figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,713
- 55,786
Salaam Wakuu,
Nimeanzisha uzi huu ili tushikamane kama Watanzania kutafuta au kutoa taarifa ya watu waliopote. Kumeibuka wimbi la Watu wa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
Rais ndo Mwenyekiti wa kwanza wa usalama, kupitia thread hii ataweza kujua ni kiasi gani watu wanapotea bila hatua zozote kuchukuliwa.
Pili nashauri Polisi kama kuna mtu wamemkamata, watoe taarifa mapema kwa ndugu na jamii ili wajue yupo Mikono salama. Hapa chini naweka baadhi ya watu ambao wamepotea, post zao au Malalamiko ya ndugu zao.
Hivyo usikalie kimya hili tatizo la watu kupotea. Tujulishane ili Mamlaka zione tatizo lilivyo kubwa.
Karibuni.
Pia soma ===>>> Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati
PIA SOMA
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Nimeanzisha uzi huu ili tushikamane kama Watanzania kutafuta au kutoa taarifa ya watu waliopote. Kumeibuka wimbi la Watu wa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
Rais ndo Mwenyekiti wa kwanza wa usalama, kupitia thread hii ataweza kujua ni kiasi gani watu wanapotea bila hatua zozote kuchukuliwa.
Pili nashauri Polisi kama kuna mtu wamemkamata, watoe taarifa mapema kwa ndugu na jamii ili wajue yupo Mikono salama. Hapa chini naweka baadhi ya watu ambao wamepotea, post zao au Malalamiko ya ndugu zao.
Hivyo usikalie kimya hili tatizo la watu kupotea. Tujulishane ili Mamlaka zione tatizo lilivyo kubwa.
Karibuni.
Pia soma ===>>> Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati
=====
BAADHI YA MICHANGO YENYE TAARIFA ZA KINA KUHUSU ORODHA YA WATU WALIOPOTEA
BAADHI YA MICHANGO YENYE TAARIFA ZA KINA KUHUSU ORODHA YA WATU WALIOPOTEA
Kwa kujibu wa ukurasa rasmi wa X (zamani Twitter) wa Maria Sarungi Tsehai, idadi ya raia wanaopotea ama kutekwa inazidi kuongezeka siku hadi siku kiasi cha kuzua taharuki miongoni kwa Watanzania. Taarifa za ndugu wa wanaopotea huwa zinatolewa vituo mbalimbali vya polisi, na kuna wakati juhudi za kuwapata wanaopotea zinagonga mwamba kabisa. Hapa chini ni baadhi ya majina ya waliopotea na/au kupatikana, kwa mujibu wa ukursa huo wa Maria Sarungi, kadri alivyokusanya kutoka vyanzo mbalimbali, kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka huu 2024.
WALIOTEKWA 2021 - 2024
(ISIPOKUWA 1. & 2. )
Hii orodha inajumuisha waliotekwa na waliopatikana na pia ambao hawajapatikana.
Kama kuna mtu una taarifa yake kutekwa 2021 - 2024 na humwoni katika orodha wasiliana nasi DM:
- Mr Thomas Mungo Ihuya- Alikuwa anafanya kazi mahakama kuu Mwanza alipotea tangu March 2018 mpaka leo hajapatikana
- Dennis Kantanga- Alitekwa sasa ni zaidi ya miaka 4 hajawahi kupatikana wala kusikika. Alikuwa akiitwa Dennis Kantanga alikuwa mkazi wa shinyanga mjini na alikuwa akifanya shughuli za tehama kwa maana ya kutengeneza na kuuza computers, desktop pamoja na laptops na vifaa vingine vya technolojia ikiwepo cctv's. Siku anachukuliwa alifatwa dukani kwake na watu wawili au zaidi lakini waliofika dukani walikuwa wawili na kujitambulisha askari waliondoka kwa gari yake mwenyewe(Dennis) na ikawa mwisho wa kusikikika kwake. Katika utaratibu wa kureport polisi na kutrack simu ilionekana simu yake iliwashwa Musoma na baada ya hapo haikupatikana tena. Gari yake ilikuja kupatikana maeneo ya nzega ikiwa imeegeshwa katikati ya mji baada ya wiki moja or so.
- Abdallah Salumu Msangi - Alipotea Iringa mwishoni mwa mwezi july 2021 na hajapatikana mpaka leo. Kazi yake alikuwa lecturer chuo cha Mkwawa tawi la UDSM.
- Joseph Mnyonga - Alitekwa july 2021 nyumbani kwake Mwanza na watu waliojitambulisha kuwa ni askari polisi kutoka mkoa wa Mwanza mpaka sasa hajapatikana.
- Mzee Haji Soft - Alikuja kuchukuliwa kibarazani kwake alipokuwa amekaa, ilikuja gari ikisema kuwa wao ni mapolisi, toka hapo hakuonekana tena mpaka leo, tumetafta sanaa...ikiwemo polisi, mortuary mpaka kwa waganga
- James Sije - Alitekwa na askari polisi anayeitwa sgt. Mageni Musobi A.K.A Majani wa kituo cha polisi nyakato 17 Aug.2021 mpaka sasa hajapatikana.
- Tawfiq Mohamed - Alitekwa Kariakoo 26th Dec.2021 eneo la Kamata akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana
- Self Swala - Alitekwa Kariakoo 26th Dec.2021 eneo la Kamata akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana
- Edwin Kunambi - Alitekwa Kariakoo 26th Dec.2021 eneo la Kamata akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana
- Hemed Abass - Alitekwa Kariakoo 26th Dec.2021 eneo la Kamata akiwa na wezake watano. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana
- Rajabu Mdoe - Alitekwa Kariakoo 26th Dec.2021 eneo la Kamata akiwa na wezake watano. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana
- Alphone Bilasenge - Alitoweka ghafla. Simu yake mara ya mwisho ilizimiwa kibeta Bukoba mjini (Kagera)
- Albert Kiseya Selembo - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Moloimeti Yohana Saing'eu- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Ndirango Senge Laizer- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Joel Clemes Lessonu - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Simoni Nairiam Orosikiria - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Damiani Rago Laiza - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Mathew Eliakimu Siloma - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Lukas Kursas Njausi - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Taleng'o Twambei Leshoko - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Kijoolu Kakey Olojiloji - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Shengena Joseph Killel- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Maseke Mwita Maseke - Aliondoka nyumbani TARIME - Nkerege mwaka 2022 kwenda Geita akawa anakaa Geita kimakazi kujishughulisha na kazi ndogo ndgo kwa zaidi ya miezi 6 na aliweza kuwa anarudi hata nyumbani Tarime kusalimia baada hapo simu yake haikuwahi kupatikana ,jitihada za kumtafuta kwenye vituo vya police& hospital vimegonga mwamba maana hazijazaa matunda.
- Molongo Daniel Paschal - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Simeli Parmwati Karongoi - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Lekayoko Parmwati Sirkoti- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Sapati Parmwati Sirkoti - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Alituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi..
- Ingoi Olkedenyi Kanjwel - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Sangau Morongeti Ngiminisi - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Morijoi Ngoisa Parmati- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Morongeti Meeki Masako - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Kambatai Lulu- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Orias Oleng'iyo- Ni mzee wa makamo sana. Aliumizwa wakati vikosi vya usalama vilitumia risasi dhidi ya wakazi wa Loliondo. Alichukuliwa na watu wanaoaminiwa kuwa sehemu ya vikosi vya usalama na hajaonekana tena.
- Wilson Kolong- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- James Taki- Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Joseph Jartan - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi.
- Kelvin Shaso Nairoti - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Lekerenga Koyee Orodo - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Fred Victor Ledidi - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Simon Morintant - Alikamatwa wakati serikali ilianza kuhamisha wananchi kwa nguvu kwa kutumia silaha kutoka vijiji vya Loliondo. Aliituhumiwa na shtaka la mauaji. Alitekwa na kutoweka baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na hatimaye kuachiwa baada ya mashtaka kukosa ushahidi.
- Dotto Kabwa - Alitekwa 4th july 2022 na askari polisi anayejulikana kwa jina la Wambura Mwita kutoka kituo cha polisi Ifunda Iringa na hajapatikana mpaka leo.
