Vitu vya uongo tunavyoonyeshwa kwenye muvi za kizungu

Tena ya mguu 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 au ngumi moja tu anazima jumla
Kuna hiyo "Welcome to sudden death" Star aliua adui na kikopo cha coca, alimpiga kikopo cha uso dada chali hajaamka mpaka movie inaisha
 
Kuna hiyo "Welcome to sudden death" Star aliua adui na kikopo cha coca, alimpiga kikopo cha uso dada chali hajaamka mpaka movie inaisha
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 hivi ndio vitu sasa vinavyofanya tulalamike sio kama hatuna sababu ya msingi ya kulalamika
 
Unatembea zako njiani uko bize na simu. Ghafla unagongana na mdada aliebeba makorokoro kibao na yanaanguka chini (always huyu mdada lazima awe pisi kali). Anachuchumaa kuyaokota na wewe unamsaidia.

Wakati mnayaokota unamshika mkono.. anakuangalia usoni na wewe unamuangalia macho yanagongana... mnaangaliana kama dakika mbili halafu taratibu mnaanza kusogeleana mpaka midomo inakutana mnakiss, mvua inaanza kunyesha na kuanzia hapo mnakua wapenzi! Kesho yake mnaonekana mko beach mnakimbizana na kumwagiana maji....Life is so easy kwenye movies.😂😂
🤣 🤣 kina sharukani ndo zao hizo kila muvi!
 
Na unakuta dakika mbili zilizopita huyo adui (ambae ni muuaji wa kutisha) alikutana na huyo mpenzi wa staring kwenye ngazi, akampiga ila hamuui anamuacha amelala hapo na bastola ipo pembeni ndio anamfata staring. 🤣🤣🤣 Jamaa wanatuona maboya sana
🤣🤣🤣
 
Huu uzi umenichekesha sana

Mambo mengi yaliotajwa yanapatikana sana kwenye movies za zamani na action movies
 
Star hata apigwe risasi hua hafi anaweza chezea kichapo cha hatari ila mwishoni utashangaa eti yeye ndio anashinda. Wakati huo huo maadui wakipigwa ngumi moja tu wanazima moja kwa moja wala hawaamki tena asilani


Ngumi moja tu mtu kakata moto.
 
Wahindi sio watu wazuri hawataki ujinga ujinga kabisa we mtu anaruka fuso unazani mchezo
Gari ile kubwa (van) inatumika kama silaha ya kuadhibia watu!!! yaani maadui wanakuja mbio wakiwa na silaha basi kabla hawajamfikia staa anaikanyaga buti gari inaserereka na kuwakumba na kuwaua wote (tena gari hiyo inawakumba kiupande upande- siyo kwenda mbele wala nyuma)

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Ndio mkuu muvi zote maadui/majambazi hua wanaishia kuuawa 😀
Kaka ile ni sanaa,na moja ya kazi ya sanaa ni kufundisha na kuelimisha.
Hapo jamii inaelimishwa kuwa ukijihusisha na mambo mabaya hususani ujambazi,mwisho wake ni mbaya.
 
Back
Top Bottom