Nimekuwa nikijiuliza sana je kunani kwenye Chama cha mapinduzi mpaka kuanza harakati za kufungua matawi ya chama chake nje ya nchi, ninaamini kwamba watanzania walioko nje hawajaruhusiwa kupiga kura, hivyo kama unataka kushiriki kwenye siasa ni lazima urudi tanzania wakati wa uchaguzi ndipo utaweza piga kura. Swali jingine ni kwamba gharama za uendeshaji tawi ni za juu sana nje ya nchi haswa kwenye nchi za ulaya na marekani ya kaskazini.
Je haya ni matawi ya CCM ama ni mbinu za kifisadi kuibia fedha za umma kwa mgongo wa CCM.
Kimtazomo kinachofanyika ni kukusanya watoto na jamaa za mafisadi ilikuweza kuridhishwa ufisadi. Matawi mengi yanayoazishwa yanaanzishwa na watoto wa vigogo au wa ndugu au jamaa waliopo madaraka kwa ahadi ya kutumiwa fedha kwa mgongo wa chama au kupewa tenda za serikali kwa mgongo wa mwenzetu au kupatiwa kazi.
Hii sumu inayopandikizwa ni sumu mbaya sana, ukiangalia kuanzia uingereza na marekani safu ya matawi haya ni utapeli, wizi, hujuma na uzandiki. Wanatumia fedha za serikali kufanyia mambo ya chama, wanatumia vyeo vya serikali kufanyia mambo ya chama wanatumia fedha za wananchi kulelea watoto wao na jamaa zao kwa kutumia jina la chama.
Badala ya watanzania kuungana kitaifa CCM inabomoa hilo nje ya Tanzania na kuanzisha imani za chama. Viongozi wa serikali wakitembea nchi za nje badala ya kukutana na watanzania wa kada mbalimbali eti wanakutana na viongozi wa ccm kwenye matawi ya nje kweli tutafika.
Wapo watanzania wengi nje ya tanzania wasomi, wataalamu mbalimbali, wafanyabiashara,nk lakini haya yote ndani ya serkali ya ccm hayaonekani wanaleta siasa mpaka kwenye mambo muhimu ya maendeleo ya nchi.
hawa viongozi wa matawi ya CCM wataisaidia nini nchi?
Badala ya kutengeneza network ya watu wanaohitajika kwa maendeleo ya nchi inatengenezwa network ya ufisadi.
Rejea upatikanaji wa GIRE wa Richmind.
Imefikia wakati watu hawaamini wanaweza fanya biashara, kazi, au kutumia ujuzi wao tanzania bila kuwa CCM na hii inaletwa na kasumba na vitisho vinavyoenezwa na CCM na serikali yake dhidi ya wananchi wake.Ijulikane wazi kwamba sio kila mwananchi lazima awe mwanasiasa au na chama cha siasa.
Tusipo ziba ufa tutajenga nyumba.