venine
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 1,458
- 1,571
Uamuzi wowote wa kuinusuru elimu yetu huo ni mmoja wao, waziri ajielekeze kuwekeza kwenye elimu ya ufundi.
walimu wengi pia uwezo wao ni mdogo sana kufundisha Bachelor, aachilia mbali kiwango cha elimu.
Hakuna sababu za kufunga vyuo, nadhani ni muhimu vyuo hivyo vikashushwa madaraja na kuendeleza elimu ya ufundi na utoaji wa course zenye uhitaji mkubwa kwa jamii, hasa masomo ya sayansi.
Inafika muda unajiuliza hivi inawezekanaje vyuo vyote vikawa course zao ni HR, ACCOUNTING, BA, MARKETING, PROCUREMENT, ICT, na Education....something must be wrong somewhere....
Hatujachelewa kuirudisha hii nchi in those days where a degree was a Bachelor Degree.... sio sasa.....
GO make it happen Prof.
Well said. Hili wimbi la kuongeza degree za HR, Accountancy, marketing, Ualimu wa civics na english ndio unaharibu hii nchi. Hayo maeneo siyo priority areas kwa sasa. Tunahitaji watu wa kwenda kufanya kazi na wananchi. Tunahitaji maafisa ugani wa kwenda kusidia wananchi wetu kwenye kilimo, mifugo, uvuvi and the likes.
Hao marketing managers, HRO, na wahasibu wao wakimaliza wanajibana mjini wanawaza kuajiriwa na makampuni makubwa tu. Production ya hao graduates inaongezeka kila mwaka lakini hao watu hawana msaada mkubwa kwa 80% ya watanzania waliopo vijijini zaidi ya kulalamika hakuna ajira. Mtu kasoma HR, uhasibu courses inayotolewa na kila chuo then anategemea ajira za kumwaga? U have to demonstrate kitu ambacho ni extraordinary ili uajirike kirahisi. Otherwise huyo mtu akafanye kazi kanisani au kafunge hesabu za wahindi maana na uhasibu wake hata CPA haimudu
Badala ya kujikita kwenye first degrees, serikali i-concentrate kwenye watu wa kufanya kazi na rural sector. Pia kwenye vyeti vya mafundi mchundo, uashi ili watu wajiajiri wenyewe wasije lalamika hakuna kazi za kuajiriwa. Ukiangalia, vyuo vlivyoundwa kutoa wataalamu wa aina hiyo karibu vyote vimebadilishwa ili kuanza kutoa degrees. Sababu kubwa ni serikali kushindwa kuvi-support, so the only options kwa vyuo ni ku-offer course zinazovutia wengi. Serikali ina lawama ya kubeba hapa.
Kwenye elimu kuna mambo mengi sana hayaendi sawa