Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nilikuwa nje sana ya Dom kuelekea singida ..... Nilipaki tu kwenye kamji hapo kuna kacenter ..... Fresh lakini ilirudi mpesa
Ulimaliza hela yote nmb kupeleka mpesa?

Pole sana. Ila Dodoma nadhani kuna hotel unaweza kulala na kulipia kwa mpesa. Pole sana mkuu.

Lakini pia unaweza kwenda kulala hotelini na pesa ukalipa asubuhi.

Kulala kwenye gari ulijitakia mwenyewe.
 
Juzi nilihamisha Tshs 1000
Toka M-Pesa kwenda Tigo ninunue vocha, hela ikapote. Tigo wakasema niulize Voda program ya Voda hairuhusu kuongea na muhudumu.

Voda hakuna na Tigo hakuna, huduma kwa wateja iko programed hakuna kuongea na muhudumu.

Naona Voda mmeridhika hamna shida na wateja, mmeweka wezi wakwapue hela zetu!!
Ahsanteni!!
 
Huduma ya M-pesa kulipia kisimbuzi cha Azam kwa nini hadi sasa hivi toka asubuhi haipatikani? Hamuoni kama mnahujumu makusudi biashara ya kisimbuzi cha Azam?

Rekebisheni hiyo haraka
 
Kwenye menyu yenu ya huduma za vifurushi ambayo ni *149*01#
Ondoeni vifurushi hivi

1.REDRXL
2.Pinduapindua
3.Kimataifa % Kuzuru
4.Tuzo
5.Muda wa maongezi(OFA)
6.Dar Ofa

Badala yake wekeni menyu hizi
1.WAJANJA NIGHT
Hii itawakuwa ni GB 1 kwa 500 kuanzia saa 6 usiku mpaka saa 12 asubuhi.
Na GB 5 kwa 1,000/kuanzia saa 6 usiku mpaka saa 12 asubuhi.


2.YA KWAKO TU
Sh 500 = Dakika 20(Voda) SMS 300 na MB 400 kwa masaa 24.
Tsh 1500 = Dakika 75(Voda) SMS 1500 na GB1.2 kwa siku 7 tu.


3.INTANETI
1.Siku
Sh 500 - MB 250
Sh 1000 - MB 500

2.Wiki =
Sh 1000 - MB 500
Sh 1500 - MB 1024(GB)
Sh 2000 - MB 1500(GB 1.5).


3.Mwezi =
Sh 5,000 - GB 5
Sh 10,000 - GB 12
Sh 20,000 - GB 25
Sh 30,000 - GB 35


4.Youtube = GB
Siku -
Sh 500 - 500 MB5
Sh 1000 - GB 1.2


Wiki -
Sh 1000- GB 1
Sh 2000 - GB 2.5

Mwezi -
Sh 3000- GB 3
sh 6000 - GB 6


4.VIFURUSHI VYA WHATSAPP
A.WHATSAPP TU
Sh 500- MB 300 kwa saa 24
Sh 1000 - GB 1.5 kwa simu 7
Sh 2000 - GB 3 kwa mwezi.

B.WHATSAPP na INSTAGRAM
sh 500 - MB 500 kwa saa 24
Sh 1500 - GB 1.6 siku 7
Sh 3000 - GB 3.2 mwezi


5.WELCOME OFFER
Mteja mpya aweke salio la 1000 apewe Dakika 60 (voda) SMS 500 na GB 1 wiki nzima.

6.YA KWAKO TU
Sh 500 - Dakika 30(Voda) SMS 500 na MB 500
Hii huduma ipatikane kwa kila mtu hata kama anaishi Chato au Msoga au Tandahimba.

Mteja akinunua kifurushi kupitia M Pesa apate punguzo la 10%

Asanteni kwa kunisikiliza.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Voda wana vifurushi vya kiboya sana na network yao iko down!! Nna voda ila situmii maana huu mtandao umeshaingiliwa na wahuni.

Unaweza kushangaa siku mke anakusikilizisha sauti ukiwa unaongea na mchepuko na unamsema kweli kweli!! Yani wamekudukua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asee ikiwa hvo watakua wametuinua sana

Sent using Jamii Forums mobile app
halafu wazingue
Screenshot_20200106-002558.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
(Hii ni kwa Wateja wa Vodacom tu)

Habarini za Wiki wakuu,

Ni hivi Juzi kati nilikua nimekaa na ndugu yangu mmoja kwenye story mbili tatu ikatokea mada ya Freemason kwamba ukituma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno Freemason text inafail kutoka yaani haitoki kabisa duh basi mimi sikuamini kirahisi tukachukua simu yake akafanya kama ananitumia kitu kikagoma sikuamini pia mimi nitomaso kiaina.

Nikachukua simu yangu nikafanya mwenyewe sasa Hola text haikutoka duh basi ikabidi ni nyooshe mikono juu kukubali tu sasa hawa jamaa wana maana gani kuzuia text zenye maneno haya?...

Kwa wateja wa mitandao Mingine sijui labda mjaribu na nyie
 
ni sawa na kumpa mbinu adui yako za kushinda vita,wacha wajifie kiburi kiliponza shingo ikaenda.

mara ya mwisho naangalia ya kwako tu katka line yangu waliniwekea mb 250 kwa buku,nikacheka sana halafu nikaitoa line kwenye simu nikaweka uvunguni.imepita miezi 2 tu,naulizia ya kwako tu nakuta wamerudisha gb 1 kwa buku,na nimegoma sasa sinunui.

ufalla una gharama zake.
 
Back
Top Bottom