Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Hapa watapata wanachama wengi tu.

Si unajua mitoto yote ya Mafisadi ipo hapa?

Shule haiendi kazi yao kubwa ni kuangusha Birth Day, BBQ, Ulabu na kujifanya Buzy kwenye kila Misiba hata kama aliyekufa ni rafiki wa rafiki yake kutoka Ghana au Nigeria.
 
chama cha mapinduzi tawi la marekani ambalo makao yake makuu yapo mjini houston texas kwa kushirikiana na chama cha mapinduzi shina la missouri kitafungua rasmi shina lake la kwanza nchini marekani katika jimbo la missouri hapo siku ya jumamosi ya tarehe 13/9/2008.


Wanachama wote wa chama cha mapinduzi,wakereketwa,pamoja na wanamapinduzi wote popote hapa marekani na nje ya marekani mnaalikwa rasmi katika shughuli za uzinduzi huo.


Shughuli ya uzinduzi itaongozwa na mwenyekiti wa tawi la ccm marekani ndugu michael ndejembi ambaye ataambatana na viongozi wengine wa tawi na wanachama kutoka houston texas pamoja na mwenyekiti wa shina la missouri ndugu deogratis rutabana viongozi wengine wa shina la missouri.siku ya uzinduzi:
Tarehe 13/09/2008
mahali:jimbo la missouri
ukumbi:coves club house 5417 nw.85th
mtaa:kansas city mo 64154.


Kadi za chama cha mapinduzi zitakuwepo ukumbini tafadhali wanachama mje na picha(passport size).


Kwa maswali yoyote kuhusu uzinduzi huo,tafadhali wasiliana na mwenyekiti wa ccm missouri ndugu deogratis rutabana simu 816-812-5495 au kennedy mallya simu 816-255-4944.
Kumbuka: Kiingilio kitakuwa bure na kutakuwa na vinywaji
 
chama cha mapinduzi tawi la marekani ambalo makao yake makuu yapo mjini houston texas kwa kushirikiana na chama cha mapinduzi shina la missouri kitafungua rasmi shina lake la kwanza nchini marekani katika jimbo la missouri hapo siku ya jumamosi ya tarehe 13/9/2008.


Wanachama wote wa chama cha mapinduzi,wakereketwa,pamoja na wanamapinduzi wote popote hapa marekani na nje ya marekani mnaalikwa rasmi katika shughuli za uzinduzi huo.


Shughuli ya uzinduzi itaongozwa na mwenyekiti wa tawi la ccm marekani ndugu michael ndejembi ambaye ataambatana na viongozi wengine wa tawi na wanachama kutoka houston texas pamoja na mwenyekiti wa shina la missouri ndugu deogratis rutabana viongozi wengine wa shina la missouri.siku ya uzinduzi:
Tarehe 13/09/2008
mahali:jimbo la missouri
ukumbi:coves club house 5417 nw.85th
mtaa:kansas city mo 64154.


Kadi za chama cha mapinduzi zitakuwepo ukumbini tafadhali wanachama mje na picha(passport size).


Kwa maswali yoyote kuhusu uzinduzi huo,tafadhali wasiliana na mwenyekiti wa ccm missouri ndugu deogratis rutabana simu 816-812-5495 au kennedy mallya simu 816-255-4944.
Kumbuka: Kiingilio kitakuwa bure na kutakuwa na vinywaji

FMES,

Mkuu heshima mbele,

Huoni kama CCM wanachemka hapa kidogo, kwa sababu hawajafungua hata tawi tayari wana mwenyekiti wa tawi, democrasia si lazima viongozi wachaguliwe? Hao wanaotajwa hapo kama mwenyekiti wa CCM na mwenzake ni viongozi wa chama cha watanzania wa jimbo hilo sasa kama dhamana yao ya uongozi wa watanzania wa hapo ambao walitengeneza umoja bila kujiaffiliate na chama chochote utatumika kwa ajili ya CCM then wanakuwa wamewasaliti watanzania waliowachagua.
 
Kama ccm ime declare kuwa EPA ni Halali...Then sioni shida wakiendelea kujipanga na kuzikinga!
Ujinga na uelewa mdogo wa watanzania uta wacost na inatakiwa iwe hivyo hadi waingize akili...Dawa ni moja tu.....ccm waendelee kupeta...Kwani nini...Wale ugali na mrenda hadi wachoke na ..Na wakibahatika kula samaki ndio hao tena...mbofu mbofu...Si unajuwa maji yenyewe yeshakuwa polluted kwa sana?
Wacha wapewe pilao mara moja moja kwani huwezi kumwambia mtu apiganie mabilioni wakati pilao lenyewe bongo DILI.
Mmesahahu watu wanaombea msiba ili wale?
 
Waacheni wafungue mpaka ahera ,lakini wakae wakielewa kuwa mwisho wao hauko mbali ,hivyo kufungua huko ni kwa baadhi ya wajanja waliomo humo ndani ya CCM ili kujirahisishia maisha ya baadae ,ambayo yatakuwa magumu CCM itakapopigwa na chini hapa Tanzania.
Hao wenye meza na viti walioko majuu ndio watakuwa wameshajipatia rasilimali na kutakuwa hakuna wa kuwadai.
 
Huoni kama CCM wanachemka hapa kidogo, kwa sababu hawajafungua hata tawi tayari wana mwenyekiti wa tawi, democrasia si lazima viongozi wachaguliwe? Hao wanaotajwa hapo kama mwenyekiti wa CCM na mwenzake ni viongozi wa chama cha watanzania wa jimbo hilo sasa kama dhamana yao ya uongozi wa watanzania wa hapo ambao walitengeneza umoja bila kujiaffiliate na chama chochote utatumika kwa ajili ya CCM then wanakuwa wamewasaliti watanzania waliowachagua.

Mkuu Heshima ikurudie,

1. Binafsi I am very troubled na hizi tabia, unless kama kuna somebody anaweza kunielimisha, kwamba WHY? Tawi la CCM? Kwanini sio chama cha wa-Tanzania wote tu?

- I mean tawi la wa-Tanzania wote linakuwa na nia ya kuwajumuisha wananchi wote walioko nje, katika area fulani, lakini sasa hii ya CCM tu I mean ni haki ya kila mwananchi kuamua kufanya anchokitaka, lakini wale mnaoanzisha haya matawi, please mnaweza kuwa open kwamba nia na madhumuni yenu hasa ni nini?

2. Karibu robo 55% ya maisha yangu nimeishi nje ya bongo, na nimeona mengi sana, na moja la muhimu nililojifunza lilikuwa kwamba wananchi wengi kule nje, ambao hatukuwa kule kusoma, au kupelekwa na taifa, au international communities, ukweli ni kwamba kwa standard za bongo tulikuwa ni life failures, na kule majuu ndio tumepata a second chance, au tulikuwa masikini bongo tumekwenda kubangaiza kujaribu kujichomoa kwenye umasikini, kwa lugha nyingine ni watafutaji wa maisha na uchumi, by anymeans necessary,

- Sasa hapa ni kwamba, kama hii ndio ukweli wenyewe na ni clear kuwa nikiwa majuu sijawahi kuona mbongo anafanya shughuli yoyote isiyokuwa na manufaa kwake, pleaase! now my question ni kwamba kwa kufungua hizi matawi ya CCM, ambayo wananchi wote sio members, na kwamba ubalozi chombo muhimu kwa wananchi huko ni lazima kiwe pro-CCM, sasa hawa waanzishaji wanatafuta manufaa gani hasa? Halafu wanafikiri vipi kuhusu wananchi wasiokuwa wanachama?

- Rais au kiongozi yoyote wa taifa anapokwenda huko majuu ni vyema akakutana na wananchi wote bila ya kubagua, lakini kwa mwendo huu sasa hivi tutakuwa na matabaka huko nje, ambayo pia yapo nyumbani katika hizi party lines, sasa wananchi wanyonge huko nje ambao ni wengi itakuwaje kuhusu their fate na serikali yao, ambayo sio siri with tawi la CCM in hand, wataamini kuwa only through taiw hilo ndio wanaweza kuwa-reach out wananchi wote? wakati realistically ni false idea?

- Hivi mji kama Missouri utakuwa na wabongo wangapi? Labda roughly kama 500, sasa 200 wakifungua tawi la CCM, wengine 300 wanafanya nini iwapo sio wanachama wa tawi hilo hasa wanapopatwa na matatizo? Hivi kweli hapo hakuna group pressure ya kuwalazimisha kujiunga na tawi bila their will? Kwa sababu Rais akija huko na ana muda mfupi hawezi kuwaona wananchi wote hao 500, guess what? According to my experience wataitwa wachache tu yaani members wa tawi la hapo mahali CCM, that is wrong!

Ninaomba kuona ni ana madhumuni ya kuanzishwa kwa haya matawi, kwa sababu yananitia wasi wasi sana kuwa kuna watu achache wanaotaka kujiweka sawa na CV zao kwa ajili ya mbele ya safari, infact hivi ndyvyo mbunge Nyami, alivyofanikiwa kuwa mbunge akitokea Minnesota ambako alijihusisha sana na serikali na NGO ya mama mkapa na kujipatia kijiko,

Kwa hiyo mkuu Mag kwa kweli ni vyema tukachambua vizuri kuhusu hasa nini nia za vinara wa haya matawi, ambayo emngi yao ayanishia kuongozwa na watoto wa viongozi wetu wa CCM bongo, sasa maaana yake hasa ni nini? Maana nina wasi wasi kuwa wengi wetu tunajaribu kutafuta a second chance ya kujaribu maisha bongo kwa migongo ya wachache wenzetu, and that is wrong!
 
Mzee FMES umeongea pointi tupu tunahitaji wanachama wengi wa CCM kama wewe sio wale vichwa pumba wanaotaka kutuletea huu ujinga.
 
Hawa si wale watoto wa mafisadi Balaahili type nk. kwani si unajua wao husoma majuu tu na ni kati ya watu ambao husema Tanzania hakuna shida ni kama peponi ila watanzania ni wavivu na wajinga. Ukiuliza wazazi wake wanalima heka ngapi utasikia no my father is a politician. Sasa akiulizwa je siasa Tanzania ni business mbona kila mwanasiasa mtoto wake yuko hapa Marekani au nje ya nchi kusoma. Wanapatwa na kigugumizi. Zaidi wakiulizwa je wazazi wenu wametoa wapi pesa ya kwenda kuwasomesha nyinyi. wanadai salary na miradi. Je kwa nini Tanzania ni masikini na baba zenu wanafedha wasiwasaidie watoto wa kitanzania ambao hawana fedha wasome? Hapo ni pabaya zaidi. Mimi nasema siku yaja na haiko mbali upepo wa maamuzi utabadilika kabisa hapa Tanzania na tutaishi kama mwalimu alivyo-anticipate. Tuelimike kwanza tujue vyetu na nani anakula vyetu tumfanye hamna. Au mnasemaje wanaJF

I beg to differ with you,Sir.Kwa kuangalia experience ya hapa UK ambapo mfumuko wa matawi ya CCM unashindana na huko TZ,wengi wa wanaopiga debe kuhusu matawi ni wababaishaji flani ambao wanategemea kujikomba kwao kwa Chama Cha Mafisadi kutawapatia fursa za ulaji huko mbeleni.Watoto wengi wa mafisadi huku nje wako too busy "kula vipande vya keki ya taifa walivyomegewa na wazazi wao mafisadi" to care about ufunguzi wa matawi ya CCM.By the way,hata huko nyumbani,mafisadi wako busy sana na dili zao za kijambazi kuliko ustawi wa chama chao cha kifisadi.Wanaohangaika kupongeza hotuba za kipuuzi au kugawa kadi ni walalahoi wa chini ambao ndotoni mwao wanaota siku moja kuwa mafisadi wakubwa kama EL,RA,etc.(However,this MIGHT in a long run,and assuming A NUMBER OF FACTORS remain constant,lead to the downfall of CCM)

In a bigger picture,hili ni tatizo linalolikabili taifa letu kwa ujumla.Let's be honest,kuna idadi kubwa tu ya Watanzania ambao wangependelea zaidi kufikia mafanikio kwa njia ya mkato (eg kujiweka karibu na mafisadi kwa mategemeo kuwa na wao watapata good time) kuliko kujibidiisha kwa njia halali kufikia mafaniko hayo.Hapa siwalaumu watu wenye mentality ya aina hiyo hata kama haiko sahihi.Huu ni uzao wa jamii inayoona kila siku kuwa in Bongo hard work never pays.

CCM imetengeneza a vicious circle of ufisadi ambapo mafisadi wachache wanaonekana kuishi maisha yasiyoelezeka huku wakiwaminya walalahoi lukuki,ambao kila jitihada wanayofanya kuwadhibiti mafisadi inaishia kwa mafisadi hao kuneemeka zaidi,and as a result (believe me or not) baadhi ya walalahoi hao wanamaizi kuwa if you cant fight them,join them,wanapatwa na mentality ya ufisadi,na pindi mwanya ukijitokeza (kama huo wa ufunguzi wa matawi) wanachangamkia tenda.

Tuna safari ndefu sana ya kufikia ukombozi wa kweli dhidi ya mafisadi.

I am open to criticism.
 
Ikiwa CCM imeshakufa kule Pemba na kifo kimeanza kuhamia Unguja na pia upande wa bara sehemu nyingi kimeshakufa ,usitegemee kama huko majuu watapata uhai labda watumie zile mashine za hospitali.

Jambo moja ambalo limenigonga ndani ya akili ni kuwa huenda kasi hii ni ya kujitayarishia mbinu za wizi wa kura ,aidha katika makamilisho huenda ikatangazwa kuwa WaTz walioko Inchi za nje wataweza kupiga kura , CCM watakuwa tayari wameshajiweka au kwa kiswahili cha leo wameshajipanga ,hivyo ushindi mkubwa utatokea nchi za nje na si ndani ya Nchi. Usishangae ukasikia kura za nje ni milioni kumi ambazo zimeichagua CCM na laki tatu zimegawika kwa upinzani.
 
Mzee FMES umeongea pointi tupu tunahitaji wanachama wengi wa CCM kama wewe sio wale vichwa pumba wanaotaka kutuletea huu ujinga.

Mkuu Geeque,

Kwa kweli I am very troubled na this thing kwa sababu, wabongo nje wanatoa wapi muda wa kujitolea bure kwenye matawi haya ya CCM?

I mean, baaada ya kuishi sana huko the West, tumejifunza simple explanation za how binadamu functions well economically, moja wapo ni kwamba binadamu ni selfish by nature na ni mpaka akiachiwa ku-develop his/her selfishness mpaka mwisho ndio anakuwa at least satisfied na hata kuweza kuwa productive kwa taifa au wenziwe, na in this case wenziwe itakuwa familia yake au ndugu zake, sasa huyu binadamu aliyekimbia maisha mabovu nyumbani Tanzania, ambayo yamesababishwa na ile ile CCM, leo anakuwaje kinyonga na kukikumbatia chama kile cha CCM ambacho ni chanzo cha misery yake mpaka kufikia kwenda huko nje mpaka kufikia kukiaznishia tawi huko ughaibuni?,

Ambako ukweli ni kwamba anaishi maisha madogo sana na ananyanyaswa kila siku iendayo kwa Mungu na wenyeji, kama amesoma basi wamepa kazi ambayo hawamlipi kama mwenyeji kwa kisomo kama chake na kazi ile ile, akihitaji masilahi fulani toka serikali anaulizwa maswali kama mwizi, sawa lakini still kwa bado analipwa mshahara wa kumuwezesha kuishi maisha bora kuliko aliyokuwa nayo bongo,

Sasa ungetegemea huyu binadamu angelala macho kuwasidia ndugu zake waliobaki nyumbani na yeye mwenyewe, na labda ungetemea ajiunge an Golf Clubs za huko aliko, Sports Clubs, huko kuna clubs za kuendesha magari, kuna makanisa, kuna Charities, ambazo huyu mwananchi mbongo angejiunga nazo angeweza kuliasaidia sana kwanza familia yake, taifa na wananchi wengine kwa ujumla kwa kutumia nafasi hiyo ku-communicate who he is, matatizo yake na jinsi alivyokuwa kwa matatizo, matatizo aliyoyaacha nyumbani, watu wa huko majuu huwa wana utu na uwzo wa kuangalia beyond ma-box yao, na hivyo kuweza kumsaidia kama ni kompyuta za shule kijijini kwake, kama ni mipira na jezi kwa kijiji chake, na the rest of the story,

Lakini eti sasa huyu binadamu atatumia akiba ya kipato chake kwa ajili ya tawi la CCM tu kule ughaibuni? It does not make a sense at all, kuna wanaotaka kuwafanya wengine monkeys hapa, naomba mtu mmoja afanye mahesabu na utafiti wa haraka haraka, wenyeviti na viongozi wengi wa hizi matawi watakuwepo huko majuu kwa muda gani? I bet you wengi wao wako karibuni kurudi nyumbani, sio rahisi kuwakuta wale waliolowea wanajihusisha na hizi matawi meaning kwamba kuna mchezo wa kujiweka sawa na nyumbani hapa na sio anything else!

Jamani wabongo huko majuu jifunzeni kujichanganya na wenyeji wenye nchi mliko, haya matawi ya CCM ni kujitenga tu hamna lolote, unajua hapa nina picha ya Rais akiwa majuu, nchi moja ambako alishindwa kukutana na wabongo wote, kwa hiyo ni viongozi tu wa tawi ndio waliotakiwa kwenda hotelini kwake, that is wrong, ninasema kuwa it is wrong na kwakweli ninakusudia kulifikisha hili kwa viongozi wengi wakuu na hasa Muungwana mwenyewe, ninasema kuwa wananchi wasibaguliwe huko nje, wote ni sawa tu! Na si kweli kuwa CCM taifa nyumbani ndio wanahusika huu unzsihaji matawi huko nje!

Sasa ni kitu gani hasa hawa wananchi wenzetu wanakiona huko nje ambacho sisi hautukukiona mpaka kufikiria kuanzisha matawi ya CCM?

Ahsante Wakuu!
 
Kama wabongo bado wanaichaguwa ccm unategemea hao walioko hapa wafanyaje?
Yani EPA wale ccm wa bongo tu?
Ama si ubaguzi huo?
Mabadiliko kama hawatayafanya watanzania...Basi waanzishe matawi tu...Hamna shida wala nini....Mbona yakianzishwa huko Uru Mawela ama pale kwa Rafaeli hamlalamiki?
 
Wale wenye maslahi ya kisiasa bongo wanataka EPA peke yao...Sasa nadhani THE "NAPE EFFECT" IMEWAKUNA....Huyo ametoka hapo India...Sasa unadhani wanataka kichaa mwingine wa USA?
Wacha wale kwa nafasi zao.
 
Easy.
Kuna baadhi ya Watanzania wakiahidiwa Pizza na Soseji za kuchoma na ulabu wa kuchombeza,wako tayari kujitolea kufanya ujinga wowote hata kama kwa kujitolea kwao itabidi walale masaa 3 katika masaa 24.
 
Tuache Politics serikali ingefungua chama cha umoja wa Watanzania USA ingesaidia zaidi na ingesaidia nchi badala ya nyama vya siasa.
 
Hongera Wana-CCM wa Missouri chama ni chenu mna kila haki ya kukijenga mnavyojua.
 
Wale wenye maslahi ya kisiasa bongo wanataka EPA peke yao...Sasa nadhani THE "NAPE EFFECT" IMEWAKUNA....Huyo ametoka hapo India...Sasa unadhani wanataka kichaa mwingine wa USA?
Wacha wale kwa nafasi zao.


Nape ni Diaspora wa India...you wait watakapokuja Diaspora wa USA...wakina Nchimbi na PhD zao feki wakae tayari.
 
Back
Top Bottom