yaani hiyo mitandao ya simu ni kero sana. Hata airtel ni janga. Unaweza kuwa unafanya kazi muhimu sana mara unasikia msg unadhani ya muhimu unakatisha kazi uione kumbe hao wapumbavu.
Bora inayokuja na namba uta screen,kuna wale wanaozileta kwa majina mara INTERNET, mara SHINDA and the like sijui uta screen nini?
Kuna muda simu inaita ukipokea tangazo! Uwiiii! Wanakeraje?
Hii inaonyesha nikwajinsi gan hali ilivyo kuwa ngumu mpaka kwenye makampuni...wanapiga debe promoshen zao ili wapate $....ilikuwa tigo sasa Voda na bado!! Na sisi wateja tunakula jiwe.
Kuna huduma yao nyingine ya PERUZI,ambayo kujiunga unatuma namba 15368.Issue inakuja kwenye kujitoa maana meseji wanazokutumia wanakata helj.JAMANI WANAJITOAJE KWENYE HII HUDUMA YA PERUZI?
nikiona ya kuanzia 15xxx nafutaga kabla ya kusoma. Nakatwa kila mwenzi buku jelo eti bima sijui nimewafata lakini wapi kila mwez nakatwa je nifanyeje lakin ni tigo.
Ndugu hauko peke ako mimi nililiwa hela mpaka nikakoma.Nilijitoa sana ila wapi kila mwisho wa mwez wanachukua chao. mara ya mwisho nilienda kwenye kituo chako k/koo msimbaz nikaivunja line mbele yao.
Namba yangu ya voda inaishia 90 .vodacom hazipiti siku 2 wananitumia mesej unasikia " Huu si utani ndugu mteja namba yako inaishia 90 imeshinda million tisin tuma neno OK kwenda ....(namba flan hv) uje uchukue million zako. yan WIZI MTUPU