Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Mkuu ni beneficiary wa makato wanayokata nini...jamaa wanakera sana juzi nimeweka pesa nijiunge ikawa inagoma huku salio linazidi kuisha taratibu mpaka ikabaki zero sasa nimehamia airtel sina wasiwasi.

Umefanya maamuz sahihi
 
Na mimi vilevile ni mhanga kwani kuna siku nilikuwa nalipia king'amuzi kwa mpesa tatizo nilikosea kwenye acaunti ya malipo, hapohapo nikawapigia customer care wakaniambia watalishughulikia ,lakini wapi nikaona kimya,sikukata tamaa nikaenda voda shop hali ikawa ni hivyo,ila kiukweli hela yangu 10,000 imeniuma sana, kwa kumbukumbu ya muamala W36UQ279 Wa tar 02/11/2013 wahusika mtakua mmenielewa
 
vodacom ni wezi sana mi nilishawafata hadi oficini kwao ubungo na kuwatishia kuwapeleka Tume ya mawasiliano. yaani wanaiba sana hela zilizo kwenye mpesa, wakikutumia hata msg ya matangazo yao ukiangalia balance kwenye mpsea utakuta wamekuchagi

Jamani, kinachoniuma zaidi, ni ule mpango wa kujiunga na vifurushi, unalipa hela, na inakatwa,wanakwambia subiri ujumbe mfupi ili uanze kutumia kifurushi chako, holaa! Hakuna sms wala nini na hela imeliwa why!????
 
Sio kwamba nwatetea vodacom ila ukisahau kuswitch off intanet connection kwenye simu yako na labda iko kwenye 3G/HSDPA pesa inalambwa haraka sana, mimi huwa nanunua bando ya cheka na kuhakikisha sina salio kabisa.
 
Sio kwamba nwatetea vodacom ila ukisahau kuswitch off intanet connection kwenye simu yako na labda iko kwenye 3G/HSDPA pesa inalambwa haraka sana, mimi huwa nanunua bando ya cheka na kuhakikisha sina salio kabisa.

Kwa nini mitandao mingine hali ni tofauti.? Waweza fafanua hili.?
 
Hatuwezi kuhahalilisha ujambazi kwa kutumia ujambazi.....kama watu walikuwa wanaiba kw akutumia PD proxy, basi wachukuliwe hatua......lakini sio kwa njia ya kulazimishana (in this case KUIBA) gharama za service ambayo mteja hatumii/bila dhamira yake

Mkuu kama unaelewa hizi gharama zinachajiwa vipi na Vodacom tusaidie tupate kuelewa.....how do these people charge your phone........huku niliko nikitaka matumizi ya internet kwenye simu yangu nanunua package ya mwezi na wala hii gharama haingiliani na pesa nitakazokuwa naweka kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mawasiliano ya simu....kwa hiyo najua kabisa how much nina-spend kwenye internet na how much kwenye mawasiliano ya simu....





...sasa kwa maelezo ya Lole Gwakisa....inaelekea yeye aliweka TShs 10K.....na baada ya muda imeisha bila ya yeye kujua imeishaje........watu wengine wanasema eti kwakuwa aliacha ON matumizi ya data!!!......kwanini hivi vitu visitenganishwe? ukiweka pesa yako kwenye simu hata iwe TShs 100K....iwe ni kwa matumizi ya mawasiliano ya simu.....na pale unapotaka kutumia internet unatuma ujumbe/code ili kununua package unayoitaka.......either kununua kupitia salio lako kwenye simu au kununua upya kabisa......

Kinachonishangaza ni kusikia huko bongo ukishaweka pesa yako kwenye simu tu.......ni lazima uhakikishe "eti data iwe OFF kwenye simu yako".....WHY?....hii ni kama kulazimisha gharama kwa mtu hata kama hatumii service yenyewe!......hence huu ni WIZI

Ogah
That's how it should have been, but contrary in this country.
 
Sio kwamba nwatetea vodacom ila ukisahau kuswitch off intanet connection kwenye simu yako na labda iko kwenye 3G/HSDPA pesa inalambwa haraka sana, mimi huwa nanunua bando ya cheka na kuhakikisha sina salio kabisa.
Huo ni UONGO unaotumika kuhalalisha WIZI.
Ili kuwa prove wrong, nimeongeza salio langu kwenye simu la thamani ya Tshs 50,000 toka juzi.Pamoja na hilo nimeweka settings za Mobile Data na 3G zote kuwa ON.

Matumizi yangu yamekuwa kawaida kabisa na mpaka asubuhi ya leo salio langu ni kubwa tu.
Hii ikiwa na maana kwamba huyo mwizi hajapata access ya " kupiga" salio hilo.

Ni uamuzi sahihi kuhama huduma hii ya VODACOM, lakini kuna watu wengi sana kana mimi ambao wana simu moja tu wayanyoitumia kwa shughuli zote za kiofisi, kibiashara na hata matumizi ya kibinafsi.

Nategemea TCRA waje na njia ambayo mteja anaweza ku-sue kimahakama na kudai fidia, akiona kuna kuna wizi wa dhahiri kama huu.
 
Bora yako uliye ibiwa salio la vocha, mimi niliibiwa laki2 mpesa, na rb nikapewa, wizi kwa njia ya mtandao! Nilihangaika mwezi mzma bila mafanikio
 
Nasikitika na kulia Voda wamekwangua bundle la internet 5GB nililo nunua Tar.27/12/2013 jana Tar.31/12/2013 bundle lote jamaa wamekwangua na matumizi yangu ni ya kawaida sana ni email na kuingia JF yaani inaniuma sana hawa Voda walicho nitenda nawapigia longo longo nyingi.
 
Gwakisa, umesahau kuwa Rostam bado ana hisa Vodacom? Hata watu kama January Makamba hawafai kusimamia sekta nyeti kama ya mawasiliano!

January na Boss wake katika wizara ya mawasiliano wanatakiwa kujiuzuru. Pesa tunazoibiwa kila siku na makampuni ya simu ni nyingi mno!
 
Gwakisa, umesahau kuwa Rostam bado ana hisa Vodacom? Hata watu kama January Makamba hawafai kusimamia sekta nyeti kama ya mawasiliano! January na Boss wake katika wizara ya mawasiliano wanatakiwa kujiuzuru. Pesa tunazoibiwa kila siku na makampuni ya simu ni nyingi mno!
Nakubaliana mkuu, malalamiko ya wizi yamekuwepo siku nyingi katika mtandao wa VODACOM ingawaje mimi nimekumbwa hivi karibuni tu.

Badala ya kuyafanyia kazi malamiko ndani ya eneo lao la kazi, January Makamba yuko busy kuusaka urais,
Waziri wake Makame Mbarawa is no better, hawajawahi kuyafanyia kazi malalamik yanayoweza kuibua wizi wa mabilioni.
 
Kuna kitu nadhani watu wengi wanaolalamika kuwa wanaibiwa mnakosea. Kama unatumia smartphone na hujajiunga na bando la internet ni lazima pesa yako itaendelea kuliwa taratibu hadi iishe. Cha msingi kama wewe hutumii inernet nenda kwenye mobile network then iweke off! Otherwise applications ambazo zinafanyakazi katika background zitamaliza pesa yote.

Ukijiunga kwenye bando ndio unaibiwa vizuri mchanaaa. Bado linaisha hakuna hata notification text. Unaanza kukatwa pesa kwa kiwango kikubwa sana
 
Vodacom ni wezi kwa kwenda mbele. Kwanini wasilete utaratibu wao wa kutoa taarifa ya jinsi ulivyotumia pesa yako kwa matumizi ya simu mara tu unapokuwa umemaliza kupiga au kutuma sms.

Hao ni wezi wa hatari. Cha msingi acha kutumia mtandao wao basi.
 
Back
Top Bottom