Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Not really..as the saying goes you have to agree that one will disagree..so im actually praising your stance on the CCM propaganda machine...lets hope they wont let u down..coz ni watu principled kama wewe ambao mara nyingi huwa dissapointed with the results pale watu fulani watapo onyesha why they really ther..

Sijui unatumia vigezo gani kunifananisha na mwana-Nazi, hili kwangu ni tusi; lakini sitaki kuchafua mjadala kwa kulijibu.

I stand na wale wanaona kuwa na matawi ya chama chochote UK kutachangia kwa namna moja au nyingine kuharakisha maendeleo ya kisiasa Tanzani. Hapo ndipo ninaposimama mimi; ndio maana nikasema (kumjibu Ben) bila kuwa na hoja thabiti dhidi ya CCM popote pale walipo hamuwawezi na wataendelea kuwa madarakani milele labda wenyewe kwa wenyewe wagombane waamue kusambaratika (ndoto..). Pamoja na hayo, siko mwepesi kutoa kashfa kwa hawa wanamapinduzi; pengine kweli wana malengo mazuri au pengine wana ajenda zao binafsi. Siwezi kuwahukumu kwa sasa, ndio maana kwa sasa nasema Time Will Tell.

Narudia tena; mimi kwa sasa nipo upande wa hawa wanamapinduzi, I will take my time kuwahukumu.

Sasa nikuulize wewe upo upande gani...katika kuchangia kuharakisha mabadiliko ya siasa Tanzania?
 
Sasa jamani wandugu mimi hili suala siku zote huwa linanitatiza. Na naona Ulaya ndo linashamiri sasa, suala la kufungua matawi ya chama ughaibuni; Nilifikiria kama tungeweza kuelekeza nguvu zote katika kujivunia utaifa wetu,tungefika mbali zaidi kuliko haya masuala ya wewe CCM mimi CUF yule CHADEMA. Sidhani kama yatawaletea manufaa yoyote yale kwa walio nje au hata ndugu zenu mliotuacha, au kama umetumwa na chama fulani kwenda kutafuta elimu zaidi ili urudi ukiendeleze chama hapo baadae then sina la kukwambia.
Lakini ningeomba sana kwanza jivunie kuwa wewe ni mtanzania, then msaidie mwenzio. Dhambi ya ubaguzi wa itikadi za chama sidhani kama itaisha.

Mnaonaje hapo washikadau.
 
Kwa kweli mimi binafsi my political stance is as a result of CCM's doing sio upinzani wala nini labda kuwe na chama cha wazalendo kwasababu policy za cuf,nccr,tlp, chadema bado sizijui, nimekuja UK mara ya kwanza bila uoelewo wowote wa siasa za bongo (or maybe i just ignored them) lakini kadri miaka inaenda na kuona systems of accountability at work ndo taratibu najikuta nikianza uliza yatokeayo nyumbani and how they are being dealt with reaching to the conclusion kwamba mchawi ni nani kama sio serikali ongozi under CCM. Sasa nilivyoanza kuona haya matawi UK, Malaysia and India i got shocked!! Kumbe kuna wengine labda hawaoni nayoyaona mimi au wana agenda nyingine? Ukifuatilia kwa karibu kuna agenda kama wewe upo UK nadhani unajua watu wawili watatu wanadili zao na sio siri unless this statement strikes closer to home (issue of interests of the people hakuna!)

Hope that answers your question..mabadiliko ya kisiasa home through tawi la ccm london is a joke to me, mabadiliko kama diaspora tunahitaji kufanya ni ya kimawazo na kuwa wakweli na wa uwazi sio kujidumbukiza kwenye shimo la maji machafu (siasa na vyama). Nchi kama zimbabwe saizi redio wanazosikiliza ni za diaspora na wanawaambia wananchi hali halisi..sasa kama watz tupo busy kubring party politics abroad wakati washida who will be the voice of the people??Kama unataka kuwa mbunge home sio lazma uwe member kokote..rudi toa sera zako wananchi kama watakukubali utapita tuu..tusitafute njia mkato ,tumeona madhara ya EPA to buy votes..ndo hiyo system sisi tulionje tunataka ijua??

Tuwe wa wazi watz wenzangu nje na tuweke wazi why we the lucky few , who see tanzania from a different perspective tunataka kurudi kwenye uozo?
 
Sasa jamani wandugu mimi hili suala siku zote huwa linanitatiza. Na naona Ulaya ndo linashamiri sasa, suala la kufungua matawi ya chama ughaibuni; Nilifikiria kama tungeweza kuelekeza nguvu zote katika kujivunia utaifa wetu,tungefika mbali zaidi kuliko haya masuala ya wewe CCM mimi CUF yule CHADEMA. Sidhani kama yatawaletea manufaa yoyote yale kwa walio nje au hata ndugu zenu mliotuacha, au kama umetumwa na chama fulani kwenda kutafuta elimu zaidi ili urudi ukiendeleze chama hapo baadae then sina la kukwambia.
Lakini ningeomba sana kwanza jivunie kuwa wewe ni mtanzania, then msaidie mwenzio. Dhambi ya ubaguzi wa itikadi za chama sidhani kama itaisha.

Mnaonaje hapo washikadau.

Nakuunga mkono kusema tudumishe Utanzania.

Ila nashindwa kujua hofu yako inatokana na nini; Hapo Tanzania kumekuwa na Vyama vingi tangu 1992, sijapata kusikia Tanzania bara kuwa watu hawazikani au hawaowani kwa sababu zao za kisiasi. Kwa nini unahofia hilo litatokea huku kuliko endelea?
 
if youidentify yourself with the 'haves,' you loose a positive image infont of the 'have-nots'.

