoyote ile katika dunia ya sasa.

Unakuta asilimia kubwa ya wananchi kuanzia asubuhi mpka muda wa kulala ni kupigizana kelele na mambo ya usimba na uyanga, siasa, wanawake na umbea tu.

Kweli kwa dunia tunayoilekea bado tunajadili ujinga kama huo.!? Yaani tunakaa na kupoteza muda wakati wenzetu huko wanafanya makubwa kila uchwao sisi tumebaki na kejeli za kijinga huko mitandaoni.

Wapo watano sema Serikali ndio imetufikisha hapa, naam kwa asilimia kubwa ni wao na hii ni kutokana kuwepo kwa sera mbovu hasa katika sekta ya elimu.

Hawa jamaa wanajiita viongozi hawana huruma kabisa na sisi wao wanajiangalia wenyewe tu, tuachane na hao jamaa maana hawana msaada wowote kwetu.

Nauliza sisi kama sisi tumechukua hatua ipi?

Duniani kumetokea mapinduzi makubwa mno ya teknolojia ila sisi hatujui tuko wapi na tunaelekea wapi. Leo hii huko China wana barabara inapita chini ya maji ila sisi kurusha tu satellite tumeshindwa wakati Kenya na Rwanda wamemeza.

Wapo watakao sema usilinganishe China na Tanzania, naam ni sahihi kabisa ila huoni taifa lako lina rasilimali nyingi kuliko hiyo China, sasa jiulize wamefanya nn mpaka wakupite. Akili mtu wangu

Leo hii kuna ishu ya Cryptocurrency, hii kitu nadhani kwa asilimia kubwa wengi wameisikia ama kuifahamu kabisa.

Cryptocurrency hii itakuja kuwa mapinduzi makubwa kwenye masuala ya kifedha hapo baadaye, je ni wangapi wana ufahamu kuhusu hii kitu na wako tayari?

Sisi watanzania tumekalia mambo ya kipumbavu na kuacha mambo ya msingi, hatujifunzi vitu vipya wala ata kusoma vitabu hatutaki tupo tupo tu yaani inauma sana.

Barikiwa sana mkuu naomba nipe dondoo za hiyo cryptocurency NAITAJI kuwekeza uko mkuu
 
Mtu asiye jali muda hana tofauti na mfu
Ndio maana wakenya wanatuita wadanganyika
Hata viongozi wanajua sisi ni mradi liende
 
Bas ka ndo hivyo barca madrid liver zisngekuwepo na unajua jins gan mbele wanawekeza kwa michezo sasa wote tukjadili technology na unaona uchumi wetu hata madarasa shida nijadili barbara chin ya maji wakati ya kawaida tu bado sana acha watu waburudike we fikiri ya uwezi wako
 
Naam, sahihi kabisa mkuu. Hawa viongozi wao ndio chanzo kikubwa cha Taifa letu kuwa hivi wakati huo huo wanatuona sisi ni imladi tu. Inauma sana

Muda ni ishu pana sana ila tunaichukulia poa tu
Mtu asiye jali muda hana tofauti na mfu
Ndio maana wakenya wanatuita wadanganyika
Hata viongozi wanajua sisi ni mradi liende
 
Sawa broo
Satelite ya rwanda unajua imetengenezwa kwa collabo na nani? Ni kasatelite tu kale...
Raisi mbona jambo la crypto alishalisemea, ila kwasasa naona kuna wehu kwenye haya mambo ya blockchain, kila mwenye uwezo na nyenzo anaanzisha crypto yake, mataifa mengine yanaipinga mpaka kutengeneza sheria kabisa, mengine yanaikubali, mengine yanaamua kuja na ya kwao ya kiserikali.
Bado mara NFTs naona nao ni kama wehu flani, hujakaa sawa eti watu wananunua viwanja kwenye metaverse kwa millions of dollars.
Mimi naona ni kama wehu bado watu wanahangaika kutafta njia za kumonetize web 3. Huu wehu pia ulikuwepo wakati internet inaanza especially in the early 2000s watu walikuwa wanahangaika wakiona internet ni kitu kizuri but how can they monetize it. Kwenye hili na lile ndo mengine yakafail mengine yakatoboa.
Ila hata mimi naona cryptos ndo the future of money.
Blockchain ni kitu bora sana kwa karne hii.
 
