Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Ukifkiria kuvunja kadi uhamie mtandano mwingine una tumiwa sms pata dakika 60 kwa shilingi 200 tu kwa siku nzima. Vodacom kazi ni kwako!
 
Mimi sijawai kupata hilo tatizo in fact nawafagilia sana vodacom! nadownload mafile kibao ya maGB kupitia kifurushi chao cha unlimited......labda hujakijaribu. na speed yao ni bomba sana.
 
Mobile networks zote zinasumbua sana kwa suala la internet! Mtandao usiokuwa na matatizo ni TTCL labda sema sasa wao wana gharama sana.
 
Nashukuru Vodacom Tanzania wameona tatizo langu wameni PMniwatumie number yangu nafikiri wanashughulikia tatizo

Sasa huu ndio wizi. Ina maana gani kuhudia mteja mmoja mmoja tena aliyelalamika? Kwanini wasiwatreat wateja wao fairly tu mpaka biashara za kuPM?

Mimi nilishachukia kwenye iPad kwenye iPhone unaweka monthly bundle lakini internet sloooow na inakata mapema sana.

Ni shida sana.
 
Fikiria mtu unatuma/kutumiwa sms alafu hazifiki kwa wakati. Hivi hii tabia ya huu mtandao kujiona sana kiasi cha kudharau hata malalamiko ya wateja ina sababishwa na nini hasa?

Alafu kitu kingine nmegundua Vodacom ukiwa maeneo ya mjini hasa posta network hasa upande wa internet inasumbua sana!
Hiki kiburi chenu kiwe na mwisho!

bila kusahau kuwa wanatuibia sana salio, unanunua dk 105 za 2800 ukiwa na salio la 7200 kwa simu yako, unapiga dk 25 zinaisha zote, na ile 7200 inalambwa yote
 
Back
Top Bottom