Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Vitu sita ambavyo si viumbe vya Mungu

Mwanao anatoka shule anatembea njiani kuja nyumbani kwako.

Ile njia si makazi ya kudumu, nyumbani ndiyo makazi ya kudumu.

Wwewe mzazi una uwezo wa kufanya njia iwe safi haina miiba, au una uwezo wa kumuwekea miiba kemkem.
Kwa nini umuwekee mwanao miiba ya mbigiri njiani, wakati uliweza kumsafishia njia iwe safi haina miiba?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu usio na mabaya yoyote, hapa ambako si makazi ya kudumu na huko kwenye makazi ya kudumu?

Huko kwenye makazi ya kudumu unaweza kuthibitisha kwamba kupo?

Nikikwambia ni stories tu za kujifariji, unaweza kutoa uthibitisho kwamba kupo?
Kwenye njia hii Mungu ameweka mbigili na miba lakini ametupa utashi wa kufahamu mbigili na miba. Pia maumivu yakizidi ukimuomba msaada hutashangaa kumuona Kiranga akiwa kwenye 404 akakupa lift mpaka mlangoni. Ni kuwa ametumwa na Mungu.
 
Well kwakua walikuwa navwazazi wao
Unaelewa kuwa tsunami ile wanyama wote walipata utashi wa kuondoka msala ule waliuvaa binadamu tu? Kwanini?
Hujajibu swali la vichanga.

Mungu gani mkatili hivyo? Hujajibu. Ukisema "kwa kuwa walikuwa na wazazi wao" ndiyo unajibu nini hapo?

Hujanieleza inakuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote anaachia vitoto vichanga vinauawa kikatili bila msada.

Kuhusu wanyama, one does not need God to explain that.

Soma hapa

Did Animals Sense Tsunami Was Coming?

"Earthquakes bring vibrational changes on land and in water while storms cause electromagnetic changes in the atmosphere," he said. "Some animals have acute sense of hearing and smell that allow them to determine something coming towards them long before humans might know that something is there."
 
Kwenye njia hii Mungu ameweka mbigili na miba lakini ametupa utashi wa kufahamu mbigili na miba. Pia maumivu yakizidi ukimuomba msaada hutashangaa kumuona Kiranga akiwa kwenye 404 akakupa lift mpaka mlangoni. Ni kuwa ametumwa na Mungu.
That is a ridiculous logic.

Yani Mungu hana kazi anajitekenya mwenyewe halafu anacheka mwenyewe?

Kwa nini uweke mbigiri njiani makusudi, halafu umpe mtoto ujuzi wa kufahamu na kuepuka mbigiri?

Kwa nini usifanye kusiwepo na mbigiri to begin with ili kusiwe na haja ya mtoto kuepuka mbigiri kabisa?
 
Hujajibu swali la vichanga.

Mungu gani mkatili hivyo? Hujajibu. Ukisema "kwa kuwa walikuwa na wazazi wao" ndiyo unajibu nini hapo?

Hujanieleza inakuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote anaachia vitoto vichanga vinauawa kikatili bila msada.

Kuhusu wanyama, one does not need God to explain that.

Soma hapa

Did Animals Sense Tsunami Was Coming?

"Earthquakes bring vibrational changes on land and in water while storms cause electromagnetic changes in the atmosphere," he said. "Some animals have acute sense of hearing and smell that allow them to determine something coming towards them long before humans might know that something is there."
Watoto huzaliwa bila dhambi zaidi ya dhambi ya asili tuliyoirithi kutoka kwa Adam na Eve.
Tunaamini watoto ni malaika na kufahamu kwa watoto wana kwenda mbinguni. Kifo ni mwisho wa kila binadamu. Kheri yao wafao bila dhambi
 
That is a ridiculous logic.

Yani Mungu hana kazi anajitekenya mwenyewe halafu anacheka mwenyewe?

