Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nina swali moja kwa watu wa mtandao, naombeni tafadhali mnijibu.

Ni hivi, kwa mfano mtu ameenda kusoma nje ya nchi hasa nchi za mbali huko, wakati akiwa nchini alikua akitumia mawasiliano ya simu kwa kupitia laini zenu je anavokua nje ya nchi halafu akakaa huko zaidi ya mwaka atakapokua amerudi masomoni ile laini yake ya simu atakua bado anaendelea kuitumia au haiwezekani na kama haiwezekani je kuna taratibu za kufuata ili aendelee kuitumia ile laini yake?
Naombeni majibu ya hili swali, au kama hamna majibu nianzishe uzi wa hivi ili wanijibu wenye ujuzi wa haya mambo.
 
Vodacom bwana. Eti anatokea mtu anajitambulisha eti anatoka promosheni ya miaka 10 ya Voda. Eti wanagawa pato-bonus kwa wataeja. Naambiwa nimezawadiwa sh.laki tatu na sabini elfu (370,000/-).

Nasubiri ziingie kwenye account yangu ya simu mpaka leo sijaiona. Vodacom hapo niwape jina gani.

Kama kweli hiyo bonus ipo basi fanyeni kweli.
 
Wahusika wa Vodacom Tanzania taarifa ni kitu cha msingi sana kwa wateja wenu.. mchezo wa kubadili units za pindua pindua bila taarifa mnakosea.

Jana unit 5 ilikua sawa na dakika moja mitandao yote. Leo unit 50 ni sawa na dakika moja yaani mara kumi zaidi ya ilivyokua sikua ya jana? Shikamooni...
 
Achana nao,njoo Halotel
 
Vodacom. Kuna nini watu tunanunua umeme hamtumi TOKEN tunatuma pesa hazifiki sehemu husika. Kama kazi imewashinda semeni kuliko kuwalaza watu bila umeme na maudhi mengine kibao.
We are not happy with these shithole services
 
Mimi.nimeshulumiwa 150000 na mfanyakazi wa Vodacom Geita na hataki kunilipa pesa zangu.naombeni mawasiliano ya Vodacom.Geita nisaidiwe kupata pesa yangu.
Ishu kwenda policy na sms iyo mawasiliano haitakusaidia ndyo wenye dhamana Voda watazaidiana
 
Kitendo mlicho kifanya leo voda mmenikasirisha sana mnashindwa nini kutoa taarifa? Mnashindwa nini kupokea simu?

Mnaongea kizungu wateja wenu wote wanajua? Customer care ni ziro kama sio sufuri

Nimejiunga mara ya kwanza mtandao ukagoma hela yangu mkakata sms amkutuma

Nimebonyeza mara ingine kujiunga hela mkakata amjaleta nilichojiunga wala amjatuma sms

Nimerudi mara ya tatu mmerudia ujinga ule ule hela mmechukua huduma amjanipa wala sms amjatuma

Mnapigiwa simu ampokei baada ya lisaa hela zangu mmekata mnanitumia huduma nilio jiunga nyuma tena kwa mkupuo

Huu ni usengeeeeeeee
IMG_6630.JPG
IMG_6631.JPG
IMG_6632.JPG
 
Hivi CEO wa Vodacom Tanzania ni nani ? The perfomance of VT was very good in the past. But from the beginning of this year VT has been going down the drain.

Mumebadilisha management au munataka nini. Siku hizi hakuna gawio la huduma ya mpesa. Ukituma pesa inachukua over 48 hrs ndio ifike.

Ukiongea kwa simu ikifika katikati ya maongezi wanakata simu. Mbaya zaidi internet ni ya kuvizia. It is on and off.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Habari za Kazi.
Mi nilimiliki line ya Voda kwa miaka12, kuanzia mwaka 2006. Mwaka jana Mwezi wa 9 nilisafiri kwenda kusoma nchini China, mwaka huu mwezi wa 7 (baada ya miezi 10) nimerudi rikizo ile line imefungwa, nikaanza kuirudishia (Swap) nikaambiwa imeishauzwa kwa mtu mwingine. Na liicha ikiwa na Airtime salio lisilopungua elfu 20.

Mbaya zaidi Ndugu na jamaa zangu wanampigia huyo mwenye namba anarespond kama yeye ndio mimi na kuna wengine anajaribu kutaka kuwatapeli, kama vile kuwaomba hela. Au katika kujibu anasema ile hela hajaipata kama ana bahatisha kutaka kutapeli.

Najua katika kusajiri laini ya voda kuna detail za muhusika kwa kua katumia kitambulisho na kuna sehemu tulikua tunaandika email zetu, kabla hamjauza line ya mtu muwe mnafanya uchunguzi kama huyo mteja kweli hatoitumia tena. Na inawezekana vipi muuze laini ya mtu huku ndani ya laini kuna salio kubwa kiasi hicho? maana ndio line yangu official nimeisajilia kila sehemu kama Benki na pia nilikua napokea muda wa maongezi (Postpaid) kazini kila mwezi 50,000/= kabla sijaja China kusoma.

Kama kuna uwezekano naomba nirudishiwe line yangu. Document za kurudishia (swap) na Lost report ya police ninayo hapa.

Shukurani.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Mimi laini sikuthibitisha usijili kutokana na kupoteza vitambulisho vyangu vyote, he kuna msaada wowote naweza pata au ndio niachane nayo? maana mmenifungua huduma zote na mtandao wenu naupenda
 
Vodacom wizi wa kutuibia salio wananchi wanyonge kwa ujanja ujanja usio na maana utaisha lini?, au hadi tuwashtaki kwa Rais?.

Kila nikiweka vocha na kubakiza salio kwenye line yangu vodacom mnaiba izo pesa. Utakuta umefanikiwa kujiunga games longe afu salio linakatwa, najitoa kwenye hiyo games longe lakini wapi...hamchoki kuniibia. Zile mia tano zangu mnazoniibia kila siku, mkiiba kwa wateja wenu milioni moja inamaana kwa siku mnajiingizia shilingi milioni mia tano kiujanja ujanja na kwa mwezi ni bilioni kumi na tano.

Hizi pesa hizi sizinajenga hospitali huko vijijini?. (Huu mfano tu ila ni kweli hua naibiwa mia tano kila nikibakiza salio. Namba yangu ni 0769515507)
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom