Vyuo Vikuu visivyo na sifa kufutwa!

Vyuo Vikuu visivyo na sifa kufutwa!

Hiyo ni SAUT, kimeshusha sana hadhi ya vyuo vikuu. Kimefungua matawi kila mkoa na kinataka kuweka kila wilaya. Hii ni hatari sana.
Sidhani kama uko sahihi!, UDSM nacho kinamatawi, kimetoa product yake kwa nchi wamebaki kukimbilia siasa na kuwa na mafisadi serikalini, tatizo hapa sio SAUT kufungua matawi mengi mikoani, Tatizo ni serikali zetu kushindwa kuweka mifumo bora ya kutoa elimu bora.
 
Hata chama kisipoingilia kati, yeye mwenyewe hawezi kuwa na huo ubavu wa kufuta vyuo vyote! Manake sidhani kama kuna chuo chenye at least 50% PhD Lecturers ukiondoa UDSM na SUA...

Hata Muhimbili university hawajafikisha 50%?
 
vifutwe tu, mtu anasoma form six CBG alafu chuo kikuu anasoma Engineering umeona wapi hiyo.
 
Mbaya zaidi hivyo vyuo visivyo na sifa vimeangalia udhaifu wa Bodi ya mikopo na kuamua ku capitalise on it.

Mfano kutoa kozi ambazo zina udhamini wa mikopo ili kujihakikishia kupata wanafunzi kwa asilimia 100.

Pili kuna tuhuma za rushwa kwenye kuchagua wanafunzi. Kuna hicho Chuo kisicho na sifa kina wanafunzi wa kutosha kwa mwaka 2015/2016 wakati vyuo vingine hasa vya Serikali vimekosa wanafunzi.

Wanafunzi wengi wanalalamika kozi walizochagua namba 1 na 2 hawakupelekwa na wamepelekwa kozi tofauti ili ku fit kwenye hivyo vyuo visivyo na sifa.

Mbaya zaidi watoto wanaomaliza huko ni majanga, hawaajiriki kutokana na upeo mdogo mno. Prof Ndalichako rudisha heshima ya vyuo vikuu pia.

Queen Esther

Kuna chuo kimoja cha prvt, kina matawi mikoa mingi, walimu wake nao ni tatizo,
 
Prof. Ndalichako naomba atazame pia kwenye suala kudahili yaani unakuta mtu kapata E E S alafu yupo chuo kikuu anachukua Education na anapata mkopo kama kawaida. Kiukweli hivi vyuo vikuu uchwara vimekuwa kimbilio la watu wenye ufahulu hafifu na kibaya zaidi wanakimbilia kwenye kozi za education ili wapate mikopo.

Enzi za miaka ya nyuma wakati vyuo vikuu ni UDSM na Sokoine tu, hiyo EES hata diploma ya ualimu tu katika vyuo vya ualimu hupati nafasi. Kwa hali ilivyo sasa sioni kwa nini tunamtafuta mchawi wa kuporomoka kwa elimu yetu. Vyuo vikuu vingine viko kwenye magodown ya bia (beer), hii nchi inakokwenda hakuna anayejua, Prof. Ndalichako fanya kazi yako.
 
Wamechelewa sana.Tremendous damage has already been done to the human resource base of our country.Hata hivyo hongera mama Ndalichako.Siku zote huwa najiuliza swali ambalo halipati majibu.Je,waliotufikisha hapa watafanywa nini?
Serikali ina mpango wa kukagua vyuo vikuu vyote nchini na vile ambavyo vitakuwa havina sifa itavifunga bila kusita kwani haitaki watanzania wafanyiwe majaribio katika elimu.

Taarifa hiyo imetolewa na waziri wa Elimu,Prof. Ndalichako ambaye amesema vyuo vingi havina sifa licha ya vyuo hivyo kupewa ithibati.

Prof. Ndalichako amesema inatakiwa angalau asilimia 50 ya walimu katika kila chuko kikuu kimoja wawe na shahada ya uzamivu(Ph.D) na kwamba haitakiwi mwalimu mwenye shahada ya kwanza kufundisha wanafunzi wa shahada ya kwanza.

Prof. ameongeza kuwa uwepo wa vyuo vingi visivyo na sifa kunapelekea uwepo wa vijana wengi wasio na ajira mitaani na hivyo kuongeza hasira.

Chanzo: Nipashe

Prof. Kaeleza mengi ambayo ninahakika yakifanyiwa kazi,vyuo vingi vitafungwa na itakuwa majanga makubwa.

Waaanze na MZUMBE university hasa matawi ya MWANZA na Tanga, ni wizi unafanyika na pia ada zao haziendani na Content wanayotoa yaaani 6,380,0000 huku mwalimu anaingia darasan siku 5 hadi 7 course kwisha
 
Serikali ina mpango wa kukagua vyuo vikuu vyote nchini na vile ambavyo vitakuwa havina sifa itavifunga bila kusita kwani haitaki watanzania wafanyiwe majaribio katika elimu.

Taarifa hiyo imetolewa na waziri wa Elimu,Prof. Ndalichako ambaye amesema vyuo vingi havina sifa licha ya vyuo hivyo kupewa ithibati.

