Kampuni ya Bradda acheni wizi

( Tabata Region ) Internet Provider Yupi Mzuri

  • VODACOM

    Votes: 2 66.7%
  • SMILE

    Votes: 1 33.3%
  • TTCL

    Votes: 0 0.0%
  • AIRTEL

    Votes: 0 0.0%
  • TIGO

    Votes: 0 0.0%
  • Other

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    3
  • Poll closed .

Termux

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
406
980
Habari Jf, Baada ya kuangaika sana katika harakati za kutafuta sehemu nzuri au kampuni nzuri itakayoweza kutoa Internet nzuri ya nyumbani na ofisini kwa gharama nafuu.

TTCL : Nilitumia ka muda mfupi baadae nikaachana nao maana wazito katika kutoa huduma au ukiwa na shida inachukuwa mda mrefu kukupatia huduma. Nilitumia kifurushi cha Tsh 150,000/= kwa mwezi na bado huduma hilikuwa mbaya nikachana nacho.

SMILE : nilinunua Router ya smile pale mlimani city na kuanza kutumia internet yao. Hii kidogo niliona kuna utofauti mkubwa sana katika matumizi yangu ya internet. Kifurushi cha mwezi unlimited kwa Tsh 185,000/= Nilifikisha mpaka katika mwezi 2TB ya mathmizi ya internet kwa mwezi. Hii ilikuwa nzuri sana ila baada ya miezi kama 8 mara mda mwengine internet inakuwa akuna au laini aisomi. Bar za network zinakuwa chini mara no servise. Ilikiwa shida sana mpaka nikahamua kutaguta mbadara mwengine wa internet. Maana wengine kazi zetu aziendi mpaka internet. Maisha yetu na kazi zetu za kila siku bila ya internet kunakuwa akuna kazi. Nyumbani internet na ofisini pia internet. Nikaachana nao

BRADDA : Kwasasa natumia internet ya hawa jamaa mana kuna rafiki yangu kaweka mwake hawa jama ananiambia wapo vizuri sana. Na mimi nikapata tamaa ya kuwajaribu nione maana wana 5G internet kwa kutumia router za Nokia. Baada ya mwezi wa kwanza kujiunga niliambiwa Tsh 150,000/= speed 30MBps kwa mwezi Unlimited, iko vizuri sana. Baada ya ku sain mkataba wao nikaambiwa nitoe Tsh 300,000/= kwa maana ya 150k kwa security na 150k iliobaki ni internet ya mwezi kwaiyo jumla inakuwa 300k nikalipa.

Sasa majuzi kati hapa nipi nao mwezi wa pili huu natumia internet yao, mara naona notifications za voda. Ikabidi niwapigie voda nione kifurushi vyao vikoje.

Home / office 5G intenet ni Tsh 120,000/= 30MBps hii ambayo nalipia kwa 150,000/= 30MBps Bradda. Nikachoka sana maana 150k kwa voda 5G ni 50MBps. Ikabidi niulizie Router ya voda ya 5G ni bei gani? Nikaambiwa ni Tsh 600k router peke yake. Nikanunua teyari nnayo home hapa ya voda. Kwaiyo router ya voda nmenunua imekuwa yangu kabisa kazi yangu mimi ni kulipia internet bundle tu kila mwezi. Nalipia Tsh 150k unlimited kwa speed ya 50MBps.

Maoni yangu kwa wapenda Internet
VODACOM:
ni sehemu sahihi ya kutumia internet, kwa mtazamo wangu mimi kulingana changamoto nilizo pitia hapo nyuma. Tsh 150k speed ya 50MBps kwa mwezi na Unlimited. BRADDA WAMEKUWA Broker au watu wa kati. Wananunua voda internet kwa 120k arafu wanajifanya 150k kwa speed ndogo kabisa.

Kama kuna internet provider mwengine mzuri zaidi tuambizane humu katika huu uzi. Karibuni jamani. Mimi nipo Tabata zuku azijafika huki bado na nilikiwa nafatilia Starlink kwa baadae.
 
Back
Top Bottom