Vyuo Vikuu visivyo na sifa kufutwa!

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,850
Serikali ina mpango wa kukagua vyuo vikuu vyote nchini na vile ambavyo vitakuwa havina sifa itavifunga bila kusita kwani haitaki watanzania wafanyiwe majaribio katika elimu.

Taarifa hiyo imetolewa na waziri wa Elimu,Prof. Ndalichako ambaye amesema vyuo vingi havina sifa licha ya vyuo hivyo kupewa ithibati.

Prof. Ndalichako amesema inatakiwa angalau asilimia 50 ya walimu katika kila chuko kikuu kimoja wawe na shahada ya uzamivu(Ph.D) na kwamba haitakiwi mwalimu mwenye shahada ya kwanza kufundisha wanafunzi wa shahada ya kwanza.

Prof. ameongeza kuwa uwepo wa vyuo vingi visivyo na sifa kunapelekea uwepo wa vijana wengi wasio na ajira mitaani na hivyo kuongeza hasira.


Chanzo: Nipashe

Prof. Kaeleza mengi ambayo ninahakika yakifanyiwa kazi,vyuo vingi vitafungwa na itakuwa majanga makubwa.
 
Last edited by a moderator:
Serikali ina mpango wa kukagua vyuo vikuu vyote nchi na vile ambavyo vitakuwa havina sifa vitafungwa mara moja.

Taarifa hiyo imetolewa na waziri wa Elimu,Prof.Ndalichako ambae amesema vyuo vingi havina sifa licha ya vyuo hivyo kupewa ithibati.

Prof.Ndalichako amesema inatakiwa angalau asilimia 50 ya walimu wa chuko kikuu kimoja wawe na shahada ya uzamivu(Phd) na kwamba haitakiwi mwalimu mwenye shahada ya kwanza kufundisha wanafunzi wa shahada ya kwanza.

Prof.ameongeza kuwa,uwepo wa vyuo vingi visivyo na sifa kunapelekea uwepo wa vijana wengi wasio na ajira

Chanzo:Nipashe

Prof.kaeleza mengi ambayo ninahakika yakifanyiwa kazi,vyuo vingi vitafungwa na itakuwa majanga makubwa.
Yes ni kweli hili aisee
 
Mwalimu mwenye shahada ya kwanza kufundisha shahada ya kwanza...haaaa.. hii nimeipenda..
 
Kuna mwalimu wa PhD? Anakua na sifa gani? Nani anamtunuku hizo sifa?

Naunga mkono hoja ya kuhakiki viwango na ubora wa elimu na kuchukua hatua stahiki.
 
Vyuo vingi vitafungwa hasa kwa kigezo cha walimu wenye sifa maana wengi wanaofundisha vyuo vikuu wana degree moja na wenye shahada za uzamivu ambao ndio wanatakiwa wewe angalau nusu ya walimu wote katika chuo kimoja ni wa kuhesabu kwenye vyuo vingi.
hicho kigezo cha nusu ya waalimu kuwa na phd ni too high .hata hivyo vyuo huanzishwa baada ya kusajiliwa na mamlaka husika.tusifurahie kuvifunga bali kuvitaka vizingatie viwango.
 
Kutokuwepo kwa ajira kunasababishwa zaid na kutokuwepo uwekezaji wa kutosha ktk sekta zinazozalisha ajira kwa wingi mfano viwanda vya usindikaj mazao ya kilimo, samaki, na mazao ya biashara, sidhan kama inasababishwa na ukosefu wa walimu wenye sifa ktka vyuo, unless kuna study imefanyika kuprove hiyo, nakubali vyuo vimekuwa vingi na ubora wake ni wa mashaka mfano vyuo vingi sana viko kariakoo havieleweki vizur, wakati tukifuta vyuo visivyo na sifa tuangalie pia je wahitaji walikuwa na sifa za kuingilia vyuon? kama wanazo na wamekosa vyuo linaweza kuwa tatizo jingine, ambalo linatukabili saiv, kuwa na wanafunz wenye sifa za kwenda chuo, pengine wengine wanaweza kujilipia lkn kwa ile kasumba ya kubalance supply ya wanaomaliza vyuo na nafasi za kaz ikasababisha kuwa na wataalam wachache mfano kwene fan ya udaktari.
 
Prof. Ndalichako naomba atazame pia kwenye suala kudahili yaani unakuta mtu kapata E E S alafu yupo chuo kikuu anachukua Education na anapata mkopo kama kawaida. Kiukweli hivi vyuo vikuu uchwara vimekuwa kimbilio la watu wenye ufahulu hafifu na kibaya zaidi wanakimbilia kwenye kozi za education ili wapate mikopo.
 
Prof. Ndalichako naomba atazame pia kwenye suala kudahili yaani unakuta mtu kapata E E S alafu yupo chuo kikuu anachukua Education na anapata mkopo kama kawaida. Kiukweli hivi vyuo vikuu uchwara vimekuwa kimbilio la watu wenye ufahulu hafifu na kibaya zaidi wanakimbilia kwenye kozi za education ili wapate mikopo.
...hiyo issue wahusika ni TCU sio hivyo vyuo..
 
Prof. Ndalichako naomba atazame pia kwenye suala kudahili yaani unakuta mtu kapata E E S alafu yupo chuo kikuu anachukua Education na anapata mkopo kama kawaida. Kiukweli hivi vyuo vikuu uchwara vimekuwa kimbilio la watu wenye ufahulu hafifu na kibaya zaidi wanakimbilia kwenye kozi za education ili wapate mikopo.
[/QUOTE

Principal pass mbili hiyo ni sifa ya kimataifa kwa mtu kujiunga chuo kikuu ingawa concern yako ni ya msingi pia.
 
Back
Top Bottom