- Chande Kizega- Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi 18th Aug.2022 akiwa dukani kwake Machinga Complex. Mpaka sasa hajapatikana.
- Yahya Ally - Alitekwa 6th Sept.2022 Mbagala Kizuiani na askari polisi wakiongozwa na OCCID Abdalah Suleiman. Mpaka sasa hajapatikana.
- Mzee Samwel Matiko Mkongo - Alitekwa Geita 27th Jan.2023 na askari polisi sgt. Hamis mwenye namba 0789938835 na kupelekwa kituo cha Muriaza –Butiama – Mara. Ndugu walifika hapo na wakamuona akiwa ametapakaa majeraha, lakini waliporudi kumletea chakula hawakumkuta tena kituoni hapo na hajaonekana mpaka leo. Tarehe 23 Machi 2023 tulitaarifiwa kuwa DCI alifika Mkoani Geita kushughulikia jambo hilo. Tarehe 24 Machi 2023 tukataarifiwa kuwa DCI ameunda timu na ilihoji ndugu wa Samwel.Kuna taarifa askari waliomteka Mzee Samweli Matiko Mkongo wamekamatwa akiwemo Sgt. Hamisi. Sgt. Hamisi analalamika kuwekwa lock up wachache wakati kwenye jambo hilo wako wengi. Anadai kuwa taskforce ya kuteka watu wasumbufu katika mikoa ya Geita na Mara iliundwa na wakubwa. Analalamika kwa nini wakubwa wanahojiwa wakiwa nje? Anajiuliza ni kwa nini Tume ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) imewang'ang'ania wao tu.
- Aziz Kinyonga - Alipotea mwaka jana mwez wa pili, hadi anapotea alikuwa akiishi chamaz dar es salaam na mkewe n watoto wawili, Gar yake ilikutwa imetelekezwa maporini Mtwara, siku anapotea usiku mkewe alimpigia simu ilipokelewa ila alikuwa anasikia mabishano na mumewe na mwanamke simu ilivyokatwa hadi leo hajapatikana zaid ya mwaka, kwa mujibu wa mkewe walikuja askar kukagua nyumba hawakupata walichotaka waliulizia kama ana miliki silaha anapohifadh, walikuta laki 2 askar wakapita nayo wakasepa, ikaja tena Noah tinted ikashusha kioo mkono ukapoint nyumba hakumfahamu km ni mumewe au nan maana kilishushwa nusu, baada ya hapo wamehangaika mochwar zote hadi vituo vya polis hawajampata, gar walimwambia apeleke laki 5 ili wampatie mkewe kule kituoni, familia imekata tamaa hadi leo.
- Mohamed Mayengo Kalebela - Walikatwa jumla watu 6 wa maeneo ya katoro mwaka 2023 mwezi wa 4 tarehe 5 na tukatafuta vituo vyote vya mkoa wa geita na mwanza bila mafanikio hadi Leo hawajulikani kama wapo au wamekufa na hakuna ilyerudi kwake.
- DEUSDEDITH SOKA - Alitekwa maeneo ya Kinondoni Studio Asubuhi saa 7:00 Asubuhi na kupelekwa garage ya Ostarbay Polisi, baada ya muda mchache kelele zikawa nyingi ndipo wakampeleka kituoni japo hawakumsajili hadi ilipofika jioni.
- Amon Mrimi Magige - walikuja na defender mbili wakamchukua nyakato Mwanza, tangu mwezi wa kumi mwaka Jana mpaka sasa haijulikani alipo imeshakuwa historia.
- Jerome Kisoka a.k.a Mapii - Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi 14th Nov.2023 Njoro-Moshi na hajapatikana mpaka leo.
- Benson E.A. Ishungisa - Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi 26th Novemba 2023 akiwa nje ya Hospital ya Makangarawe Yombo . Benson alikuwa akimsubiria abiria nje ya hospital hiyo na hata bodaboda wenzake walipoulizwa kituo cha polisi anachopelekwa hawakujibiwa. Mpaka leo hajapatikana.
- Charles Aden Mwampyate - Alitoweka tangu 7th Dec.2023 akiwa Dar es Salaam na hajapatikana mpaka le0.
- Mussa Venerable Mziba - Alitekwa Disemba 7 2023 alipokuwa ofisni kwake, walikuja watu waliojitambulisha kama polisi na kumwita nje ya uzio wa geti na kuondoka naye. Musa ni mfanyabiashara wa madini na alikuwa amekwisharipoti polisi kesi ya kusumbuliwa na mshindani wake wa kibiashara na polisi wengine. Hadi sasa simu yake imezimwa na familia haina taarifa zake.
- Hamza Said - Katibu wa chama cha NCCR Mageuzi mkoa wa Geita. Alitekwa 17th Dec.2023 nyumbani kwake mtaa wa Mwatulole – Geita na watu waliojitambulisha ni askari polisi. Mpaka leo katibu huyo hajapatikana.
- William Herman - Alitekwa Mwanza 1st Jan.2024 na askari polisi anayefahamika kwa jina la sgt. Mageni Musobi A.K.A Majani wa kituo cha polisi Nyakato.
- Yonzo Shimbi Dutu- Alitekwa 2 Machi 2024 na askari polisi wa kituo cha polisi Kwimba Mwanza akiwa na wenzake maeneo ya Bushini-Kishapu Shinyanga. Wenzake waliachiwa ila yeye hajapatikana na hayupo vituo vyote vya polisi.
- Abdulrazak Mohamedi- Alikamatwa na Polisi huko Mkoa wa Ruvuma wilaya ya Tunduru tangu tarehe 07 March 2024 kwa tuhuma za ugaidi.Cha ajabu Ndugu walipoenda kituo cha polisi cha Tunduru mjini kwa OCD kuulizia ndugu hawakumkuta na polisi wanasema hawajamkamata wao. Ndugu wakasema “kama hamjamkamata basi tufungue shauri la ndugu yetu kupotea” polisi wakakataa wakatufukuza na kuwaambia wakamtafute ndugu yao kwingine. Baadae ndugu wamefuatilia hadi kwa RPC wa Ruvuma ndo wakafungua kesi ya kupotea. LAKINI Alikamatwa na polisi maeneo ya Cross road Tunduru mjini mchana kweupe, watu kibao walishuhudia tukio hilo. Hadi hajapatikana
- 58DEUSDEDITH SOKA - Alitekwa 12 March 2024 nyumbani saa kumi usiku na badae kupelekwa kwenye Godown na kupigwa na kuumizwa sehemu ya jicho, na mgongoni. Aliachiwa baadaye.
- David Gaspar Lema - Alitekwa 6 Aprili 2024 Baada ya kelele nyingi kwenye mtandao aliachiwa.
- Yusuph Dudu - Alitekwa tarehe 9 April mwaka 2024 mpaka sasa hajulikani alipo. Siku ya tukio wanaume wawili walikwenda nyumbani kwake wakiwa na silaha mida ya saa moja usiku wakagonga mlango akafungua mtoto wake wa kiume mwenye miaka 8 wakamwambia amwite baba yake. Yusuph alivyofika mlangoni wakamwambia awafate nje wana mazungumzo nae. Baada ya Yusuph kutoka nje kuwafata hatua kadhaa kutoka kwenye nyumba yake walitokea watu wengine wanane wakiwa na silaha. Walitembea mpaka yalipokuwa magari yao wakamchukua Yusuph na kuondoka nae na tangu siku hiyo mpaka leo hajarudi nyumbani na hajulikani alipo. Taarifa ya kutekwa kwa Yusuph imeripotiwa katika kituo cha Polisi Mbagala maturubai kupewa RB yenye namba MBL/RB/2891/2024. Yusuph alikuwa anafanya kazi katika bank ya Habib iliyopo stesheni dar. Yoyote atakae pata taarifa zake atoe taarifa kituo cha polisi kilichopo karibu nae au awasiliane na namba 0676125590 au 0717699898.
- Kennedy Mwamlima- Alitekwa Mbeya na watu waliojitambulisha ni askari polisi 11 April 2024. Alipatikana Igunga Tabora 16th April 2024 akiwa ametapakaa majeraha. Kwa maelezo yake alikuwa akiteswa katika vituo vya polisi na alikuwa akiulizwa nani anamtuma kukosoa serikali katika mtandao wa TikTok.
