Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatano tarehe 11 Juni, 2014

Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatano tarehe 11 Juni, 2014

wabungenjaa

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
1,782
Reaction score
337
Wanajukwaa,

Bunge la bajeti linaendelea tena leo ambapo kinachojiri kwa asbuhi hii ni mambo makubwa mawili.

1. Maswali ya wabunge kwa serikali- tayari yanaendelea hiv sasa
2.uchaguzi
i.uchaguzi wa wajumbe watatu wa baraza la chuo kikuu huria cha Tanzania
ii.uchaguzi wa mjumbe mmoja wa tume ya utumishi ya bunge.

Nitaendelea kuwapa updates.

My take: Mahudhurio ya wabunge ni hafifu sana.viti vingi vipo wazi nadhani wale wafanyabiashara waliovamia mji wa dodoma kushawishi wabunge wasipitishe mapendekezo ya serikali kuondoa misamaha ya kodi imechangia hali hii..wabunge wanaendelea kudanganywa huko nje.
matangazo haya a bunge yanarushwa live kupitia tbc1,tbc fm na star tv.

Update.
Swali limeelekezwa wizara ya fedha ambapo mbunge mh.prudensia kikwembe. ameuliza serikali kupitia TRA na bandari imeanzisha mfumo mpya wa kutoa huduma ambao hautuhusu wakala na ofisa wa ushuru kuonana lengo likiwa ni kupunguza rushwa..
i.je ni kwa kiasi gani rushwa imepungua tangu utaratibu huu uanze?
ii.je, kumekuwa na ufanisi kiasi gani wa makusanyo ya ushuru wa forodha toka utaratibu huu uanze?
.....pia aliuliza maswali ya nyongeza...kwamba kodi zinazotolewa kutokana na ushuru wa forodha na kama hayashawishi rushwa kutokana na ulipaji wa pesa taslim dirishani....kero ya mtandao ie network wakati mteja anaenda kulipa.
naibu waziri wa fedha anajibu kwamba mamlaka imeongeza muda wa kufnya kazi hadi masaa 24 il kuongeza ufanisi na malipo yanafanyika benki hivyo hakina rushwa..kuhusu mtandao pia serikali kupitia tra imeweka mitambo na mifumo ya kisasa kuwezesha ufanyaji kázi bora wa mtandao wa Internet.
wizara ya katiba na sheria.
mh. Susan kiwanga anauliza.....wazee wa mahakama za mwaanzo hawajalipwa posho zao kwa muda mrefu sasa licha ya malipo hayo kuwa yameshaidhinishwa? Je,ni lini serikali itawalipa wazee hao haki zao?...,naibu waziri anaendelea kujibu.

swali kwa wizara ya nishati na madini...
mh ezekiel maige anaulîza, halmashauri ya wilaya ya kahama meshindwa kukûsanya ushuru wa huduma toka migodini unaofikia dola 7,406,992.7 kutokana na serikali kufunga mikataba ya uendelezaji wa migodi ya bulyanhulu na buzwagi na kuvunja sheria ya fedha za serikali za mitaa inayoruhurusu halmashauri kutoza ushuru wa huduma usiozidi asilimia 3.
i. Je,seriksli iaisaidiaje wilaya ya kahama kulipwa haki yake
ii.je, serikali itarekebisha lini kasoro hiyo kwrnye mikataba iliyovunja sheria?
ii.je, serikali itatekeleza lini ahadi ya kuleta mikataba bungeni ili wabunge waone ina maslahi kwa taifa?
..,,waziri anaendelea kujibu

update..
mh. Spika anatoa utaratibu hapa wa kuwataka wabunge wa maintain despline,waache kupita pita na kupiga kelele..ametoa mwongzo kuwa atakayeonekana anafanya fujo atatajwa jina na îkiwezekana sheria itachukua mkondo wake

update.
Kipindi cha maswali kimekwisha na sasa unafuata uchaguzi wa wajumbè kama înavyoonyesha hapo juu

Wenje ameomba mwongozo kuhusu suala la wamachinga...anasema hivi sasa kuna mabomu yanapigwa mwanza dhidi ya wamachinga, wakati serikali ilisema kuwa inasimamisha zoezi la hamisha hamisha ya wamachinga hadi utaratibu mzuri utakapowekwa....anaomba serikali isimamie kaulinzake.

uchaguzi umeanza ambapo hv sasa katibu wa bunge anasoma nafasi na wagombea....
1. Wagombea wanafasi za wajumbe wa baraza la chuo kikuu wamejitokeza watatu na nafasi zinazotakiwa ni tatu hivyo wamepita bila kupingwa....ambao ni zainabu kawawa, henry shekifu na...

Nafasi ya mjumbe wa tume ya utumisi wa bunge waliojitokeza ni murtaza mangungu na anajieleza hivi sasa...
Maswali kwake Mkosamali amemuuliza atasimamia vp maslahi na stahiki zq wabunge kama sheria inavyoelekeza.
Swali from Peter Msigwa..anauliza kuna tabia ya kuchaguliwa kisha wanaochaguliwa hawarudi kwa waliowachagua.....
mtutura anamuuliza mangungu...unaonekana ni kijana mdogo kiumri lakini ki cv uko juu...mangunguanajibu

Mgombea mwingine ni Seleman Zedi anajieleza
anaeleza kuwa wabunge wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na mishahara midogo kwa wabunge na kuchelewa kupata posho zao.
Maswali.

Halima Mdee...umeeleza kuwa utasimamia posho,mishahara na marupurupu, j
 
Baada ya spika makinda kukemea udhuluraji wa wabunge na kupiga domo kwa kuwasomea kanuni zinazowazuia wabunge kupiga kelele na kudhulura, cha kushangaza mbunge wa msalala Ezekiel maige ameendelea kukaidi na spika kufumbia macho. my take, je maige ana matatizo gani au ni baada ya kupoteza uwaziri akili yake haiko sawa tena?
 
Mbwembwe za Lugola nazipenda kweli. Hakika huyu jamaa anastahili kuwa comedian kwenye kundi la Futuhi
 
Daaah yani hapo ni maslahi tuu! Nimeona mdee kauliza swali zuri limepotezewa
 
Kesho ni siku ya bajeti....na bajeti itasomwa kuanzia saa kumi kamili jioni ambapo nchi za afrika mash zitasoma bajeti zao
 
Mh. Wenje akiwa bungeni ameuliza swali la dharura na amesema kuwa sasa hivi Mwanza hali sio shwari tena maana mabomu nayapigwa kila sehemu.Maduka jijini Mwanza yamefungwa kwa siku ya leo katika operesheni ya kuondoa machinga mtaa wa Makoroboi.

Ameomba pia serikali kuweka mipango madhubuti kwa wafanyabishara ndogo ndogo (Machinga) ili wapate sehemu ya kufanyia biashara.

Ameomba serikali kusitisha hiyo operesheni mara moja na muafaka wa swala hilo upatiwe ufumbuzi na wizara husika ya viwanda na biashara.

Mh. Lukuvi amejibu swali la dharura kwa kusema, Amesema ni kweli jambo hili limetolewa humu ndani na bado serikali inakusudia kutoa taarifa, anasema mh waziri mkuu alitoka bungeni na kwenda kuongea na wahusika na watachukua hatua kwa ishu ya Mwanza kutafta ukweli wa hali halisi na pia hawawezi kusimamisha operesheni hiyo kwa kauli wakiwa bungeni.Mhe Amekuja bungeni kupiga kura na anaendelea kushughulikia hili jambo.

attachment.php


attachment.php


attachment.php
 
Naomba msaada jamani! Kwa nini wabunge wamekubali kupiga kura za siri badala ya kura za wazi? Wana siri gani na kura za wazi ndani ya bunge maalumu la katiba! Si wao waliodai upigaji kura za siri ni unafiki!!!? Nielimisheni!
 
ccm ni wahuni sana wanapiga watu alafu waziri mkuu ananongona nongona tu bungeni watu wanaumia
 
Back
Top Bottom