Ndugu mteja,
Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
Karibu
Vodacom Tanzania
Kukosea kutuma pesa na kwenda kwa mteja mwingine na mteja husika kuzitoa pesa husika.
Kweli kosa la mtumaji na kwa kiasi kama mtoa pesa akaunti yake ina pesa kwa uzoefu uliopo huwa msaidia kuzirudisha ila ugumu ni pale mhusika/mteja aliyepokea pesa isiyomhusu/ mtuhumiwa akaunti yake haina kitu hivyo kubaki kuvizia kama ataingiza pesa.
Eneo hili la kuvizia kama ataingiza pesa ndiyo na Shauri muwe na Automated Computer system inayotoa alert ya transaction ya mtuhumiwa badala ya mfumo wa Mteja aliyekosea kutuma pesa kujaribu mara kwa mara kupiga simu customer care kuulizia kama akaunti ya Mtuhumiwa inapesa au lah!.