- Kastory Kapinga - mwanafunzi wa Saint Augustine University of Tanzania . Arusha Centre mwaka wa tatu Alitekwa Mbinga, Ruvuma Ghafla alitoweka na chuo hakuonekana geto lake lilikuwa limefungwa. Takribani miezi miwili sasa. Alikuwa anapenda kutumia mtandao wa kijamii wa facebook, Baada ya hapo hajaonekana tena. Tumekuja kushtukia tarehe 25 ya mwezi wa nne baada ya kutoonekana chuo. Taarifa kituo cha polisi zilifika.
- Lilenga Isaya Lilenga - Alitekwa 11th May 2024 maeneo ya Kibirizi-Kigoma na watu wanaodaiwa ni polisi kisha kutokomea naye kusikojulikana. Mpaka sasa hajapatikana.
- Daniel Elias Sayi - Alichukuliwa na watu wasiojulikana kutoka nyumbani kwake tarehe 13 May 2024. Waliondoka naye kwa gari na hadi sasa hajaonekana wala kupatikana katika vituo vya polisi.
- Kombo Mbwana Twaha- Alitekwa nyumbani kwake Handeni Tanga na watu waliojitambulisha ni askari polisi 15th June 2024. Baada ya kupotea kwa siku 29, jeshi la polisi mkoani Tanga limekiri kumshikilia, kwa tuhuma za makosa ya kimtandao.
- Edgar Mwakalebela (alias Sativa )- Alitekwa 23 june 2024 Ubungo Dar es Salaam. Alipatikana 27 june 2024 huko Katavi porini akiwa ametapakaa majeraha.
- Mjukuu wa Mustafa Songambele - Mfanyabiashara wa Kariakoo alitoweka baada ya kufunga duka lake jioni na hadi leo hajapatikana wala hakuna taarifa zake
JESHI LA POLISI LINASEMAJE KUHUSU MATUKIO HAYO YA UPOTEVU WA RAIA?
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camilius Wambura amesema Jeshi la Polisi Nchini halihusiki na vitendo vya utekaji huku akisema ni kweli matukio ya utekaji na Watu kujiteka yapo lakini Polisi wanapambana kuwakamata Wahalifu na kuwaokoa wanaotekwa.
Akiongea Mkoani Simiyu jana, Julai 15, 2024, IGP Wambura amesema “Hatuhusiki na utekaji Watu, sisi ni Jeshi ambalo linalinda usalama wa Watu na mali zao, wanaoleta tuhuma za namna hiyo ni vitendo vya kutuvunjia adabu, matukio ya utekaji yaliyofanyika Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa na kuwakamata Wahalifu na kuwaokoa wale waliotekwa”
“Kwa mfano alitekwa Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi na kuuawa wale ni Jeshi la Polisi?, Jeshi la Polisi limewakamata wale, kuna Mtoto mwingine ametekwa Geita na Watekaji wakadai milioni 5 kwa Wazazi wake, Jeshi la Polisi limewakamata na kuokoa Mtoto, wale Watekaji ni Jeshi la Polisi?”
“Kuna Mtoto ametekwa Mbeya na Wazazi kudaiwa watoe milioni 20 lakini Mtoto huyo aliuzwa na Mama yake kwa huyo aliyejifanya Mtekaji ili wapate pesa kwa Baba wa Mtoto, hao ni Jeshi la Polisi?, kuna Watu wanajipoteza na kudai wametekwa, tumeshuhudia juzi Mwanza Mtoto wa miaka 12 amejiteka na Mdogo wake na kudai pesa kutoka kwa Mzazi wake”
“Cha msingi Jamii yetu ibadilike, Jamii yetu iache taarifa za uongo tuzingatie maadili, kuteka Watu, kujiteka na kutoa taarifa za uongo, nyie Waandishi mnapopewa taarifa hizi muwe mnacheki na Vyombo vyenye Mamlaka ya kuchunguza, tusichukue tu maneno ya Mtu mmoja anasema nimetekwa, ametekwa, amepotea, tayari mnakwenda kutoa taaarifa”
#MillardAyoUPDATES
PIA SOMA
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana