Wa mwisho ndiyo mshindi

Utakuta mtu huyo ndiye anaeharibu mtiririko Wa Uzi Kule sie twaendelea mwambie arejee tena kule aone tunavyotiririka
 
Sasa mkuu si ungeumalizia kule kule?

Mchezo umechezwa Taifa, eti kipenga cha kumaliza mchezo kimepigwa Kirumba!

Nilijua wachangiaji wengine wangeificha post yangu kwa kurudi tena nyuma, kitu ambacho tayari kimetokea. Hivyo nikaona niliweke wazi kabisaaa kwamba mchezo umekwisha. Zaidi ya hapo mtu kaamua kulazimisha mambo kama uchaguzi wa uraisi kisiwani.
 
Kimepigwa Kirumba na mchezo haukwisha maana kabla filimbi haijalia refa kajikwaa filimbi ikadondoka hivyo bado tunaendelea na mchezo
 
tu ndo nini sasa, hebu wewe anzisha sentensi tuone
 
tu ndo nini sasa, hebu wewe anzisha sentensi tuone

Mkuu hukusoma kiswahili nini? "Tu"ni kivumishi kinachotoa msisitizo juu ya neno linalotangulia, kwa mfano, "weka matone matatu tu", au "NI wale tu walio na kadi cha chama chetu ndio watafanikiwa kibisahara".

Hivyo nikiuliza "Ulaya tu?" ina maana hakuna nchi nyingine ambako vinyago vinauzwa bei mbaya?

Au unaweza kusema "Hapa kazi tu"
 
Hapa kazi tu ni kauli mbiu iliyotikisa Afrika hadi kufikia matangazo ya biashara
 
hahaa, ile gemu haiwezi pata mshindi kwa kua haina refa, labda tumwombe moderator mmoja awe refa, kuna jamaa alimalizia kwa kichina ila bado wakakichakachua!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…