Kwa nini uweke mbigiri njiani makusudi, halafu umpe mtoto ujuzi wa kufahamu na kuepuka mbigiri?

Kwa nini usifanye kusiwepo na mbigiri to begin with ili kusiwe na haja ya mtoto kuepuka mbigiri kabisa?
Mbigili ni sehemu ya mitihani uliyowekewa ili ufike mbinguni. Hakuna free lunch we have to work on the better life of the eternity.
 
Watoto huzaliwa bila dhambi zaidi ya dhambi ya asili tuliyoirithi kutoka kwa Adam na Eve.
Tunaamini watoto ni malaika na kufahamu kwa watoto wana kwenda mbinguni. Kifo ni mwisho wa kila binadamu. Kheri yao wafao bila dhambi
Nimekuuliza uthibitishe kwamba huko mbinguni kupo kweli, na si stories tu.

Hakuna mtu aliyethibitisha.

Hakuna anayeweza kuthibitisha sasa.

Hakuna atakayeweza kuthibitisha.

The same applies kwenye uwepo wa Mungu.

Kwa sababu Mungu hayupo, na hivyo mbinguni hakupo.

Kama unabisha, thibitisha na mbinguni (peponi) kupo.
 
Mbigili ni sehemu ya mitihani uliyowekewa ili ufike mbinguni. Hakuna free lunch we have to work on the better life of the eternity.
Unaweza kuthibitisha mbinguni kupo na si stories tu?

Unaelewa kwamba, ukisema "hakuna free lunch" unakataa uwepo wa Mungu?

Unaelewa kwamba the idea of your God existing represents the ultimate free lunch?
 
Unaweza kuthibitisha mbinguni kupo na si stories tu?

Unaelewa kwamba, ukisema "hakuna free lunch" unakataa uwepo wa Mungu?

Unaelewa kwamba the idea of your God existing represents the ultimate free lunch?
Mark 10:17-30 A man run up to Jesus, knelt before him and put this question to him ‘Good master what must I to inherit eternal life?
In the end Jesus told him go and sell you own and give the money to the poor and you will have treasure in heaven
 
""Atakujibu Mungu"" katu hutanielewa sababu ulishaniambia hutaki kuamini, So hayo maswali yako ya simultaneous equation utamuuliza Mungu mwenyewe siku akija kisha utampa fact zako zote za sayansi yako kwamba yeye hayupo. Sayansi yako ni kubwa naamini hata Mungu atazishangaa... 🙄
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Umepest tena!!
1).Wewe umejuaje kama alikuwa na uwezo alafu baadae ukatambua kwamba ameacha tu,hakuumba hivyo unavyovitaka na akaumba nje ya hivyo?.
2).Kwanini unataja neno "KAUMBA" kwanini usichote neno lingine.Unadhani neno"KAUMBA" na neno "MUNGU" unavitaja kwa kuvihusisha,na kwanini huwezi kuhusisha vinginevyo???

3).Wewe Kiranga unatrick nyingi umeona hoja ya kuthitisha uwepo wa nimeimaliza sasa naona umekuja na 'B' yake.
4).Unatakiwa utoe majibu ungejuaje kwamba hili ni ZURI kama kusingekuwa na BAYA??? ndo tutazame hekima ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake.Mfano;
Kama kungekuwa na usiku tuuuuuu! bila ya kuwepo mchana au kama kungekuwa na mchana tuu bila ya usiku siku zingehesabikaje??
Hiyo 'umepest tena' imenichekesha sana![emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mark 10:17-30 A man run up to Jesus, knelt before him and put this question to him ‘Good master what must I to inherit eternal life?
In the end Jesus told him go and sell you own and give the money to the poor and you will have treasure in heaven
If eternal life does not extend to life on earth, it is not eternal life.

Do you understand that?

Hujajibu swali la free lunch.

Umesema Mungu katupa mitihani ka sababu hakuna fre lunch.

Unaelewa dhana ya kuwapo Mungu inatuambia Mungu ni free lunch?

