TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 6,735
- 20,787
Kwa nijuavyo mimi, endapo ikatokea kweli wakaja viumbe kutoka nje ya sayari yetu kutuvamia, sisi hatutakuwa na chochote cha kufanya.Nimeona hii habari ila nikaipuuza baada ya kuona Trump bado anapandishiana mabega na Urusi.
Unless IQ yetu iwe ndogo mno ila kama tuna IQ ya kawaida tu, ikiwa kuna hatari halisi ya ujio unaosemwa binadamu wote tutakuwa na adui mmoja hatari zaidi si rahisi kutishiana NUKE wenyewe kwa wenyewe katika mazingira kama haya.
Kiumbe mwenye teknolojia ya kutengeneza chombo cha ukubwa wa Manhattan kinachoruka angani kwa spidi hiyo iliyotajwa, hatuna cha kumfanya, ukizingatia sisi hata teknolojia ya kufika hapo Mars hatuna. ๐