Hayo `'Mambalozi`' sijui ya london sijui ya wapi hayapo upande yetu. Sio kwamba hatujui hayakuwa upande wetu, lakini inapoonekana sasa yanaonyesha wazi hivi kuwa yapo chchm, tuwe macho, kama wewe ni CUF au Chadema utajakosa huduma pale hapo baadaye!

Mpaka sasa ccm ina Ana kilango na mwakwembe tu... hawa wengine mhh!
 
Ukifuatilia kwa karibu kuna agenda kama wewe upo UK nadhani unajua watu wawili watatu wanadili zao na sio siri unless this statement strikes closer to home (issue of interests of the people hakuna!)

Mkuu Kapinga

Hiyo statement iko makini, hebu naomba kwa faida ya Wana wote wa UK ambao wanajua au wana nia ya kujumuika na Tawi la CCM London, weka wazi hao viongozi ni kina nani na malengo yao hasa unayosema hayako upande wa wananchi ni yapi?

Hii bulogu, tunamkoma Nyani Giladi ndio Jadi; weka mambo wazi watu wajue. Wanasemwa wakina Lowassa, JK na Mengi humu kwenye bulogu sembuse CCM London.!!
 
Nice try Mate! Viongozi wa mashina ya CCM London, Southampton,soon Coventry, Birmingham nadhani unawajua je wamekaa ki Mwakyembe or ki-Rostam??
 
if youidentify yourself with the 'haves,' you loose a positive image infont of the 'have-nots'.

Hayo `'Mambalozi`' sijui ya london sijui ya wapi hayapo upande yetu. Sio kwamba hatujui hayakuwa upande wetu, lakini inapoonekana sasa yanaonyesha wazi hivi kuwa yapo chchm, tuwe macho, kama wewe ni CUF au Chadema utajakosa huduma pale hapo baadaye!

Mpaka sasa ccm ina Ana Kilango na Mwakwembe tu... hawa wengine mhh!

Mkuu Siao

Mimi naamini wakina Dr Mwakyembe na Mrs Anna Kilango wapo wengi tu, watanzania tunaogopa; tunakaa pembeni kulalamika na kulaumu. UK, India, USA kuna Watanzania wengi kwa nafasi yao wakiamua wanaweza kuwa viongozi wazuri, lakini wanavunjika moyo na hii vibe ya negative kutoka kwa watanzania wenzao.
 
Nice try Mate! Viongozi wa mashina ya CCM London, Southampton,soon Coventry, Birmingham nadhani unawajua je wamekaa ki Mwakyembe or ki-Rostam??

Mimi nawafahamu kwa mazuri, sina sababu ya kuwahukumu; nimekuomba unipe sababu na mimi nipime na mzani wa akili yangu umanikatalia.

Wewe waonee aibu hapa forum ambako hakuna anayekujua. Kesho wakishakuwa Wabunge na Mawaziri ndio utakuja kusema laiti kama Watanzania wangejua..!!

Sina la kuongeza mkuu, forum idumu.
 
Watanzania wa USA hawataki kabisaa mambo ya matawi ya CCM au ni nini?

Akitokea Kiongozi kada mwana CCM imara hapo USA matawi yatakuja tu, tena kila State na Tawi lake; usifanye mchezo na CCM Mwafrika wa Kike wanatujua Watanzania vizuri sana...joke.. Kwi kwi
 
The bottom line ni kwamba mnaofungua matawi ya Chama Cha Majambazi(CCM) Ughaibuni MNANUKA kama CCM yenyewe inavyonuka rushwa na ufisadi. MNABOA SANA.
 
Mkuu naona umeishiwa Hoja. Heshima mbele, pumzika tu.
 
Naomba uiweke hiyo hotuba hapa mkuu.
SIO KWA IDHINI YAKE WALA YA ALIYENITUMIA BUT TUJADILI CONTENT,HASA MAENEO NILIYO YAKOLEZA,MIMI NAAMINI WAPO WENYE NIA NJEMA KWA MAANA WANAAMINI MABADILIKO NDANI YA CCM YENYEWE,SO WANAOAMINI NJE YA HAPO NAO RUKSA...ILA TUSICHOCHEE CHUKI BALI WAJIFUNZE VIJANA KUSHINDANA KWA HOJA,SO MSINGI UWE HOJA SIO PERSONALITIES....TUJADILI...

HOTUBA YA MH. NAPE MOSES NNAUYE, MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA CCM (NEC), MJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM(T) NA KATIBU MSAIDIZI MWANDAMIZI IDARA YA MAMBO YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA CCM MAKAO MAKUU, KWA MKUTANO MKUU WA CCM TAWI LA MYSORE-BANGALORE INDIA TAR.06.04.2008.

Ndugu zangu waratibu wa mchakato wa uanzishaji wa tawi la Chama Cha Mapinduzi Mysore Ndugu Antoni Mtavangu na Mohamed Sheini, Waheshimiwa sana wanachama na wapenzi wa CCM wa hapa Mysore.

Hakika, hii ni siku ya furaha kubwa kwangu, kwa Chama chetu na kwetu Watanzania tuishio hapa India wenye mapenzi mema na CCM.

Leo tumefanikiwa kuonyesha mwanga katika kutimia kwa ndoto ya kuanzishwa kwa mashina na matawi ya Chama Cha Mapinduzi India, kutokana na ukweli kwamba India ni moja ya nchi zenye Watanzania wengi, ukilinganisha na nchi zingine Barani Asia.

Hivyo nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa kutokana na kuwa wa kwanza kuonyesha njia ambayo naamini wenzetu katika sehemu zingine za India wataifuata.

Nina hakika kwamba katika historia ya Chama chetu, Mysore itakumbukwa na mchango wenu ndani ya Chama utaenziwa daima.

Chama Cha Mapinduzi, siku zote kinajivunia ninyi kama vijana, wasomi na ambao pia mnapata uzoefu katika moja ya nchi zinazosifika kwa kuwa na uchumi unaokimbia kwa kasi kubwa. Hongereni sana na msisite kutoa uzoefu wenu kwa Chama chenu na nchi yetu.
Vijana ndio nguzo, nguvu na matumaini kwa CCM. Na kwakuwa CCM kwa Tanzania ndio Chama kinachotawala, kilichopewa dhamana ya kuongoza nchi na chenye nguvu kubwa kwa sasa, basi ni wazi kuwa vijana wake ni nguzo, nguvu na tumaini la nchi yetu pia.

Hivyo basi, kutokana na hali hiyo, tunaowajibu wa kuhakikisha sifa na dhamana kubwa tuliyonayo tunaitumia vizuri kwa faida ya chama chetu na nchi yetu.

Wajibu huu unakuwa mkubwa zaidi, hasa kwa wale tuliopata bahati ya kupata elimu, na hasa elimu hii ya juu, na kwa kweli kama ni deni kwa nchi na chama chetu, basi letu linakuwa mara dufu.Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, ...dhumuni kubwa la elimu kwa binadamu ni kumpa uwezo wa kuyajua na kuyamudu mazingira yake....hivyo chama kinawategemea ninyi kwa kutumia elimu na uzoefu wenu kuyajua na kuyamudu mazingira yake, hata ikibidi kuyabadilisha yaendane na mahitaji ya sasa.
Inawezekana tu kutimiza wajibu wetu huu kama tutaamua kwa makusudi kutafakari kwa kina tena kwa moyo wa kizalendo, tumetoka wapi, tupo wapi na twataka kwenda wapi kama chama na kama nchi.
Pamoja na mafanikio mengi tuliyoyapata kama chama, zipo changamoto nyingi kwa chama chetu leo, ambazo kama vijana wa CCM tunapaswa kuzijadili na kuzitafutia ufumbuzi na hatimaye kupendekeza kwa chama chetu hatua za kuchukua kwa lengo la kukifanya chama kiende na wakati zaidi.

Tukisaidie chama chetu kiende na mahitaji ya wakati, jamii, uchumi na mazingira ya siasa ya leo. Kwa wasomaji wa Biblia watakumbuka Mtume Paulo katika kitabu cha Matendo ya Mitume alisema.......vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataota ndoto.... maono katika tafsiri rahisi hapa ni mipango kwa ajili ya ‘future’ tunakokwenda.

Lakini pia waswahili wanasema, “Kanzu ya Ijumaa hufuliwa Alhamisi.” Hali tuliyonayo leo ni matokeo ya jumla ya mambo yote yaliyopita, lakini kama vijana tunao wajibu wa kufanya tuendako kuwe bora zaidi kwa chama chetu na nchi yetu. Tusilazimike kujenga ukuta huko mbele badala ya kuziba ufa mapema kama upo leo.
Kwakuwa karibu wote hapa ni vijana, ninyi ni wadau namba moja wa Umoja wa Vijana wa CCM. Umoja wa Vijana wa CCM unapaswa kuwa chemichemi na chanzo cha fikra mpya za kimapinduzi kwa chama chetu na nchi yetu.

Historia inaonyesha mambo mengi ya manufaa na kujivunia kwa chama chetu na nchi yetu chanzo chake ni umoja wa vijana. Ukifuatilia historia, kwa mfano ni Umoja wa Vijana wa TANU na ule wa ASP ndio walikuwa wakwanza kuunganisha kuwa kitu kimoja na baadae vyama vikaungana kuunda CCM.

Changamoto zipo nyingi, lakini hapa nitatoa mifano michache kuchokoza mawazo. Kuna changamoto kama za upanuzi wa demokrasia ndani ya chama chetu, ili tuendelee kuwa mfano wa kuigwa kwa vyama vingine nchini mwetu na kwingineko duniani.

Ni kweli tumepiga hatua kubwa ya upanuzi wa demokrasia ndani ya chama chetu, lakini je uwakilishi katika vikao vya maamuzi vina uwiano sawa hasa wa kijinsia na idadi kulinganisha na ongezeko la wanachama na makundi mbalimbali katika jamii yetu kama wasomi, vijana nakadhalika?
Je, ni lazima leo kuendelea na utaratibu wa kuwa na jina moja tu la kupigiwa kura kwa nafasi kama za Makamu Mwenyekiti CCM kwa mkutano mkuu wa CCM (T) au hata Katibu Mkuu wa chama kwa Halmashauri kuu ya CCM(T)?, badala ya kuwa na majina zaidi ya moja kwa kila nafasi ili kuwezesha wajumbe kuwa na uwanja mpana wa kuchagua.

Je uwepo wa idadi kubwa ya viongozi wengi wa kiserikali wa kuteuliwa hasa na rais ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa chama chetu katika vikao vya juu vya maamuzi vya chama kunaathiri vipi mijadala, uwazi na utendaji wa vikao hivi?

Ni kwa kiasi gani vitendo vya baadhi ya wanachama na baadhi ya viongozi wasiowaaminifu vinaharibu sifa nzuri ya chama chetu?

Tukiangalia mifano ya ufisadi, rushwa, na hata kushindwa kutekeleza majukumu tuliyowakabidhi na hatua muwafaka za kuchukuliwa inapotokea utovu wa nidhamu, kama hatua ya kukiimarisha chama na kujenga imani ya wananchi na wanachama kwa chama chao.

Je, hatua zinazochukuliwa na chama kwasasa kushughulikia maswala kama ya ufisadi, rushwa na uwajibikaji zinatosha?

Ni vema mambo haya tukayaangalia kwa kina, kwani waathirika wakubwa wa vitendo hivi viovu kama vya rushwa na ufisadi ni sisi vijana. Sisi ndiyo tunaoathirika kwa kukosa huduma leo na kesho pia. Hivyo tusimame bila woga kuwanyooshea vidole na kuwakemea mafisadi na wala rushwa, ndani na nje ya chama chetu.Bado naamini sera na mipango ya CCM kwa nchi yetu ni bora kuliko chama chochote kwa sasa. Lakini mara nyingi inaingia doa kwa watekelezaji tunaowapa dhamana, kutokuwa waaminifu na makini katika utekelezaji wao.

Hivyo basi kama vijana wa CCM, tujadili njia bora za kuimarisha ufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa sera na maamuzi mbalimbali ya chama chetu ili kuwaletea wanachi maisha bora zaidi.

Na pale inapogundulika tatizo la kiutekelezaji basi hatua zinazostahili zichukuliwe mapema ili chama na sera zake safi zisichafuliwe kwa faida ya wachache na hasara ya wengi.

Nakumbuka zamani kulikuwa na maazimio yaliyokuwa na lengo la kusukuma utekelezaji wa sera na mipango ya CCM. Kwa mfano, Azimio la Musoma, Azimio la Iringa, Azimio la Mlalo na Azimio la Arusha, ambayo kwa kweli yalileta msukumo mkubwa katika utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali, ambayo mpaka leo matunda yake yanaonekana.

Nadhani si vibaya tukitafakari uwezekano wa kurejea utaratibu huu katika mazingira ya sasa, tukawa na maazimio mengine katika kusukuma utekelezaji wa sera za msingi.

Mimi ni mmoja ya watu wanaoamini kuwa Azimio kama la Arusha ni muhimu zaidi leo kwa hatua tuliyofikia kama nchi na chama kuliko hata lilipoanzishwa, isipokuwa linaweza kuboreshwa kukidhi mazingira ya sasa.Ni dhahiri kwamba kutokana na hali inavyokwenda, tunayo changamoto kubwa kwa sasa katika siasa za nchi yetu ya kutenganisha siasa na biashara!

Pamoja na viongozi wetu kuliona hili wakiongozwa na rais Jakaya Kikwete mwenyekiti wa taifa wa CCM, bado nadhani mjadala huu tusimwachie peke yake na vikao vya juu vya chama.

Bali tutumie uzoefu tunaoupata huku, kukisaidia chama chetu katika hili ili kukiokoa chama na makucha ya wafanyabiashara wachache wasio na nia njema na chama na kwa kweli na nchi.Tutumie vikao vyetu vya chama kama wasomi kujadili changamoto mbalimbali zinazokikabili chama na nchi kwa jumla.
Tutumie pia umoja wetu wa vijana kama sehemu ya mijadala ya hoja nzito za ujenzi wa chama chetu na nchi yetu; tuutumie vizuri ujana wetu wakati tungali na nguvu tusije shituka wakati nguvu hatuna tena, ambayo ni sawa na kukumbuka shuka asubuhi.

Tusipotumia ujana wetu vizuri sasa, tutakuwa hatujakitendea chama chetu haki, chama ambacho kwa sasa ni tegemeo la Watanzania na hivyo tutakuwa hatujaitendea haki nchi yetu pia.

Sisi wanachama wa CCM tuliopo hapa, lazima tuwe mabalozi wazuri wanchi yetu na chama chetu. Mahali chama kinapofanya vyema tusisite kukipongeza, lakini pia kinapokosea tukosoane na kurekebishana kwa faida ya chama na nchi yetu bila unafiki wala woga.
Tukiweza kufanya hivyo, tutaweza kusaidia kujenga viongozi na taifa la watu ambao wako tayari kukosolewa, kukosoana na kujikosoa.

Ni lazima tufute dhana ya kwamba ukishakuwa kiongozi basi unajua yote, hapana. Tukumbuke kuwa kiongozi ni watu. Hivyo kila mwanachama namsihi aone anao wajibu wa kutimiza katika ujenzi wa chama imara, bora na madhubuti ili kiweze kuwatumikia wanachi vyema.

Chama cha siasa ni itikadi, na itikadi ni imani. Sisi vijana na hasa wasomi tuongoze kwa kuonyesha hili kwa vitendo. Vyama vinatofautishwa kwa itikadi zao, tusiwe wepesi wa kuyumbayumba, tuepuke umalaya wa kisiasa, leo CCM kesho CUF, keshokutwa CHADEMA mtondogoo CCM tena.Nadhani vitendo vya namna hii vinachangia kuviza demokrasia yetu.

Ukimuuliza mwanachama wa namna hiyo, nini kilikufanya uamini kule, na kipi kilichokufanya sasa usiamini huku, mtu anakuwa hana jibu la msingi. Si rahisi kwa mtu kuhama kutoka dini moja kwenda nyingine bila sababu ya msingi, vivyo hivyo kwa siasa.

Ukiamini ujamaa simamia na ishi kama mjamaa, sio mara leo mjamaa kesho bepari, keshokutwa aah mjamaa tena, huu ni uhuni wa kisiasa

Sipingi utaratibu wa wanachama wa chama kimoja kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine,lakini tatizo langu hapa ni uhamaji unaoangalia zaidi masilahi binafsi na uroho wa madaraka au ahadi za madaraka au hata pesa.

Ni vizuri vyama vikajikita zaidi katika kupata wanachama wapya kutoka kwa wananchi wasio na vyama hasa vijana badala ya kubaki kunyang’anyana wanachama kama vile hakuna wananchi wengine.CCM tufanye hili kwa vitendo kwa kuimarisha utaratibu wa kupata wanachama wetu toka kundi la vijana wasio na vyama.
Tunapochagua viongozi wetu leo pamoja na sifa zingine tuangalie changamoto zinazotukabili kama chama chetu. Tuchague viongozi tutakaoshirikiana nao kwa pamoja kukijenga chama na nchi yetu, kwa faida ya kizazi chetu na vizazi vijavyo.

Sisi wanachama wa CCM Mysore tuwe mfano wa kuigwa kwa tabia njema, katika masomo yetu na uhusiano wetu na wenzetu, ili wengine wavutike kukipenda na kujiunga na chama chetu.

Tukumbuke sisi ni wanachama wa chama Tawala, hivyo tuongoze kwa vitendo, uanachama wetu ubebe hadhi ya chama kinachotawala ili kuienzi dhamana ambayo chama chetu kimepewa na Watanzania.

Mwisho nawatakia uchaguzi mwema, wenye mafanikio na amani, huku tukikumbuka kujenga utamaduni kuwa wakati wa uchaguzi CCM huwa tunapangana si kushindana, kwani wote twajenga nyumba moja si vizuri kugombania fito!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Mkutano wa CCM tawi la Mysore umefunguliwa!!.
 
Mkuu naona umeishiwa Hoja. Heshima mbele, pumzika tu.
Nadhani mlioishiwa hoja ni nyinyi mnaoanzisha kila siku haya mashina ya Chama Cha MAFISADI na huku mkiongoza kwa kujipendekeza kutoa hongera kila siku kwa uongozi wa CCM. Hatujawasikia mkitoa matamko kukaripia mambo ya Kifisadi yanayofanywa na wanachama wenu katika Serikali. Mnachojua zaidi ni kuvaa yale magwanda yenu ya njano na kujipendeza kwa kina Kikwete. Hii inaonyesha dhahiri interests zenu haziko katika kutetea maslahi ya nchi na rasilimali zake bali kutetea maslahi yenu binafsi. Mnawatia aibu wasomi wengine katika diaspora.
 
Nadhani mlioishiwa hoja ni nyinyi mnaoanzisha kila siku haya mashina ya Chama Cha MAFISADI na huku mkiongoza kwa kujipendekeza kutoa hongera kila siku kwa uongozi wa CCM. Hatujawasikia mkitoa matamko kukaripia mambo ya Kifisadi yanayofanywa na wanachama wenu katika Serikali. Mnachojua zaidi ni kuvaa yale magwanda yenu ya njano ku-kiss ass kina Kikwete. Hii inaonyesha dhahiri interests zenu haziko katika kutetea maslahi ya nchi na rasilimali zake bali kutetea maslahi yenu binafsi. Mnawatia aibu wasomi wengine katika diaspora.

kufungua mashina ndio kuishiwa hoja ? hoja na mashina wapi na wapi ? kuvaa kagwanda ya njano ni kosa ? others dont kiss and tell.

je ni haki pia kusema mlioishiwa hoja ni nyie mnaofungua radio kwenye internet kila kukicha ?
Nadhani hii mentality inahitaji dawa !
 
Nadhani mlioishiwa hoja ni nyinyi mnaoanzisha kila siku haya mashina ya Chama Cha MAFISADI na huku mkiongoza kwa kujipendekeza kutoa hongera kila siku kwa uongozi wa CCM. Hatujawasikia mkitoa matamko kukaripia mambo ya Kifisadi yanayofanywa na wanachama wenu katika Serikali. Mnachojua zaidi ni kuvaa yale magwanda yenu ya njano na kujipendeza kwa kina Kikwete. Hii inaonyesha dhahiri interests zenu haziko katika kutetea maslahi ya nchi na rasilimali zake bali kutetea maslahi yenu binafsi. Mnawatia aibu wasomi wengine katika diaspora.

Thanks Mazee Geeque!

I am with you hapa! Kukaa kwao kimya wakati nchi ikiwa kwenye matatizo mazito kama haya inaonyesha jinsi walivyojaa ufisadi wa kupindukia kama CCM mama kule Tanzania na viongozi wake mafisadi
 
Akitokea Kiongozi kada mwana CCM imara hapo USA matawi yatakuja tu, tena kila State na Tawi lake; usifanye mchezo na CCM Mwafrika wa Kike wanatujua Watanzania vizuri sana...joke.. Kwi kwi

Wamejaribu sana kufungua matawi hapa wakashindwa. Trust me kuna watu kibao ninaowafahamu waliokuwa wanaccm wazuri kabla ya kuanza kusikia viongozi wa ccm kina Mkono wanavyolipwa bilioni 8 kwa ufisadi wakaishiwa nguvu.

Wameamua kuimarisha vyama vya jumuia za watanzania wote, matawi ya ccm yanakufa kimya kimya. Ufisadi umezidi ccm hadi watu wengi wanaogopa kujihusisha.

Hata hivyo sitashangaa kama wakianzisha. Unajua hata Mugabe, Kibaki, na Hitler walikuwa na wapambe wao!
 
kufungua mashina ndio kuishiwa hoja ? hoja na mashina wapi na wapi ? kuvaa kagwanda ya njano ni kosa ? others dont kiss and tell.

je ni haki pia kusema mlioishiwa hoja ni nyie mnaofungua radio kwenye internet kila kukicha ?
Nadhani hii mentality inahitaji dawa !
Kukimbilia kufungua mashina ya CCM huku mkiongoza kuwamwagia misifa viongozi wa CCM ambao kila mtu anajua ni incompetent na Corrupt ni kuishiwa hoja ambazo zingeweza kuongoza kujenga taifa letu. Hivi inaingia akilini kweli wakati huu ambao Taifa liko katika wakati mgumu kutokana na viongozi wengi waliotoka CCM ambao wanaongoza kwa ubadhirifu wa mali za umma na rasilimali za nchi, baada ya kukaripia uchafu huu unaoendelea, nyinyi mnaongoza kuwamwagia sifa hawa mafisadi. Ilitegemewa kwamba wasomi kama nyinyi ndio mngekuwa mstari wa mbele katika mapigano ya kuleta haki na kumaliza rushwa hatimaye kuingoza nchi katika kuiletea maendeleo ya kiuchumi. Lakini leo hii ndio kwanza mnajiunga na MAFISADI na kuzidi kuwafanya waone kuwa hata wasomi wanawakubali katika ujambazi wao wanaoufanya nchini mwetu. MNABOA, MNANUKA NA MNATIA AIBU.
 
SIO KWA IDHINI YAKE WALA YA ALIYENITUMIA BUT TUJADILI CONTENT,HASA MAENEO NILIYO YAKOLEZA,MIMI NAAMINI WAPO WENYE NIA NJEMA KWA MAANA WANAAMINI MABADILIKO NDANI YA CCM YENYEWE,SO WANAOAMINI NJE YA HAPO NAO RUKSA...ILA TUSICHOCHEE CHUKI BALI WAJIFUNZE VIJANA KUSHINDANA KWA HOJA,SO MSINGI UWE HOJA SIO PERSONALITIES....TUJADILI...

HOTUBA YA MH. NAPE MOSES NNAUYE, MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA CCM (NEC), MJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM(T) NA KATIBU MSAIDIZI MWANDAMIZI IDARA YA MAMBO YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA CCM MAKAO MAKUU, KWA MKUTANO MKUU WA CCM TAWI LA MYSORE-BANGALORE INDIA TAR.06.04.2008.

Ndugu zangu waratibu wa mchakato wa uanzishaji wa tawi la Chama Cha Mapinduzi Mysore Ndugu Antoni Mtavangu na Mohamed Sheini, Waheshimiwa sana wanachama na wapenzi wa CCM wa hapa Mysore.

Hakika, hii ni siku ya furaha kubwa kwangu, kwa Chama chetu na kwetu Watanzania tuishio hapa India wenye mapenzi mema na CCM.

Leo tumefanikiwa kuonyesha mwanga katika kutimia kwa ndoto ya kuanzishwa kwa mashina na matawi ya Chama Cha Mapinduzi India, kutokana na ukweli kwamba India ni moja ya nchi zenye Watanzania wengi, ukilinganisha na nchi zingine Barani Asia.

Hivyo nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa kutokana na kuwa wa kwanza kuonyesha njia ambayo naamini wenzetu katika sehemu zingine za India wataifuata.

Nina hakika kwamba katika historia ya Chama chetu, Mysore itakumbukwa na mchango wenu ndani ya Chama utaenziwa daima.

Chama Cha Mapinduzi, siku zote kinajivunia ninyi kama vijana, wasomi na ambao pia mnapata uzoefu katika moja ya nchi zinazosifika kwa kuwa na uchumi unaokimbia kwa kasi kubwa. Hongereni sana na msisite kutoa uzoefu wenu kwa Chama chenu na nchi yetu.
Vijana ndio nguzo, nguvu na matumaini kwa CCM. Na kwakuwa CCM kwa Tanzania ndio Chama kinachotawala, kilichopewa dhamana ya kuongoza nchi na chenye nguvu kubwa kwa sasa, basi ni wazi kuwa vijana wake ni nguzo, nguvu na tumaini la nchi yetu pia.

Hivyo basi, kutokana na hali hiyo, tunaowajibu wa kuhakikisha sifa na dhamana kubwa tuliyonayo tunaitumia vizuri kwa faida ya chama chetu na nchi yetu.

Wajibu huu unakuwa mkubwa zaidi, hasa kwa wale tuliopata bahati ya kupata elimu, na hasa elimu hii ya juu, na kwa kweli kama ni deni kwa nchi na chama chetu, basi letu linakuwa mara dufu.Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, ...dhumuni kubwa la elimu kwa binadamu ni kumpa uwezo wa kuyajua na kuyamudu mazingira yake....hivyo chama kinawategemea ninyi kwa kutumia elimu na uzoefu wenu kuyajua na kuyamudu mazingira yake, hata ikibidi kuyabadilisha yaendane na mahitaji ya sasa.
Inawezekana tu kutimiza wajibu wetu huu kama tutaamua kwa makusudi kutafakari kwa kina tena kwa moyo wa kizalendo, tumetoka wapi, tupo wapi na twataka kwenda wapi kama chama na kama nchi.
Pamoja na mafanikio mengi tuliyoyapata kama chama, zipo changamoto nyingi kwa chama chetu leo, ambazo kama vijana wa CCM tunapaswa kuzijadili na kuzitafutia ufumbuzi na hatimaye kupendekeza kwa chama chetu hatua za kuchukua kwa lengo la kukifanya chama kiende na wakati zaidi.

Tukisaidie chama chetu kiende na mahitaji ya wakati, jamii, uchumi na mazingira ya siasa ya leo. Kwa wasomaji wa Biblia watakumbuka Mtume Paulo katika kitabu cha Matendo ya Mitume alisema.......vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataota ndoto.... maono katika tafsiri rahisi hapa ni mipango kwa ajili ya ‘future’ tunakokwenda.

Lakini pia waswahili wanasema, “Kanzu ya Ijumaa hufuliwa Alhamisi.” Hali tuliyonayo leo ni matokeo ya jumla ya mambo yote yaliyopita, lakini kama vijana tunao wajibu wa kufanya tuendako kuwe bora zaidi kwa chama chetu na nchi yetu. Tusilazimike kujenga ukuta huko mbele badala ya kuziba ufa mapema kama upo leo.
Kwakuwa karibu wote hapa ni vijana, ninyi ni wadau namba moja wa Umoja wa Vijana wa CCM. Umoja wa Vijana wa CCM unapaswa kuwa chemichemi na chanzo cha fikra mpya za kimapinduzi kwa chama chetu na nchi yetu.

Historia inaonyesha mambo mengi ya manufaa na kujivunia kwa chama chetu na nchi yetu chanzo chake ni umoja wa vijana. Ukifuatilia historia, kwa mfano ni Umoja wa Vijana wa TANU na ule wa ASP ndio walikuwa wakwanza kuunganisha kuwa kitu kimoja na baadae vyama vikaungana kuunda CCM.

Changamoto zipo nyingi, lakini hapa nitatoa mifano michache kuchokoza mawazo. Kuna changamoto kama za upanuzi wa demokrasia ndani ya chama chetu, ili tuendelee kuwa mfano wa kuigwa kwa vyama vingine nchini mwetu na kwingineko duniani.

Ni kweli tumepiga hatua kubwa ya upanuzi wa demokrasia ndani ya chama chetu, lakini je uwakilishi katika vikao vya maamuzi vina uwiano sawa hasa wa kijinsia na idadi kulinganisha na ongezeko la wanachama na makundi mbalimbali katika jamii yetu kama wasomi, vijana nakadhalika?
Je, ni lazima leo kuendelea na utaratibu wa kuwa na jina moja tu la kupigiwa kura kwa nafasi kama za Makamu Mwenyekiti CCM kwa mkutano mkuu wa CCM (T) au hata Katibu Mkuu wa chama kwa Halmashauri kuu ya CCM(T)?, badala ya kuwa na majina zaidi ya moja kwa kila nafasi ili kuwezesha wajumbe kuwa na uwanja mpana wa kuchagua.

Je uwepo wa idadi kubwa ya viongozi wengi wa kiserikali wa kuteuliwa hasa na rais ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa chama chetu katika vikao vya juu vya maamuzi vya chama kunaathiri vipi mijadala, uwazi na utendaji wa vikao hivi?

Ni kwa kiasi gani vitendo vya baadhi ya wanachama na baadhi ya viongozi wasiowaaminifu vinaharibu sifa nzuri ya chama chetu?

Tukiangalia mifano ya ufisadi, rushwa, na hata kushindwa kutekeleza majukumu tuliyowakabidhi na hatua muwafaka za kuchukuliwa inapotokea utovu wa nidhamu, kama hatua ya kukiimarisha chama na kujenga imani ya wananchi na wanachama kwa chama chao.

Je, hatua zinazochukuliwa na chama kwasasa kushughulikia maswala kama ya ufisadi, rushwa na uwajibikaji zinatosha?

Ni vema mambo haya tukayaangalia kwa kina, kwani waathirika wakubwa wa vitendo hivi viovu kama vya rushwa na ufisadi ni sisi vijana. Sisi ndiyo tunaoathirika kwa kukosa huduma leo na kesho pia. Hivyo tusimame bila woga kuwanyooshea vidole na kuwakemea mafisadi na wala rushwa, ndani na nje ya chama chetu.Bado naamini sera na mipango ya CCM kwa nchi yetu ni bora kuliko chama chochote kwa sasa. Lakini mara nyingi inaingia doa kwa watekelezaji tunaowapa dhamana, kutokuwa waaminifu na makini katika utekelezaji wao.

Hivyo basi kama vijana wa CCM, tujadili njia bora za kuimarisha ufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa sera na maamuzi mbalimbali ya chama chetu ili kuwaletea wanachi maisha bora zaidi.

Na pale inapogundulika tatizo la kiutekelezaji basi hatua zinazostahili zichukuliwe mapema ili chama na sera zake safi zisichafuliwe kwa faida ya wachache na hasara ya wengi.

Nakumbuka zamani kulikuwa na maazimio yaliyokuwa na lengo la kusukuma utekelezaji wa sera na mipango ya CCM. Kwa mfano, Azimio la Musoma, Azimio la Iringa, Azimio la Mlalo na Azimio la Arusha, ambayo kwa kweli yalileta msukumo mkubwa katika utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali, ambayo mpaka leo matunda yake yanaonekana.

Nadhani si vibaya tukitafakari uwezekano wa kurejea utaratibu huu katika mazingira ya sasa, tukawa na maazimio mengine katika kusukuma utekelezaji wa sera za msingi.

Mimi ni mmoja ya watu wanaoamini kuwa Azimio kama la Arusha ni muhimu zaidi leo kwa hatua tuliyofikia kama nchi na chama kuliko hata lilipoanzishwa, isipokuwa linaweza kuboreshwa kukidhi mazingira ya sasa.Ni dhahiri kwamba kutokana na hali inavyokwenda, tunayo changamoto kubwa kwa sasa katika siasa za nchi yetu ya kutenganisha siasa na biashara!

