Vodacom mnakera na meseji zenu mnazotuma hovyohovyo kwa wateja kwa kutumia namba 15778

yaani hiyo mitandao ya simu ni kero sana. Hata airtel ni janga. Unaweza kuwa unafanya kazi muhimu sana mara unasikia msg unadhani ya muhimu unakatisha kazi uione kumbe hao wapumbavu.
 
Imefikia wakati tiwashtaki ili watulipe fidia. hii inawezekana kabisa hawakutuandikisha mkataba wa matangazo wakati wanauza line. PERIOD
 
weka namba hiyo kwenye screen numbers. wala hutaona tena hizo msg zinazokuja kwa namaba hiyo kwenye simu yako.
Bora inayokuja na namba uta screen,kuna wale wanaozileta kwa majina mara INTERNET, mara SHINDA and the like sijui uta screen nini?
Kuna muda simu inaita ukipokea tangazo! Uwiiii! Wanakeraje?
 
Hii inaonyesha nikwajinsi gan hali ilivyo kuwa ngumu mpaka kwenye makampuni...wanapiga debe promoshen zao ili wapate $....ilikuwa tigo sasa Voda na bado!! Na sisi wateja tunakula jiwe.
 
Imefikia wakati tiwashtaki ili watulipe fidia. hii inawezekana kabisa hawakutuandikisha mkataba wa matangazo wakati wanauza line. PERIOD
huwa nakereka sana, sku nyingine huwa wanapiga simu kabisa. hivi sheria inasemaje katika hili?
 
Kuna huduma yao nyingine ya PERUZI,ambayo kujiunga unatuma namba 15368.Issue inakuja kwenye kujitoa maana meseji wanazokutumia wanakata helj.JAMANI WANAJITOAJE KWENYE HII HUDUMA YA PERUZI?
 
Vodacom mnakera na meseji zenu mnazotuma hovyohovyo kwa wateja kwa kutumia namba 15778.

Habari zingine ni za udaku! Mfano leo kuna ujumbe umetumwa "baada ya ndoa ya wasanii... kuvunjika...Risasi limeandika!"

Huwa hamchelewi kuanza kukata salio!
Wanakeraje? Nimewatumia STOP sijaziona tena
 
Wanakeraje? Nimewatumia STOP sijaziona tena

hahahaha ...... nimependa hiyo nimewatumia STOP.

Kiukweli, hizi meseji zao zinakera sana. ukitumia mpesa kidogo tu kosa wanakutiririshia meseji kibao halafu hazina hata maana.
 
Mimi nilipigiwa kutoka tigo kua umefanikiwa kujiunga nabima tembelea ofisi zetu upate kujua hospitali zetu, kweli inakera.
 
nikiona ya kuanzia 15xxx nafutaga kabla ya kusoma. Nakatwa kila mwenzi buku jelo eti bima sijui nimewafata lakini wapi kila mwez nakatwa je nifanyeje lakin ni tigo.
 
Msaada waungwana jinsi ya kujitoa Vodacom huduma ya PERUZI(15368),NIFANYEJE?
 
Mimi nilipigiwa kutoka tigo kua umefanikiwa kujiunga nabima tembelea ofisi zetu upate kujua hospitali zetu, kweli inakera.

Ndugu hauko peke ako mimi nililiwa hela mpaka nikakoma.Nilijitoa sana ila wapi kila mwisho wa mwez wanachukua chao. mara ya mwisho nilienda kwenye kituo chako k/koo msimbaz nikaivunja line mbele yao.
 
Namba yangu ya voda inaishia 90 .vodacom hazipiti siku 2 wananitumia mesej unasikia " Huu si utani ndugu mteja namba yako inaishia 90 imeshinda million tisin tuma neno OK kwenda ....(namba flan hv) uje uchukue million zako. yan WIZI MTUPU
 
Back
Top Bottom