Mkuu hata mie nimekuwa nikijiuliza kwa nini watu wanaidharau sana MTK?? Sijapati Jibu la kuniridhisha!
MTK mpya zipo vizuri perfomance wise, ila mpaka leo makampuni Yana Tabia ya kuchagua MTK mbovu na kuuzia watu, mfano Helio p22 imetumika sana na sio tu makampuni madogo even makampuni makubwa kama Samsung, Oppo, vivo etc wanatumia, wanachofanya wanakujazia storage kubwa na ram kubwa unaingia kichwa kichwa simu ina 4gb ram unanunua.
Kikawaida MTK zina mapungufu haya kwa hizi za kisasa.
1. Drivers za GPU si nzuri na hili si la MTK hata kirin za Huawei na Exynos za Samsung wote wanatumia Mali GPU, drivers zake si nzuri compare na Adreno za Snapdragon, hasa drivers za open Gl. Kuna baadhi ya apps unakuta soc ya snapdron inatumika simu za laki 3 ina perform vizuri kuliko mediatek ama Kirin za milioni.
2. MTK hawatoi source code za chip zao, hii ina leta ugumu kwa madeveloper kutengeneza software mbalimbali kwa ajili ya simu, vitu kama Mods, custom rom etc ni ngumu kutengeneza kwenye simu za MTK.
Mambo ambayo wame improve (mtk za kisasa tu za dimensity ama Helio G series)
-wame improve ukaaji chaji Sababu siku hizi wanatumia manufacturing process za kisasa
-perfomance si haba mpaka simu za low end wanaweka cores kubwa
Mwisho wa siku mkuu, ukiamua kuchagua simu ya MTK basi Hakikisha kwenye price point hakuna Snapdragon inayokaribia hio perfomance, ila perfomance zikiwa sawa Chukua tu snapdragon.
Xiaomi huwa anajua sana kutumia MTK, mfano redmi 9 kwa around laki 3 ina helio G80, hakuna snapdragon kwa price point hii inayofikia perfomance yake. Hivyo unajifuta machozi kwa kupata perfomance kubwa kufidia hizo weakness.