Pamoja na viongozi wetu kuliona hili wakiongozwa na rais Jakaya Kikwete mwenyekiti wa taifa wa CCM, bado nadhani mjadala huu tusimwachie peke yake na vikao vya juu vya chama.

Bali tutumie uzoefu tunaoupata huku, kukisaidia chama chetu katika hili ili kukiokoa chama na makucha ya wafanyabiashara wachache wasio na nia njema na chama na kwa kweli na nchi.Tutumie vikao vyetu vya chama kama wasomi kujadili changamoto mbalimbali zinazokikabili chama na nchi kwa jumla.
Tutumie pia umoja wetu wa vijana kama sehemu ya mijadala ya hoja nzito za ujenzi wa chama chetu na nchi yetu; tuutumie vizuri ujana wetu wakati tungali na nguvu tusije shituka wakati nguvu hatuna tena, ambayo ni sawa na kukumbuka shuka asubuhi.

Tusipotumia ujana wetu vizuri sasa, tutakuwa hatujakitendea chama chetu haki, chama ambacho kwa sasa ni tegemeo la Watanzania na hivyo tutakuwa hatujaitendea haki nchi yetu pia.

Sisi wanachama wa CCM tuliopo hapa, lazima tuwe mabalozi wazuri wanchi yetu na chama chetu. Mahali chama kinapofanya vyema tusisite kukipongeza, lakini pia kinapokosea tukosoane na kurekebishana kwa faida ya chama na nchi yetu bila unafiki wala woga.
Tukiweza kufanya hivyo, tutaweza kusaidia kujenga viongozi na taifa la watu ambao wako tayari kukosolewa, kukosoana na kujikosoa.

Ni lazima tufute dhana ya kwamba ukishakuwa kiongozi basi unajua yote, hapana. Tukumbuke kuwa kiongozi ni watu. Hivyo kila mwanachama namsihi aone anao wajibu wa kutimiza katika ujenzi wa chama imara, bora na madhubuti ili kiweze kuwatumikia wanachi vyema.

Chama cha siasa ni itikadi, na itikadi ni imani. Sisi vijana na hasa wasomi tuongoze kwa kuonyesha hili kwa vitendo. Vyama vinatofautishwa kwa itikadi zao, tusiwe wepesi wa kuyumbayumba, tuepuke umalaya wa kisiasa, leo CCM kesho CUF, keshokutwa CHADEMA mtondogoo CCM tena.Nadhani vitendo vya namna hii vinachangia kuviza demokrasia yetu.

Ukimuuliza mwanachama wa namna hiyo, nini kilikufanya uamini kule, na kipi kilichokufanya sasa usiamini huku, mtu anakuwa hana jibu la msingi. Si rahisi kwa mtu kuhama kutoka dini moja kwenda nyingine bila sababu ya msingi, vivyo hivyo kwa siasa.

Ukiamini ujamaa simamia na ishi kama mjamaa, sio mara leo mjamaa kesho bepari, keshokutwa aah mjamaa tena, huu ni uhuni wa kisiasa

Sipingi utaratibu wa wanachama wa chama kimoja kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine,lakini tatizo langu hapa ni uhamaji unaoangalia zaidi masilahi binafsi na uroho wa madaraka au ahadi za madaraka au hata pesa.

Ni vizuri vyama vikajikita zaidi katika kupata wanachama wapya kutoka kwa wananchi wasio na vyama hasa vijana badala ya kubaki kunyang’anyana wanachama kama vile hakuna wananchi wengine.CCM tufanye hili kwa vitendo kwa kuimarisha utaratibu wa kupata wanachama wetu toka kundi la vijana wasio na vyama.
Tunapochagua viongozi wetu leo pamoja na sifa zingine tuangalie changamoto zinazotukabili kama chama chetu. Tuchague viongozi tutakaoshirikiana nao kwa pamoja kukijenga chama na nchi yetu, kwa faida ya kizazi chetu na vizazi vijavyo.

Sisi wanachama wa CCM Mysore tuwe mfano wa kuigwa kwa tabia njema, katika masomo yetu na uhusiano wetu na wenzetu, ili wengine wavutike kukipenda na kujiunga na chama chetu.

Tukumbuke sisi ni wanachama wa chama Tawala, hivyo tuongoze kwa vitendo, uanachama wetu ubebe hadhi ya chama kinachotawala ili kuienzi dhamana ambayo chama chetu kimepewa na Watanzania.

Mwisho nawatakia uchaguzi mwema, wenye mafanikio na amani, huku tukikumbuka kujenga utamaduni kuwa wakati wa uchaguzi CCM huwa tunapangana si kushindana, kwani wote twajenga nyumba moja si vizuri kugombania fito!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Mkutano wa CCM tawi la Mysore umefunguliwa!!.

Speech Ndefu imejaa sifa kwa CCM instead of critising, humbling down, accepting mistakes and showing us the new ways to solve these problems (realistically)..umegusia swala la ufisadi kwa mbali kama kikwete vile...umeacha tuu kusema vijana tuunde tume ya kuhakikisha huu ufisadi kama ni kweli..campaign za kukanda upinzani were for 1995, 2005..saizi kila mtu anajua CCM chafu!!Mayb u can fool those kids in India of which 80% are on govt scholarships so they knw wer their loyalites lie....uchafu wa CCM umetapakaaa..tumechoka hadithi..hata waandishi wa magazeti ya rostam are doing a better job kusaficha chama kuliko nyie vijana wasomi mnaokula hela zetu za kodi India!!

ps: shein labda atakupa u assistant wake mkafungue mabucha na masoko wote!!
 
Back
Top Bottom