Prof. Ndalichako amesema inatakiwa angalau asilimia 50 ya walimu katika kila chuko kikuu kimoja wawe na shahada ya uzamivu(Ph.D) na kwamba haitakiwi mwalimu mwenye shahada ya kwanza kufundisha wanafunzi wa shahada ya kwanza.

Prof. ameongeza kuwa uwepo wa vyuo vingi visivyo na sifa kunapelekea uwepo wa vijana wengi wasio na ajira mitaani na hivyo kuongeza hasira.

Chanzo: Nipashe

Prof. Kaeleza mengi ambayo ninahakika yakifanyiwa kazi,vyuo vingi vitafungwa na itakuwa majanga makubwa.
Hapo kwenye red, Prof. Kabugi, kwa hiyo hivyo vyuo vikifutwa ndo vijana watapata ajira?? Hofu yake kuu ni vijana wasio na ajira wanaozalishwa na hivi vyuo au??vipi wale wasio na elimu ya chuo ila hawana ajira??
 
Hawa mawaziri wetu ni tatizo sana
Moja ya sifa tuliyo nayo sisi watanzania ni kulalamika, kulalamika na kulalamika. Sasa mawaziri tatizo lao ni nini haswa?! Watanzania tumezidi kuvunja taratibu, mtu akizingatia taratibu anaitwa mnoko na hapendwi na jamii. Tulitaka mabadiliko na mabadiliko yenyewe ndiyo haya, sasa watu wanalalamika. Serikali ya sasa na mawaziri wake hawajaleta sheria, taratibu wala kanuni mpya. wanatekeleza zilizopo na ambazo zilikuwa hazitekelezwi, sasa wengi wanaona shida... Nchi hii inahitaji dikteta kutawala na kushughulikia wote vichwa ngumu kwa kuwachalaza 'bakora' kwa maana ya kuwapa adhabu stahili.
 
Huo ni ukweli wa mambo. Umekuja kwenye sekta ya Elimu kwa wakati mwafa Professor Ndalichako. Fumua mifumo yote mibovu ukianzia na chekechea had I vyuo vikuu. Kuna university hawawezi Wahadhiri hawezi kitu lakini kwa vile ni chuo chao basi ni lazima afundishe. Shule za Magabacholi , shule za Kidini nk zina huo mfumo.
 
B
Kwa vigezo hivyo vitafungwa vyuo vingi sana. Pale MUHAS mwalimu ana master ana msupervise master student.. only in Tz
Wamalize waje kwenye vyuo vya ualimu.
Kwa mujibu wa mitaala ya vyou vya ualimu vinaonesha Mwalimu lazima awe na masters unfortunately mwl. unamkuta ana degree au diploma halafu anamfundisha diploma mwenzie sijui imekaaje hii?
Funy enough, mafunzo ya grade iiiA (Certificate ya ualimu) yamefutwa ila kuna vyuo hadi leo wanatoa kwa janja janja. Tena wanafunzi wanasoma kwa certificate a year then anaunganishwa na diploma hapo hapo kwahiyo ni 4yrs kozi kama unafanya degree ya pharmacy. Kubumba bumba kwenye elimu sijui kutaisha lini.
Wamiliki wa vyuo tafuteni watu na masters zao wafundishe na fungukeni acheni ubahili elimu ni ghali aiseh
 
shida ya viongozi wetu ni wazuri kuongelea mapungufu hususani yaliyofanywa na watangulizi wao badala ya kutafuta suluhu ya hayo mapungufu. Kwamfano prof. Ndalichako angetumia muda mwingi kutafuta majibu ya changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu kuliko kutumia muda mwingi kulaumu. Nadhani huyu waziri ni mzuri ana weledi wa kutosha ktk muktadha wa elimu, afanye kazi, arekebishe yale anayoona yeye yataongeza ubora wa elimu yetu ili kuleta maisha bora kwa watanzania. Hivi vyuo suluhu yake ni kuvielekeza namna ambayo vitaendana na mahitaji ya usajili wao kwa vile ambavyo vina mapungufu. Tuachane na dhana ya kwamba chuo kikuu ni UDSM tu, dhana hii ni potofu. Watu wote hawaezi kwenda kusoma UDSM.
 
Haya mambo ndo wanayaona leo? Serikali ya awamu ya nne ilichokuwa inajali ni kupandisha tu statistics ili ionekane imefanya mambo mengi na makubwa.

Kikwete katika hotuba zake zote alikuwa akicheza tu na statistics....kwamba sijui vyuo vikuu vimeongezeka kutoka x na sasa ni y..wahitimu wameongezeka kutoka kiasi fulani mpaka fulani...na wapuuzi wenzie humu, akina FaizaFox and the like wanakuja mbio kummwagia misifa...

Itachukua miaka mingi sana kurekebisha mikasoro kibao aliyotuachia huyu mswahili wa msoga
 
Hapo kwenye red, Prof. Kabugi, kwa hiyo hivyo vyuo vikifutwa ndo vijana watapata ajira?? Hofu yake kuu ni vijana wasio na ajira wanaozalishwa na hivi vyuo au??vipi wale wasio na elimu ya chuo ila hawana ajira??
Nadhani hoja yake hapa wanakuwa hawa-fit kwenye soko la ajira kwakuwa wanakuwa watupu vichwani.
 
kwa hiyo anataka vijana wengi warudi kijijini kulima ndiko fursa iliyobaki, mjini watabaki maprofesari tu
 
Back
Top Bottom