Vitu vya uongo tunavyoonyeshwa kwenye muvi za kizungu

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
4,974
15,310
Wengi hua tunadhani muvi za bongo tu ndio zina vitu vya hovyo. Kiukweli muvi za kizungu pia zina maujinga mengi yasiyo na uhalisia. Hivi ni kati ya vitu vya uongo na vinavyokera hasa kwenye muvi za kizugu.

1. Bunduki kutokuisha risasi. Ushawahi ona kwenye muvi mtu ana ki bastola au SMG anamwaga risasi lisaa lizima na haziishi? Uongo mtupu.

2. Watu kupigana juu ya treni huku inatembea! Hiki ni kitu cha hovyo kabisa hata kukiwaza tu. Hata kupigana juu ya treni iliyosimama ni shughuli pevu achilia mbali inayotembea.

3. Bomu la kutegwa kupiga alarm kabla ya kulipuka. Wanajeshi wanaingia kwenye nyumba, hawajui kama kuna bomu. Mara wanasikia mlio pi pi pi pi pipipipipipi...Booom! 😆 saa hiyo wanakua wameshatoka nje.

4. Watu wema kushinda. Katika muvi karibu nyingi, wale watu wema hua wanashinda na watu wabaya wanauawa. Hii haina uhalisia wowote kwenye maisha ya kawaida.

5. Kuwasha gari kwa kuchomoa nyaya chini ya usukani na kuzigusanisha. Japo hii inawezekana, lakini ni ngumu mno kutekelezeka kiuhalisia. Hata fundi mwenye vifaa, inakuchukua muda mrefu sana kufanikisha hili.

6. Maadui kuweka bunduki chini ili wapigane ngumi 😂

Hebu na wewe ongezea vitu vya kijinga ulivyowahi kuona kwenye movie
 
Ndo mana zikaitwa muvi mkuu ziko kwaajili ya kuburudisha..Japo Wenzentu wanajitahid sana kuleta uhalisia tofauti na sisi ambao licha ya uongo unakuta muvi ina makosa kibao usishangae script moja mtu kavaa nguo mbili tofauti

Ni kweli mkuu lakini wangepunguza uongo kidogo. Nyingine ni ile eti unakuta maadui kama 10 wanapigana na Jet Li ila wanaenda mmoja mmoja anawapiga mpaka wanaisha 😂 Sasa si wamrukie wote kwa pamoja mbona easy wangeshammaliza 😂😂
 
Back
Top Bottom