MpigaFilimbi
JF-Expert Member
- Apr 30, 2008
- 1,169
- 188
Sijui kama hili ni tatizo la uelewa wangu binafsi au kuna kitu kisicho cha kawaida. Nimeshuhudia katika siku za karibuni kuibuka kwa matangazo ya sherehe za sherehe za kuzaliwa CCM ktk nchi mbalimbali, hasa UK na leo tena Marekani. Si lengo langu kuwakosoa watu ambao ni wanachama wa chama chochote, lakini najiuliza ndio vipaumbele kweli vya watanzania walioko nje ya nchi? kukaa kusherehekea kuzaliwa ccm? Ni kwamba wanaipongeza na kuitakia maisha mema, kwa yote mazuri yanayofanyika au?Tena watu wanapongezana kula na kunywa bure, analipa nani gharama? anayelipa kama ni mtu binafsi ana ajenda gani? tuwe wakweli kuna matatizo ya msingi kabisa yanayowakabili watanzania, na wenzetu waliopo nje ya nchi, tulidhani wangetumia muda wao kuona namna gani ya kusaidia mawazo kuliko kupoteza muda kuanzisha matawi ya chama. Ni maoni yangu tu I stand to be corrected.
Ushahidi:
Ushahidi:
sherehe za kuzliwa CCM marekani
CHAMA CHA MAPINDUZI
TAWI LA MAREKANI
Linapenda kuwakaribisha Wanachama,
Wakereketwa na Watanzania wote popote pale mlipo
katika sherehe za kuadhimisha miaka 32ya
kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Zitakazofanyika
Houston - Texas,
siku ya Jumamosi tarehe 07 mwezi wa 02 saa Mbili kamili usiku,
katika ukumbi wa Safari.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na;
Zainab Janguo: 832 206 6277
Miraji Malewa: 832 741 4452
Michael Ndejembi. 713 384 4567.
Wote mnakaribishwa: Vinywaji, Vyakula na muziki bure!
Zainab Janguo,
Katibu Mwenezi,
CCM-Marekani.