Vodacom, mnafahamu maana ya UNLIMITED Intenet?

Vodacom, mnafahamu maana ya UNLIMITED Intenet?

Vodacom ni usanii mtupu watakwambia unlimited internet but ni uongo kwa siku unalipa 1000 unapata 700MB kwa week unalipa 7000 unapata 2048MB kwa mwezi unalipa 25000 wanakupa 5GB baada ya hapo ni speed ya konokono achana nao kabisaa full usanii mbaya zaidi hata muda wa kukwambia zimeisha ni kama wameupanga ya siku utajulishwa after 12 hours ya week utajulishwa after 36hours na ya mwezi haizidi 48hours utambiwa speed inapunguzwa yaani ni full usanii my advice afadhali kidogo Airtel
 
Kuna rafiki yangu mmoja anafanya Kazi moja kati ya makampuni makubwa ya Simu hapa nchini ashawahi kuniambia hakuna internet bundle UNLIMITED hapa bongo.

At first nikamshangaa, alipoanza kunielewesha nikamulewa.

Alisema, let's say unapewa unlimited ya wiki hapo unaweza kupewa 5gb only. Hapo 4.5 GB itakuwa very fast, na 500mb zilizobaki zitakuwa slow ajabu, na inakuwa slow till ile siku bundle lako linaenda ku expire.

Kwahiyo ndugu mi nilimuelewa sijui kama nimekuelewesha pia.
 
Ukweli wa Unlimited Za vodacom;
Siku - 1000 unapata 1 GB ukimaliza wanapunguza speed kabsa internet inakuwa slow Sana
WIKI - 7000 unapata 2 G ukimaliza wanapunguza speed kabsa internet inakuwa slow Sana
Mwezi - 25000 unapata 5 GB ukimaliza wanapunguza speed kabsa internet inakuwa slow sana

Lugha za Biashara hizo lazima uwe makini.
Basi hili ndilo dhoruba lililonikumba!!!! KAMWE SIRUDII KOSA hasa nikiwa na kazi sensitive!!! hujui vifurushi vizuri vya mitandao mingine, airtel na tigo wana unlimited au ndio kama voda?
 
Kuna rafiki yangu mmoja anafanya Kazi moja kati ya makampuni makubwa ya Simu hapa nchini ashawahi kuniambia hakuna internet bundle UNLIMITED hapa bongo.

At first nikamshangaa, alipoanza kunielewesha nikamulewa.

Alisema, let's say unapewa unlimited ya wiki hapo unaweza kupewa 5gb only. Hapo 4.5 GB itakuwa very fast, na 500mb zilizobaki zitakuwa slow ajabu, na inakuwa slow till ile siku bundle lako linaenda ku expire.

Kwahiyo ndugu mi nilimuelewa sijui kama nimekuelewesha pia.
Naskuru kwa mawazo yako mkuu!!! shida ni kwamba kwanini Vodacom Tanzania wanidanganye!!?:A S confused:
 
Last edited by a moderator:
Hawa voda ni wajinga sana. Nimenunua kifurushi ya wiki enternet bila kikomo sh 7000. Wamenitumia hii

Umefikia kiwango cha 2048MB.Endelea kutumia kwa kasi ndogo hadi tarehe ya mwisho. Kununua tena, bonyeza http://vda.cm/JazaIntaneti

Hainiruhusu hata kuingia web yoyote kirahisi. Hapa nilipo naelekea mjini kununua line ya Airtel. Vodacom go to hell!
Huko nako ni majanga jamaa angu ila kidogo wao nafuu!!! na kama ukipata vocha za UNI basi ndio burudani!!! nnachowapendea spidi yao iko constant japo sijawajua kwenye inlimited wakoje!!

https://www.jamiiforums.com/tech-ga...kutuua-watanzani-tunasubiria-vietel-sasa.html

Kwa mtazamo wangu nafuu airtel kuliko hawa wezi!!
 
Internet ya uhakika kwa hapa dar, kwa speed na kuto katakata ni SMILES tu, waliobakia wote ni wezi tu
 
Jambo la maana mnaleta u*****fu tu. maana yake Bila Kikomo. Mimi huwa pia najiuliza juu ya Huduma za internet zitolewazo na Vodacom. kiukweli ni wizi. kuna kifurushi cha 1000 tsh cha siku bila kikomo ukiweza kufungua page ya JF na ku surf kwa muda mfupi tu utagundua Kuwa tayari kifurushi kimeisha baada ya ku browse pole pole Sana na mwisho utaletewa sms Kuwa kifurushi chako kimeisha Endelea ku browse na shilingi 20 kwa dk. TCRA chunguzeni huu wizi
TTCL ndio wana uwezo wa kuwakata ngebe wamiliki wa kampuni haya ya simu - wakishusha tariff za mtandao na kuongeza kasi ya throughput, TTCL hivi sasa ina misuli ya kuwapa kashikashi washindani wao, kinacho itajika ni ubunifu wa masuala ya kufanya biashara katika shirika hilo ,wafanyakazi walio pewa dhamana ya kuendesha TTCL wasibweteke wajaribu kuiga mifano ya ma CEO wa NHC na hivi sasa CEO wa DAWASCO jamaa huyu ni mbunifu sana.

Tusijidanganye kwa kudhani TCRA inaweza kudhibiti makampuni ya simu Nchini uwezekano huo haupo kabisa mara ngapi tumeshuhudia TCRA inaitisha vikao na makampuni hayo eti wawape a way 4ward, just imagine!

Narudia kusema ulegelege wa TCRA ndio unazifanya kampuni za simu kuvimba kichwa,kuwaibia wateja kwa kutumia mbinu mbali mbali kuanzia kwenye airtime,internet bundles,kuweka services ambazo mtaje hajazi subscribe list ni ndefu sana, zinafanya wapendalo bila ya kufatiliwa kwa karibu na TCRA,sasa sijui tatizo linatokana na nini, je ni nguvu za pesa au TCRA hawajui wapi pakuanzia ili wawashikishe adabu, kusema ukweli uhuru wa makampuni ya simu yamepitiliza mipaka!
 
Mimi ni customer care mstaafu ktk hii kampuni ya Vodacom uliyoituhumu kabla ya kupata mchongo government, naomba kuchangia kwa ufupi hii hoja yako.

Kuna kitu wanaita "FAIR USAGE POLICY"

"Fair usage policy" imejikita katika suala la kuwa "fair" ktk matumizi yako usije kuchukulia "ubwete" kwamba kwa Tsh 25,000 or whatever amount you paid udownload kitu hata cha Telabyte (TB)moja au mbili....hii inakuwa haiko "fair" kwa mtoa huduma kwani na yeye analipia hizo MB/GB/TB

Utofauti wa Unlimited bundles na zile ambazo ni "limited" ni kwamba Unlimited bundles ziko "capped" kwa 700mb (daily) 2GB (weekly) na 5GB (monthly) ambazo unaweza kuzitumia kwa high speed.

Endapo utafikia hyo "cap" iliyowekwa kabla ya muda wa bundle yako kuexpire hutokatiwa Huduma ya internet bali speed ndiyo itapungua.

Tofauti na limited bundles ambazo ukishafikia ukomo wa zile MB/GB ulizopewa basi net inakata kabisa.

Kuhusu speed, maeneo mengi ya TZ Vodacom wana tumia technology ya 3G ambayo kasi yake ya juu kabisa ya kubrowse iko 3.75mb/sec

Endapo unabrowse kwa slow speed (kama umeshafikia ukomo wa zile "capped" volumes zilizo ktk unlimited bundles inashuka hadi 0.2kb/sec.. Hicho ni kiwango cha chini kabisa kutegemea na network strength ya eneo ulilopo.. Ila huwa inapanda hadi 254kb/sec haizidi hapo.

Naamini utakuwa umeelewa japo kidogo, nakaribisha wengine wajuvi zaidi yangu wakuongezee.

Asante.
 
Kuna kazi ya ku download nnayo lakini baada ya kujiunga bandle ya unlimited, naona imeanza vizuri mara ghafla hata ku load page imekua shida iko very slow na bahati mbaya zaidi hata kazi haifika nusu!

Sasa mimi nashangaa nini maana ya unlimited intenet kwanini hawa Vodacom Tanzania wasiseme ukweli mpaka tudanganyane mchana kweupe?

Je, ili niachane na huu wizi ni mtandao gani wanatoa huduma ya unlimited intenet nzuri?

Hata mahakamani watakushinda, unlimited haimaanishi "speed'.

Kiislam huwa tunasema wanacheza na mizani. Ni dhambi waifanyayo.
 
Mimi ni customer care mstaafu ktk hii kampuni ya Vodacom uliyoituhumu kabla ya kupata mchongo government, naomba kuchangia kwa ufupi hii hoja yako.

Kuna kitu wanaita "FAIR USAGE POLICY"

"Fair usage policy" imejikita katika suala la kuwa "fair" ktk matumizi yako usije kuchukulia "ubwete" kwamba kwa Tsh 25,000 or whatever amount you paid udownload kitu hata cha Telabyte (TB)moja au mbili....hii inakuwa haiko "fair" kwa mtoa huduma kwani na yeye analipia hizo MB/GB/TB

Utofauti wa Unlimited bundles na zile ambazo ni "limited" ni kwamba Unlimited bundles ziko "capped" kwa 700mb (daily) 2GB (weekly) na 5GB (monthly) ambazo unaweza kuzitumia kwa high speed.

Endapo utafikia hyo "cap" iliyowekwa kabla ya muda wa bundle yako kuexpire hutokatiwa Huduma ya internet bali speed ndiyo itapungua.

Tofauti na limited bundles ambazo ukishafikia ukomo wa zile MB/GB ulizopewa basi net inakata kabisa.

Kuhusu speed, maeneo mengi ya TZ Vodacom wana tumia technology ya 3G ambayo kasi yake ya juu kabisa ya kubrowse iko 3.75mb/sec

Endapo unabrowse kwa slow speed (kama umeshafikia ukomo wa zile "capped" volumes zilizo ktk unlimited bundles inashuka hadi 0.2kb/sec.. Hicho ni kiwango cha chini kabisa kutegemea na network strength ya eneo ulilopo.. Ila huwa inapanda hadi 254kb/sec haizidi hapo.

Naamini utakuwa umeelewa japo kidogo, nakaribisha wengine wajuvi zaidi yangu wakuongezee.

Asante.
Sasa kwanini wanatudanganya mkuu??? shukrani kwa maelezo yako!!
 
Hata mahakamani watakushinda, unlimited haimaanishi "speed'.

Kiislam huwa tunasema wanacheza na mizani. Ni dhambi waifanyayo.
Na sina haja ya kwenda mahakamani. Line yao iko kabatini.
 
Sasa kwanini wanatudanganya mkuu??? shukrani kwa maelezo yako!!

Hata ukipiga simu huduma kwa kwa wateja haya maelezo utayapata tu kama utakutana na customer care agent ambaye yuko smart otherwise ukikutana na mwingine asiyependa kujihangaisha kusoma FAQ's (Frequently Asked Questions) kwa kila product & service atakupa jibu la mkato tu kwamba "jaribu kurestart device yako" and blah blah.
 
Ndio maana hata hao TTCL wanaotoa hizo unlimited kama mnavyosema nyie gharama yake ni kubwa mno kuliko hizi za hawa Vodacom, Tigo, Airtel et al. Haiwezekan eti kwa elfu 25 upewe internet ya kufanya unachotaka kwa mwezi mzima, au upewe uhuru wa kudownload unavyotaka siku nzima hata kama utafikia Telabyte nzima kwa buku tu? Never! Well mtoa mada umeuliza why hawasemi haya...mengine ni market strategy tu mkuu ndo maana hata ile Nipige Tafu wanakuambia tu kopa mpaka kieleweke wakati in real sense mwisho wa kiasi cha kukopa ni 2000 lakini hawasemi kwenye matangazo yao kwamba mwisho ni 2000.
 
Basi hili ndilo dhoruba lililonikumba!!!! KAMWE SIRUDII KOSA hasa nikiwa na kazi sensitive!!! hujui vifurushi vizuri vya mitandao mingine, airtel na tigo wana unlimited au ndio kama voda?

Tigo , Airtel Voda wote kwa sasa hawana Unlimited!. Ngoja tuone Vietel watakuja na nini
 
Back
Top Bottom