Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Mimi mmeniudhi kitu kimoja nimepoteza laini yangu kuirudisha naambiwa namba tano nilizokuwa nazipigia Mara kwa Mara sasa Mimi nazipata wapi wakati nimepoteza simu kitambulisho ninacho lakini mmeshindwa kunirudishia nimeamua kuachana na voda kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una hoja dhaifu sana!. Kwan si kuna vifurushi visivyoisha muda?. Ni upuuzi ununue kifurushi cha 24 hours halafu utake kidumu miez 3 kwanini usinunue kisichoisha?
Namba 1 sijui huko lkn huku Mbeya mjin at least wanavutia Voda compared to others hivyo tafuta mtandao wenye uafadhar utumie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siwezi kuhangaika kujibizana nawe.unaonyesha tu jinsi uko mjinga au mlevi mlevi fulani.kweni umeona sina hiyo mitandao mingine?huu ni uzi wa halotel au tigo?pumbavu kabisa
 
Vodacom Tanzania sijui nianzie wapi kuelezea hili tatizo! Mwanzoni call quality kwa upande wa sound ilikua nzuri Sana.

Ila kwa sasa kwa kweli sio nzuri kabisaa inaumiza hadi masikio. Mmegusa nini huko kwenye mitambo yenu!? Unapiga simu inachukua dakika ku connect, au hata ku connect tu inakataa na if the call go through... It's quality is real poor you even hear ticking sounds humo humo kwa call Vitu kama "kwichi kwachu kwachu" yani ni kama vita. Mmepatwa na nini!?

Nilidhani ni simu yangu lakini sio kweli kwani nilibadili line na call quality ikawa safi kabisaa. Na sio peke yangu kwani hata wafanyakazi wenzangu wanalalamika hivihivi. Shida ni nini tena nipo Dsm inapopatikana 4g!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
(1) kwa nini mmeacha kutoa gawio la m-pesa?
(2)zaidi ya mara mbili nilijiunga kifurushi cha mb,ya kwako tu,lakini hapohapo nikaambiwa kifurushi kimeisha bila hata kukitumia,kwa nini mnakua wezi kiasi hiki!?
(3)nilikua tabora wiki iliyopita,network ikawa shida(internet),iliporudi kifurushi kikawa kimeisha muda wake,kwa nini hamrudishi mb kiungwana kama wenzenu tigo!?
Maswali ya kichochezi huwa hatujibu kwanza wewe tunamashaka na uraia wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Mtu unakuta niko na simu nzuri kabisa ya kisasa(samsung/apple n.k) na settings zangu ziko sawa kabisa lakini kumekua na tatizo la internet kiasi mpaka inatia hasira.muda unaonunua kifurushi ndo unakuta muda unanyimwa huduma nzuri,mtandao unakua chini sana na upo town wala si porini kusema kwamba labda hakuna network la hasha.

2. Wateja tunanunua kifurushi na muda unapofika ule ulionunulia kifurushi kama ni 24hrs kifurushi kinaishia hapo hata kama MB bado uko nazo,huu nauita ni wizi mkubwa.kwa nini msiache mpaka MBs ziishe ndipo mtu anunue zingine?na kwa nini msiache mtu anapoingiza muda wa maongezi iwapo kifurushi cha internet kimekwisha ukiweka vocha inaliwa ghafla eti mpaka uzime data.kwa nini msiache muda wa mtu wa maongezi uwepo hewani mpaka tu pale yeye mwenyewe atakapoaamua kununua kifurushi cha internet?kuna aina ya ujanja ujanja m'baya sana mnaufanya.

3. Ninaamini 80% ya wanatumia mtandao wa Vodacom kama isingekua huduma ya m pesa yamkini mngekimbiwa na wateja wengi sana nikiwepo na mimi.
Jaribuni kubadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ukiwa unaambiwa kifurushi ni cha masaa 24 unatakiwa ukitumie chote kiishe ndani ya masaa 24, hapo unalalamika kitu ambacho vigezo na masharti yamezingatiwa, kuna vifurushi vya wiki mwezi jaribu hivyo au vp.

Afu kuliwa vocha ni simu yako ya smatifoni, mi kila nikiweka vocha nazima kwanza data maana simu itaichukua km kifurushi na kuanza kurefresh apps online.

Nimejibu km mteja tu wa vodacom sio muhusika wa vodacom.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NaitwaNm marwa
Ilitokea bahati mbaya nkakabwa na nikaibiwa namba simu na hivyo kupkupoteza till yangu ya mpesa.

Nauliza utaratibu wa kuirenew ukoje ukizingatia kukuwa niliinunua kwa mtu tu. Viambatanisho gani natakiwa kuwa navyo ili niniweze kuo renew?
Shukrani
 
Kuna matukio kadhaa nimeyashuhudia kwa macho na masikio yangu yaliyonifanya nihitimishe kuwa Vodacom ni mtandao mbaya Tz.

-Mtu mmoja kaweka vocha, vocha ikawa invalid tukawapigia Voda, wakatujibu kuwa iliingia sokoni kwa makosa, tusubiri baada ya siku 2 tutapata vocha nyingine. Shit , vocha niisubiri siku mbili, how.

-Line ya wife ilistack na Mpesa kuna kama laki 4, akarenew line sasa kurudishiwa huduma ya mpesa masharti mengi.

-Kuna mtu jana nilimpa kiasi fulani cha fedha aniwekee kwenye Tigo Pesa, ila aweke kwake kisha aitume kwangu mimi nilikuwa nimetingwa na majukumu. Kaweka kwenye Mpesa yake ili anitumie Tigo Pesa , Pesa kwake imeshatoka kwangu haipo. Unawapigia voda wanasema mtandao unasumbua.

Are they crazy?
Eti mtandao unasumbua utaipata, why ilikubali kutoka kwenye line moja?
Je, usumbufu nioioupata mtanilipa?
Ningekuwa na mamlaka kampuni kama hizi ningezifungisha virago.
 
Mkuu ukiwa unaambiwa kifurushi ni cha masaa 24 unatakiwa ukitumie chote kiishe ndani ya masaa 24, hapo unalalamika kitu ambacho vigezo na masharti yamezingatiwa, kuna vifurushi vya wiki mwezi jaribu hivyo au vp.

Afu kuliwa vocha ni simu yako ya smatifoni, mi kila nikiweka vocha nazima kwanza data maana simu itaichukua km kifurushi na kuanza kurefresh apps online.

Nimejibu km mteja tu wa vodacom sio muhusika wa vodacom.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huelewi vyema nilichosema.kaa pembeni na ulevi wako,unatetea ujanja ujanja wa Vodacom unalipwa?kaa pembeni
 
Nina swali moja kwa watu wa mtandao, naombeni tafadhali mnijibu.

Ni hivi, kwa mfano mtu ameenda kusoma nje ya nchi hasa nchi za mbali huko, wakati akiwa nchini alikua akitumia mawasiliano ya simu kwa kupitia laini zenu je anavokua nje ya nchi halafu akakaa huko zaidi ya mwaka atakapokua amerudi masomoni ile laini yake ya simu atakua bado anaendelea kuitumia au haiwezekani na kama haiwezekani je kuna taratibu za kufuata ili aendelee kuitumia ile laini yake?
 
Back
Top Bottom