Yaani unawasema Watanzania kisa Crypto wakati unajua kabisawengi wao hata hizo smartphones hawana.

Waliojisajili na Huduma za kifedha za kibenki ni wachache.

Ingefaa ungetoa tuu elimu Kwa wenye ulewa lakini kuwakumuisha watu wanaohangaika wapate walau mlo mmoja Kwa siku utakuwa unawaonea
 
Mambo mengi tunayachukua kama yalivyo huko duniani tunayaleta hapa na hayafaulu sana. Ndiyo maana huduma za mobile money kama Mpesa zilizaliwa Afrika hapo kenya zikiwa zimelenga uhalisia wa mwafrika na hali na maisha yake, na ndiyo maana mobile money imefaulu sana Afrika. Sasa hivi karibu Afrika nzima imechukua hii teknolojia ya kutuma na kupokea pesa.
Hata huko bush hata wasiojua kusoma na kuandika mobile money imewafikia.
 
Umeongea point sana, nmekuwa nashangaa hata suala la technologies za kutunza na kufanya malipo ya pesa mitandaoni bado nchi ipo nyuma sana.

Yaan ukiongelea mambo ya cryptocurrency, paypal kwa vijana wa Tz wanaisi ni utapeli na uzushi, kumbe ktk nchi za wenzetu waliofungua akili zao wanafaidika na wanauelewa mkubwa sana kuhusu haya mambo.

Mm pia mmekuwa nkiteseka kuhusu uhamishaji wa fedha mitandaoni sabbu ya nchi yetu kuwa nyuma kimawazo kwa kutoruhusu baazi ya hizi mambo zisifanye kazi kwa sababu wanazojuwa wanasiasa na viongoz wapuuzi.

Inasikitisha kwakwel, mtu ukifanikiwa kutembelea nchi za wenzetu then uka compare the way wanavyozidi kuchanja mbuga, utaionea sana huruma hii nchi yenye maono hafifu na upumbavu wa kila aina.

Nilishangaa pia kuwaona wale watanzania waliokuwa wakiicomplain china kwa kuunda artificial sun(jua), ambalo litakuwa likiimulika nchi yao, sas hawa wapuuzi wa kitanzania kwa maoni yao na mawazo yao ukiwasikia utawaonea huruma sana jinsi gan walvyo na mindset za kitoto, eti china inamkufuru Mungu sjui ili mala lile, yaan ni ujinga mtupu.

Hii nchi ni mzigo sana yaani

Tunatia aibu yaan kuna baazi ya mambo ya msingi sana hata ukitaka kupata jawabu ukiwauliza waTz mahala popote pale, hutopata jibu, maana wengi uelewa mdogo sana, na hata wale wanaojuwa hawataki kufanya wepesi kwa hawa wasiojua.
 
Sio jambo la kufurahisha wala kufurahia kwa hali tuliyo kuwa nayo kiujumla, kuanzia namna ya tunavyo ishi kila siku. Dunia ya sana iko mbali na kwa haraka sana ila sisi watanzania tunaonekana bado sana ama hatuko tayari kwenda vile dunia iliko fika ama inako elekea. Inashangaza sana

Napenda tujadili kuhusu teknolojia, teknolojia inaonekana kwetu sisi bado tuko nyuma sana tofauti na mataifa mengine.

Staili ya maisha tunayo ishi imetufanya tudumae kimawazo hasa katika kutatua matatizo. Leo hii hapa Tanzania asilimia kubwa ya wananchi mitaani mpaka maofisini wanazungumza ama kujadili mambo yasio na mantiki yoyote ile katika dunia ya sasa.

Unakuta asilimia kubwa ya wananchi kuanzia asubuhi mpka muda wa kulala ni kupigizana kelele na mambo ya usimba na uyanga, siasa, wanawake na umbea tu.

Kweli kwa dunia tunayoilekea bado tunajadili ujinga kama huo.!? Yaani tunakaa na kupoteza muda wakati wenzetu huko wanafanya makubwa kila uchwao sisi tumebaki na kejeli za kijinga huko mitandaoni.

Wapo watano sema Serikali ndio imetufikisha hapa, naam kwa asilimia kubwa ni wao na hii ni kutokana kuwepo kwa sera mbovu hasa katika sekta ya elimu.

Hawa jamaa wanajiita viongozi hawana huruma kabisa na sisi wao wanajiangalia wenyewe tu, tuachane na hao jamaa maana hawana msaada wowote kwetu.

Nauliza sisi kama sisi tumechukua hatua ipi?

Duniani kumetokea mapinduzi makubwa mno ya teknolojia ila sisi hatujui tuko wapi na tunaelekea wapi. Leo hii huko China wana barabara inapita chini ya maji ila sisi kurusha tu satellite tumeshindwa wakati Kenya na Rwanda wamemeza.

Wapo watakao sema usilinganishe China na Tanzania, naam ni sahihi kabisa ila huoni taifa lako lina rasilimali nyingi kuliko hiyo China, sasa jiulize wamefanya nn mpaka wakupite. Akili mtu wangu

Leo hii kuna ishu ya Cryptocurrency, hii kitu nadhani kwa asilimia kubwa wengi wameisikia ama kuifahamu kabisa.

Cryptocurrency hii itakuja kuwa mapinduzi makubwa kwenye masuala ya kifedha hapo baadaye, je ni wangapi wana ufahamu kuhusu hii kitu na wako tayari?

Sisi watanzania tumekalia mambo ya kipumbavu na kuacha mambo ya msingi, hatujifunzi vitu vipya wala ata kusoma vitabu hatutaki tupo tupo tu yaani inauma sana.

Sisi watanzania tunaelewa kwamba ukimaliza kidato cha nne ama ukifika chuo kikuu baasi umemaliza kila kitu hatutaki tena kujifunza ama kupanua mawazo yetu.

Sipo hapa kuongelea habari za Cryptocurrency ila nitatolea mfano tu. Wapo wadau mbalimbali wameleta mada kuhusu hii kitu lakini matokeo yake wakaitwa matapeli hii inaonyesha ni kiasi gani baadhi ya sisi watanzania hatuko tayari kujifunza, kujifanya tunajua na kupinga kumbe ujinga tu.

Niliwahi kutana na maneno mazuri sana katika moja ya kitabu cha mwandishi Robert Kiyosaki nanukuu "The most successful people in the world are the most rejected people in the world". Sisi watanzania tumekalia kupinga, kejeli na kuto kutaka kujifunza.

Unapinga Cryptocurrency wakati huo huo unatumia internet kwa miaka ya nyuma ilikuwa ngumu kuelewa ama kuamini ishu ya internet leo hii tunaitumia.

Nini kinakufanya usiamini Cryptocurrency wakati hayo ni matokeo ya teknolojia, vipo vingi vitakuja kwenye masuala ya teknolojia.

Mwenyezi Mungu ametujalia akili ili itumike kutatua matatizo yetu sio kupinga na kujadili masuala yasio na manufaa kwetu sisi kwa sasa na hapo baadaye.

Yapo mengi ya kuyaandika ila nisiwachoshe ila tujitahidi kuwa tayari kwa mabadiliko ya dunia. Tutumie akili zetu kutatua changamoto zinazotukabili na pia tuwe tayari kujifunza sio kila kitu ni ubishi tu, asanteni.
Umeongea point.
 
Najua lengo lako lililenga Cryptocurrency ila kitu ulicho sahau ni kuwa uwelewa sahihi juu ya jambo unalilidhungumzia watu wengi hawana.
Punguza michambo toa elimu kwanza juu ya hilo jambo, watu wajue uhalisia wake, usalama wake, nan vip atapa faida sio kuanza kama ulivyoanza
 
Hawa watu wana mbwembwe sana ... Kama cryptocurrency ina hela kuna haja gan ya kusanua wengine? Si wapige hela kimya kimya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom