Mtanzania
Sio kama nakutusi kwa hayo maneno niliweka ili nieleweke vizuri sasa wewe unamoja na unalalamika, ijapokuwa umekubali sasa more deposit unayoweka low monthly repayment itakavyokuwa sasa wewe hutaki kweli kuwa na hiyo investment property na kuepuka na hayo mabox
Si unajua mabox yanaababisha mtindio wa ubongo
wewe hiyo moja tuu unalalamika sasa mwenzio analipa tatu au zaidi na bado anaisaidia CCM na mwaka jana alidhamini Umoja Cup na timu ya mpira ya Reading walishinda hilo kombe
....watu wanatafuta dataz zaidi au ndio wamekubali yaaishe?? kilikuwa kiburudisho tosha!! GT, weka picha zaidi....
Sasa huko nyuma ilivyokuwa rahisi wewe unazo ngapi ?
unakubali mwenzio ana investment wewe una nini au kujua kwingi
Risk ipo ni popote hata ndoa tuu wakati mwingine inajamba sembuse nyumba
Kama huna pesa Sasa hiyo Mortgage deposit utaweka na nini mavuzi au mdomo unaounuka
Myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
Jamani tusidanganyane hapa. Tumeona ya RA na JK na pesa chafu za kampeni. Hivi huyu mwenye CAFE ni tajiri sana kuweza kulipia jengo la ofisi ya CCM UK? Je, analipa kodi yake bila ubadhirifu? Maana hapa tunayo SOCA kama haya mambo ni kweli itabidi tuwaeleze wenyewe wayachunguze isije ikawa pesa ya walipa kodi wa UK ndio inafadhili UFISADI wa CCM kwa kutumia mgongo wa WTZ au vice versa.
Mkuu huoni kama unamhukumu bila hatia ni nani anayekudanganya ? vile vile ukumbuke kutoa ni moyo usambe si utajiri
Kwa maisha ya UK na wengi wa WTZ ambao ni wanafunzi au wabeba mabox watakuwa very lucky kupata £20 kwa saa, Je kama wanapata chini ya hapo hiyo pesa nyingine inatoka wapi? Je, hii sio pesa ya walipa kodi wa Tanzania ambayo inachezewa?
Yebo2 hebu tupe ufafanuzi mkuu.
.......Mods.....please, huyu mtu anapaswa kuelezwa kuwa asome sheria zetu kuhusu matumizi ya lugha hapa JF.......
Mods na Mkulu Invisible,
Heshima mbele wakuu, unajua kuna tunao lala macho kuweka credibility na heshima ya hii JF mbele, sasa mnaporuhusu lugha za chooni kama hizi za huyu Mkora, mnatuambia nini?
Kwanza asimamishwe na maneno haya yafutwe, halafu I have a feeling huyu mtu alishwahi tena kutumia maneno kama haya akitumia jina lingine,
I mean haiwezi ku-get lower than this!
Mods na Mkulu Invisible,
Heshima mbele wakuu, unajua kuna tunao lala macho kuweka credibility na heshima ya hii JF mbele, sasa mnaporuhusu lugha za chooni kama hizi za huyu Mkora, mnatuambia nini?
Kwanza asimamishwe na maneno haya yafutwe, halafu I have a feeling huyu mtu alishwahi tena kutumia maneno kama haya akitumia jina lingine,
I mean haiwezi ku-get lower than this!
Sasa mbona na wewe unasema lugha ya chooni
Sijui kuwa mada hii tayari imeshawekwa hapa au la. Kama ishawekwa mnisamehe.
Napenda kuuliza kuwa, hivi maana ya kuwa na matawi ya vyama vya siasa ughaibuni ni nini? Ni harakati gani za kisiasa zinazoendelea katika nchi za watu ambazo zinahitaji kuwa na chama cha siasa humo? Wakati ule wakati nchi nyingi zilikuwa bado zinagombea uhuru, tulishuhudia kuwepo kwa vyama vya siasa nchini mwetu. Vyama hivyo vilikuwa, kwa mfano, FRELIMO, ANC, MPLA, ZANU,ZAPU, SWAPO, PAC, PLO na kadhalika. Vyama hivyo vilikuwepo Tanzania kwa sababu haikuwezekana kuwa na harakati za kisiasa nchini mwao. Walipewa kibali na serikali ya Tanzania kuwepo kwa vyama humo nchini.
Je haya matawi yanayofunguliwa ughaibuni yana malengo gani? Ni jinsi gani wanachama wake wanaweza kushiriki katika siasa nyumbani? Watanzania tuishio ughaibuni kwa kiasi kikubwa hatuwezi kushiriki katika mambo ya kisiasa yanayoendelea nyumbani, hii ni pamoja na kupiga kura. Hivyo binafsi, sioni maana ya kuwa na matawi haya. Kama kungekuwa na uwezekano wa waishio ughaibuni kupiga kura, maana ya matawi anagalau ingekuwepo.
Watanzania wengi, tukiwa nje ya mipaka yetu, kitu kinachotujumuisha wote ni Utanzania wetu. Kitendo hiki cha umoja na undugu wa Watanzania unawashangaza wengi, hasa Waafrika wa nchi zingine ambao hawana umoja kama sisi. Mara nyingi tunaulizwa, 'je yule ni ndugu yako, mlikuwa mnafahamiana zamani'? Wakijua ndio kwanza mmekutana huwa wanashangaa, na jibu wanalopata ni, 'Sisi ni Watanzania.' Hapo ndipo wakati ambapo najivunia kuwa Mtanzania.
Kwa maoni yangu naona kwamba kuanza kuwepo kwa matawi ya vyama vya kisiasa ughaibuni kutaanza kuleta mgawanyiko kwa Watanzania waishio huku. Hata siku moja sijawahi kusikia au kuona kama kuna matawi ya Republicams, Democrats, Labour, Conservatives, CDU au Forza Italia katika nchi zingine! Au huu ni mtindo mpya wa siasa za kimataifa ambao unahamishia siasa za ndani ya nchi, kwenda nchi zingine? Ikumbukwe kuwa, nauliza tu.
Ni kweli na ndio maana tunawapinga wa kina Susan..kwani hatujali kwamba wao ni wana CCM..bali wamefanya nini ili kuweza kuutokomeza ufisadi?Je nia yao ya kufungua matawi ya CCM nje ya nchi ni kwa manufaa ya wanyonge wanaokandamizwa na kuibiwa ama ni kwa ajili ya kuendeleza dhulumati hizo?Kwanini waone kuwa wakati huu wa kashfa za ufisadi ndio wakakti mzuri wa kufungua hayo matawi?Nia!...je ni nzuri kwa taifa,ama ni kuendelea kutenganisha,kutawala na kunnyoya?Elimu yao waliyoipata huko uk wataitumia kwaendeleza wananchi ama kujiendeleza wao na vyama vyao vya kisiasa na maswahiba zao?Susan uje hapa utueleze!Ama yebo yebo anaweza kukuwakilisha!Naam chuki na uhasama zitazidi. Sasa hivi Watanzania katika nchi mbali mbali huwa wanahudhuria sherehe katika balozi zetu bila matatizo. Sasa kukiwa na haya matawi ya CCM, CUF, CHADEMA n.k. basi wanaCUF na wanaCHADEMA wanaweza kabisa kuamua kukata mguu kwenda katika sherehe zozote za ubalozi na watakwenda ubalozini wakiwa na shida ambayo ni lazima waende huko ili kuitatua, vinginevyo watakata mguu. Ndiyo sera za CCM hizo siku zote huweka mbele maslahi ya chama chao badala ya nchi. Hivi umeshasikia kama Wamarekani wanaweka matawi ya Demecrats na Republicans Dar? Wakiwa Tanzania wote ni wamarekani tu bila kujali itikadi zao, sosi tunataka kuanza kubaguana hata kwenye nchi za watu! Kigumu chama cha mafisadi! kigumu!
Hii mbona haichangiwi tena?ama wachangiaji wametokea kufahamiana?Ukimya umekuwa mkuu kiasi cha kutisha!Ni kweli na ndio maana tunawapinga wa kina Susan..kwani hatujali kwamba wao ni wana CCM..bali wamefanya nini ili kuweza kuutokomeza ufisadi?Je nia yao ya kufungua matawi ya CCM nje ya nchi ni kwa manufaa ya wanyonge wanaokandamizwa na kuibiwa ama ni kwa ajili ya kuendeleza dhulumati hizo?Kwanini waone kuwa wakati huu wa kashfa za ufisadi ndio wakakti mzuri wa kufungua hayo matawi?Nia!...je ni nzuri kwa taifa,ama ni kuendelea kutenganisha,kutawala na kunnyoya?Elimu yao waliyoipata huko uk wataitumia kwaendeleza wananchi ama kujiendeleza wao na vyama vyao vya kisiasa na maswahiba zao?Susan uje hapa utueleze!Ama yebo yebo anaweza kukuwakilisha!