Mwanzo mwisho jinsi Filamu ya Moana ilivyotengenezwa. What a masterpiece!

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,686
106,811
Aloha kakahiaka.... 👋👋

Kama wewe ni mpenzi wa kutazama mieleka kwa muda mrefu na unawafahamu baadhi ya wacheza mieleka utagundua kwamba michoro/tattoo zilizopo kwenye mikono na mabega ya The Rock (Dwayne Johnson), Roman Reign, Jimmy and Jey (the Usos), umaga nk zinafanana.

Sababu inayofanya tattoo zao zifanane ni kwakua hawa wote ni ndugu(cousins), wanatokea kwenye familia ya wacheza mieleka inayofahamika kama Anoa’I Family. Familia hii imetoa wacheza mieleka wengi sana toka miaka hiyo mpaka leo hii wakina Roman Reign bado wanawakilisha familia, familia hii imetoka katika mji/kisiwa wa samoa.
images (6).jpeg

[Roman Reign na The Usos]

Lakini pia ukimtazama mwigizaji Jason Momoa utagundua pia anafanana kwa kiasi Fulani na watu hawa japo sio ndugu wala hawatoki eneo moja maana yeye anatokea Hawaii ila michoro yake pia iliyopo kwenye mikono yake inaendana na ya akina The Rock.
images (7).jpeg

[Mwigizaji Jason Momoa]

The Archipelago, literally…

Polynesia
ni eneo lililopo katika bahari ya Pacific ambalo limeundwa na Zaidi ya visiwa Zaidi ya elfu moja vilvyosambaa katika maeneo ya katikati na kusini mwa bahari ya pacific. Wakazi wa eneo hili wanafanana vitu vingi sana ikiwemo lugha,tamaduni, Imani nk

Inasemekan karne kadhaa zilizopita walikua wanatabia ya kusafiri pamoja majini (sailing) wakati wa usiku wakitumia nyota ka dira zao. Archipelago ni mkusanyiko wa visiwa vingi vilivyopo pamoja hivyo basi Polynesia imeundwa na archipelago kadhaa kama vile viiwa vya Hawaii, visiwa vya samoa na Tonga...New Zealand ndio eneo kubwa Zaidi katika eneo la Polynesia. Tafiti za wasomi wa lugha,wataalam wa DNA za binaadam, wachimbuaji/ archaeologist zinaonyesha kwamba asili ya watu wa Polynesia wametokea nchi ya Taiwan na kwa kiasi kidogo Vietnam, Comoro, Cambodia, Myanmar na Thailand.

Kama ni mfuatiliaji wa muvi uliebobea utagundua kwamba muvi nyingi sana zenye mazingira ya milima au maji mara nyingi sana hua zinarekodiwa (shooting) katika kisiwa cha New Zealand zipo muvi nyingi sana ambazo zimeigiziwa huko kama vile King Kong, Avatar zote, Lord Of the Ring zote, Mission Imposible fallout, Hobbit zote, Mulan, alien convenant, X-men Origin, Chronicle of Narnia, Anaconda, Aquaman, na zingine nyiingi…! Sababu kuu ni kutokana na kwamba new Zealand ina mazingira mazuri sana ya kila aina kwa kushoot film, lakini pia erikali yake imewekeza nguvu kubwa katika film industry.
images (8).jpeg

[New Zealand landscape]

Huko juu tumeona kwamba the rocky,usos bros, Roman Reign wanafanana michoro iliyo katika mabega yao tukajua ni kwa sababu hawa ni ndugu wa ukoo mmoja lakini pia mwigizaji Jason momoa naye michoro yake inafanana nay a akina the rocky japo yeye hatokei samoa bali anatokea Hawaii, sababu kuu ni kwamba wote hao wapo katika ukanda hua wa Polynesia ambapo tamaduni zao zinafanana ndio maana hata michoro yao inafanana japo hawatoki eneo moja bali ukanda mmoja.

Katika simulizi za kigiriki neno demigod huwa inamaanisha mwanadamu ambaye anakuwa na nguvu Fulani za kimungu yaani anakua nusu mwanandamu nusu mungu kutokana na uwezo wa kutenda mambo mbalimbali, wagiriki pia wanasema demigod ni mwanadamu ambaye ametokana na miungu. Mfano katika Imani za wagiriki wanasema miungu yao ilikua ina tabia ya kuwazalisha wanadamu na kutoa watoto wenye nguvu za ajabu kama vile Hercules, perseus, Achileus nk.

Kwa mantiki hiyo hata Yesu wa Nazareth ni Demigod. So, katika ukanda wa Polynesia kulikua kuna demigod aliyefahamika kwa jina la Maui inasemekana aliabudiwa na kupendwa kama shujaa wao katika ukanda huo. Watu wa huko wanasema kwamba maui alikua anauwezo wa kwenda kuzimu na kuiba moto kisha anawaletea wanadamu wautumie, alikua analiziwia jua lisitembee ili siku iwe ndefu, alikua anavua visiwa vilivyozama baharini kwa kutumia ndoana yake ya ajabu. Kiufupi jamaa alitumia nguvu zake kuwasaidia watu wa maeneo hayo inasemekana mpaka leo hii bado anaheshimiwa.
images (9).jpeg

[Maui kwa mujibu wa Polynesian Mythology]

Kuna jamaa mmoja anaitwa John Musker ni direct wa muvi hasa animation katika kampuni ya Walt Disney Animation alikua anasoma kuhusu simulizi za huko Polynesia akawa amevutiwa na habari za maui, ikabidi amshirikishe rafiki yake ambae ni director pia Ron Clement kwamba watengeneze animation itakayohusu maisha ya Maui. Mwaka 2011 wakaandaa proposal wakapeleka kwa CEO wa Walt Disney animaton bwana John Lasseter, Lasseter akapenda proposal yao akawaambia basi waende wakafanye research juu ya stori hizo huko Polynesia….hivyo mwaka 2012 Musker na clement wakapiga safari ya kwenda kufanya utafiti katika visiwa vya Tahiti,Samoa na Fiji ili waweze kuongea na kupewa taarifa sahihi juu ya stori za maui kutoka maeneo hayo.
images (10).jpeg

[Ron Clement na Jon Musker Directors wa muvi ya Moana]

Katika tafiti zao director hao walivutia na kuambiwa kwamba watu wa Polynesia walikua wanafanya safari za masafa marefu(voyage) baharini lakini baadae wakaacha, inasemekana kwamba mabaharia wa Polynesia walikua washatabiri ujio wa wa wapelelezi wa kizungu kabla hata ya christofa Columbus hajafikiria kwenda America lakini miaka kama elfu moja mbele walirudia kufanya zile safari zao za masafa marefu. Hivyo basi clement na musker walitaka watengeneze muvi itakayokua inahusu watu wa Polynesia kufanya safari zao na kusitisha kisha kuanza tena huku muhusika mkuu wakitaka awe maui.

Clement na musker wakaajiri watu ambao watakua wanafatilia uhalisia was tori ya muvi nzima ili iendane na tamaduni za Polynesia Ishu ikaja kwa maui walitaka awe na kipara ila wenyeji wakasema maui alikua hana kipara bali nywele nyingi, unaambiwa story ya muvi ya moana ilipitia mabadiriko mara tisa hadi ikakamilika…hata moana mwenyewe hakutakiwa kua main character wa muvi bali maui, story nyingine ilikua inataka baba yake moana ndio awe main character ambae atahamasisha watu warudie kufanya safari zao za baharini ili ikafutwa ikaandikwa upya….mwaisho kabisa story ya moana hii tunayoijua leo hii ikapita. Kazi ikawa kumtafuta actors watakaoigiza.
images (13).jpeg

[Observe The Rock tatoo]​

Mamia ya watu walifanyiwa interview ili kupata atakae endana na character bahati ikamuangukia binti mmoja aitwae auli’I cravalho enzi hizo akiwa na miaka 14. Karibia ya waigizaji wote walioigiza kwenye hii muvi wanatokea Polynesia. Auli’I (moana), Nicole scherzinger(mama moana) wote hawa wana asili na wazaliwa wa Hawaii. The Rocky (maui) anatokea samoa. Rachel house (bibi moana), baba moana, tamatoa wote hawa ni wazaliwa wa Maori.
images (11).jpeg

[Auli'i Carvalho akiwa na miaka 14]​

2016 muvi ikatoka ikawa global hit, hakuna mtu ambae ameshaiangalia hii muvi akaacha kuipenda. Moana katokea kua character maarufu sana watoto wote wanampenda...Kwa mujibu wa Disney Live action ya muvi ya moana ipo jikoni inategemea kutoka 2025. The Rock ndio atakuwepo as Maui! Ngoja tuone watatuletea nini.
images (12).jpeg

Signing Out...
Da'Vinci 🤞✌️​
 
Shiny Lyrics

Well, Tamatoa hasn't always been this glam
I was a drab little crab once
Now I know I can be happy as a clam
Because I'm beautiful, baby
Did your granny say listen to your heart
Be who you are on the inside
I need three words to tear her argument apart
Your granny lied
I'd rather be
Shiny
Like a treasure from a sunken pirate wreck
Scrub the deck and make it look
Shiny
I will sparkle like a wealthy woman's neck
Just a sec
Don't you know
Fish are dumb, dumb, dumb
They chase anything that glitters (beginners)
Oh, and here they come, come, come
To the brightest thing that glitters
Mmm, fish dinners
I just love free food (free food)
And you look like seafood (seafood)

Jadda
FB_IMG_17053392321407987.jpg
 
Shiny Lyrics

Well, Tamatoa hasn't always been this glam
I was a drab little crab once
Now I know I can be happy as a clam
Because I'm beautiful, baby
Did your granny say listen to your heart
Be who you are on the inside
I need three words to tear her argument apart
Your granny lied
I'd rather be
Shiny
Like a treasure from a sunken pirate wreck
Scrub the deck and make it look
Shiny
I will sparkle like a wealthy woman's neck
Just a sec
Don't you know
Fish are dumb, dumb, dumb
They chase anything that glitters (beginners)
Oh, and here they come, come, come
To the brightest thing that glitters
Mmm, fish dinners
I just love free food (free food)
And you look like seafood (seafood)

Jadda
View attachment 2876586
Huu ndio wimbo nilioupenda zaidi kwenye Moana, jinsi huyo crab anavyoringa nilikuwa nacheka sana.

Umeandika vizuri 👏🏽👏🏽
 
Huu ndio wimbo nilioupenda zaidi kwenye Moana, jinsi huyo crab anavyoringa nilikuwa nacheka sana.
Napenda sana scene ya Tamatoa na moana, mwenyewe anaringa na uzuri wake anatembea anatikisa kabisa😀
Mwishoni muvi inaisha alionekana tena anaomba wamgeuze maana alivyoanguka aliangukia mgongo akashindwa kuinuka.
BTW napenda mwanya wa Tamatoa 🤣
.....
[Moana, who is covered in sparkling seashells, is snatched up by Tamatoa]

Tamatoa:
Oohh hoo hoo hoo hoo... What have we here? It's a sparkly, shiny... Wait a minute. [tosses Moana into the air, making her lose the seashells covering her] Ugh! It's a human! What're you doing down here in the Realm of the Mons–? [Tamatoa's eyes are twitching differently causing Moana to constantly look back and forth between them] Just pick an eye, babe. I can't... I can't concentrate on what I'm saying if you keep- Yeah, pick one. Pick one! You're a funny-looking little thing, aren't ya? [toys with Moana's necklace]

Moana:
Don't! That's my grandma's!

Tamatoa:
[high-pitched voice] "That's my grandma's!" [angrily] I ATE MY GRANDMA! And it took a week, 'cause she was absolutely humongous. Why are you here?!

[Behind him, Maui slips and makes a noise while trying to retrieve his hook, nearly making Tamatoa look]

Moana:
[distracting him again] 'Cause you're amazing! And we mortals have... heard of the tale of the crab, who became a legend! And I had to know how you became so... "crab-ulous"? [chuckles nervously]

Tamatoa:
[suspicious] Are you just trying to get me to talk about myself? Because if you are... [happily] I will gladly do so!

Moana:
Huh?

Tamatoa:
In song form!
Umeandika vizuri 👏🏽👏🏽
Thanks for Appreciation mkuu. Bless✌️
 
Uzi mzuri sana. Just imagine mtoto wa dada angu aliyezaliwa mwaka 2016 ndio anaipenda balaa kmchakushangaza hadi mtoto wangu wa mwaka 2020 naye ndio movie ya kumbembelezea na anaipenda balaa. Nimefuta movie zote kwa PC ila kuna animations siwezi kuzifuta Moana, The Incredibles, The Super Mario Brothers, Bellerina, The Grinch. Hizi watoto wangu wanazipenda balaa.
 
Back
Top Bottom