Hujanijibu.
 
Watoto huzaliwa bila dhambi zaidi ya dhambi ya asili tuliyoirithi kutoka kwa Adam na Eve.
Tunaamini watoto ni malaika na kufahamu kwa watoto wana kwenda mbinguni. Kifo ni mwisho wa kila binadamu. Kheri yao wafao bila dhambi
Hivi kabla ya binadamu kuletwa duniani, Mungu anauwezo wa kujua kama mtu huyu ninaye muumba akienda duniani atakuwa ni mzinifu na mwishoni atakufa akiwa wa motoni au hajui?
 
Kabla mimi cjakusaidia kukupa majibu ya haya mawzo yako nijibu hili kwanza.
Mungu ninan? Ukipata jibu hilo utakuwa umepata majibu yote.
Nitakudokeza kidogo then utupe jibu ya hilo swali langu.
Kwanza nataka kukuambia tunamfahamu Mungu kwa sehem ndogo sana. Lakin ile super power yenyewe ni kubwa kuliko uwezo wetu wa kufikir. So huyu mzee kajifunua kwetu kwa sehem ndogo sana.
 
Unashindwa kuelewa kwamba kuna tofauti ya kuumba ulimwengu ambao una mema na mabaya halafu ukawafanya viumbe wako misukule kwa sababu hawajui mabaya na kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya na hivyo viumbe wako wasipojua mabaya si misukule kwa sababu hakuna mabaya at all.

Kwa nini mungu karuhusu mabaya wakati angeweza kuumba ulimwengu usio na mabaya?

Na mimi ngoja nijaribu kuelezea ninavyofahamu; Mungu aliumba mema na mabaya ili awaone watu aliowaumba kama watampenda na kuzifuata amri zake au vinginevyo. Kwa nini?
Mungu ni wa haki, kwa vile ni wa haki, asingependa wanadamu wawe na maisha ya kulazimishwa kufanya mambo ambayo angependa yeye tu. Kumbuka pia kwamba, hapa duniani sisi ni wapitaji na wasafiri tu, wenyeji wetu ni huko katika maisha ya milele, eidha motoni au peponi alipo yeye. Hapa duniani ni kama tuko katika mtihani, tukishinda ndipo sasa tutaishi maisha ambayo hatutaweza tena kutamani dhambi; ni huko mbinguni. Hii imetokana na sisi wanadamu kuuharibu mpango wake wa kwanza aliotupa katika ile bustani ya Edeni hapa duniani. Sasa, ili tuwepo alipo yeye, kwa mara nyingine, ametupa mtihani huo wa kufanya yaliyo mapenzi yake hapa duniani, ambayo kimsingi kila mwanadamu anayafahamu, hata wewe unayesoma habari hizi, ametupa kuchagua.

Imeandikwa katika Yoshua 24:15 ;“ Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao...; " Na kwa jitihada zetu sisi wenyewe hatuwezi kufanya yanayompendeza Mungu mpaka tupewe msaada, na msaada sasa unatoka kwa Kristo Yesu. Hilo ni swali gumu pia! Kwa Yesu kivipi? Mimi nazungumzia kwa upande wa wanaojitambia kuwa ni wa-Kristo. Baada ya mwanadamu kuupoteza ule mpango wa Mungu ambao alitaka tuishi milele hapa duniani, Mungu aliuanzisha mpango mwingine wa wokovu kwa njia ya Yesu Kristo. Baada ya mwanadamu kuwa ametenda dhambi, alimleta mwanae wa pekee, Yesu Kristo ambaye kimsingi alikuwa hana asili ya dhambi kama ilivyo kwa wanadamu wote, akamleta huyo ili kila atakaye mwamini asitende dhambi, maana yake ni kwamba atampa uwezo wa kushinda dhambi, lakini ni wale tu watakaokubali na kumwamini; siyo wote. Imeandikwa katika;

"Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake" Hivyo kama hujampokea Yesu, hujawa bado kuwa mtoto wa Mungu, ndiyo maana unakuwa na maswali yasiyo na kikomo, huwezi kuelewa. Kuna maandiko mengine yanasema, mambo ya rohoni hutambulika kwa jinsi ya rohoni, katika 1Wakorinto 2:14-15 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. " Unaona!, hatambuliwi na mtu, maana yake ni kwamba hata wewe unaona ni kama upuuzi, lakini ndivyo ilivyo.

Nisitoke nje ya mada, kwa nini Mungu ambaye tunasema ana uwezo wote hajamfanya mwanadamu kufanya mema ili asitupwe huko kunakoitwa Ziwa la moto? Kama nilivyoeleza hapo juu, ni kwamba; hapa duniani tuko katika mtihani, Mungu anatupima baada ya kutupa uelewa wote wa kujua mema na mabaya, je tutafanya mabaya au mema? Hapa kimsingi siyo petu tena, na kama kungekuwa hakuna majaribu, basi kungekuwa hakuna kufa maana ukamilifu umefika. Tupo chuo, tukimaliza tunarudi mitaani na matokeo yetu, iwapo tumefaulu tunapata kibali cha kuwa na Mungu iwapo tumepata zungusha au tumeshindwa viwango alivyoviweka tunakuwa takataka, hatuhitaji tena kule kwake, anatuchoma kama takataka. Huu ni mpango wake aliojiwekea mwenyewe, hatupaswi kuhoji, ametuwekea dhamiri ndani mwetu inayotushuhudia, kwamba tuko katika dhambi au la. Mtu yoyote awe didi gani, awe anayeitwa ameokoka sijui nini; wooote wamewekewa dhamiri ambayo ndiyo itakayowahukumu. tunaona hayo katika kitabu cha Warumi; Warumi 2:14-15 tunasoma; Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea; Unaona! Watu wa mataifa ni watu gani! Ni watu ambao hawaamini juu ya mpango wa Mungu wa wokovu, japo wanasema wanaamini, lakini hawajakubali kuokolewa, yaani kutubu dhambi zao kwa kumaanisha kuziacha na kuomba neema ya Kristo ya ushindi dhidi ya dhambi hizo. Hayo kwa wengi pia ni mambo yasiyoeleweka! Sina lugha nyingine.

Mtu ambaye anakuwa na swali kwamba, kwanini Mungu ameruhusu dhambi wakati anao uwezo wote wa kuzuia ni kwa sababu tu hafahamu mpango mzuri wa Mungu kwetu, yaani wokovu. Kimsingi, baada tu ya mwanadamu wa kwanza kutenda dhambi, ilibidi atuache tuangamie, yaani tutupwe motoni kwa sababu mpango aliotaka tuuishi kwa hiyari tulichagua uasi. Hivi sasa tuko jatika jaribio la pili, tukishindwa na hili, tutatupwa hakika motoni. Mungu ameweka mpango wake ndiyo huo na ametupa kabisa kujua mema na mabaya, kinachotakiwa ni kumtafuta Mungu kwa gharama yoyote, siku ya mwisho haitajalisha kwamba labda hatukujua, la hasha. Kama zilivyo sheria za wanadamu duniani, kwamba kutokujua sheria si kinga ya msamaha, ndivyo Mungu alivyo. Tunasoma hiyo katika "Warumi 2:11-13 kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu. Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria. Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki." Unaona Mungu alivyoweka, haitajalisha kwamba wewe ulikuwa hujui, la msingi ni kumtafuta Mungu kwa bidii yote, mimi sikuuamini wokovu kabla, lakini baada ya kuona wengi wanaelezea habari za wokovu na mimi nikafanya bidii kuutafuta; nikaupata; nikabadilika.

Mungu yupo, na pia ametuagiza tusitende dhambi, mwenye kutuwezesha tusitende dhambi yupo [Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai] hivyo kuhoji mwaswali mengi; kwa nini, kwa nini, kwa nini, haitatusaidia, kama tulivyoona kwenye kitabu cha Warumi hapo juu.

Namalizia kwa kusema tena kwamba, Mungu ametuweka hapa duniani kwa sasa ili tufanye mapenzi yake na pia kufanya hivyo kupo ndani ya uwezo wetu, tukikataa yeye hana hasara sisi ndiyo tutakaopata hasara. Maswali ya namna yoyote hayatatusaidia, ametuweka ili tujaribiwe, Yesu mwenyewe ni kielelezo chetu, alijaribiwa sawasawa na sisi, lakini hakutenda dhambi kabisa "Waebrania 4: 14-16 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji." Wanazungumziwa watu wanaomchaji Mungu.
Shalom Aleichem!
 
Kwa mnatiki ya kawaida kutokuwepo kwa mwanga maana yake giza linakuwepo muda wote. Kwa hiyo ukiketa mwanga basi unaondoa giza. Lakini kusema guza ni kiumbe pia sikubaliani kwa sababu mianga tunaiona na kila kinachitoa mwanga huonekana lakini kile kitoacho mwanga kisipokuwepo au kisipotoa mwanga basi matokeo yake hubaki giza.
Giza sio kiumbe muda wote haihitaji kuumbwa bali kile kitiacho mwanga ili kusiwe na giza.
Giza maana yake "HAKUNA" kukiwa hakuna maana yake ni giza. Kabla ya kuzaliwa kwako ulikuwa giza, maana yake haukuwepo, hakuna kitu. Giza tunalozizungumzia hapa ni muhimu kufahamu kuwa ni zaidi ya weuzi tunaofikiria, giza ni hakua, ni sifuri. Nakubaliana na moja hapo juu kuwa giza siyo kiumbe. Kukiwa hakuna maana yake, nothing even a space, no tangible thing, ndiyo giza linalozungumzwa hapo katika biblia. Hivyo giza halikuumbwa, hakuna haiwezi kuwa imeumbwa, kabla hujakuwepo haukuwepo, ulikuwa hujaumbwa. Giza la weusi ni mahali palipo na space lakini hamwonani tu, lakini gizaanalolizungumzia Mungu maana yake hakuna kitu.
 
We jamaa nimwongo kwanini hukubali kujifunza ndugu? Njoo nikupe elimu
VITU SITA AMBAVYO SI VIUMBE VYA MUNGU.

View attachment 331270

Tarehe Mar 2016 niliandika makala juu mahusiano kati Kiza, Mungu, Kifo, Vita, Njaa, na Maradhi. Makala ile ilizua mjadala mkubwa facebook na whatsapp nilipoiweka, na moja jambo kubwa lilotuvuruga ni uwezo na mamlaka ya Mungu katika uumbaji, na hasahasa ile nadharia ya kuwa MUNGU ni muumbaji wa viumbe vyote ilitumiwa sana na watu katika kuikosoa makala yangu.

Awali ya yote nakubali bila kigegezi chochote kuwa Mungu ni muumbaji wa viumbe vyote na ya kwamba ni Mola wa viumbe hivyo. Nakubali kuwa ulimwengu haukuzuka tu wenyewe katika tukio la lisilo ratibiwa. Bali yupo injinia wa Ulimwengu huu ambaye si mwingine bali ni MUNGU.

Misaahafu ya dini za Ibrahim, yaan uislamu, uyaudi na ukristo yote kwa pamoja bila kukhitililafiana inasema ulimwengu na vilivyomo ndani yake havikuzuka kwa bahati mbaya bali vimeumbwa na Mungu.

Kuna viumbe hai kama wanyama na mimea, lakini pia kuna viumbe ambavyo havina uhai kama mawe na mchanga. Vyote hivi Muumbaji wake ni Mungu.

"Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Kwa hakika katika hayo ipo Ishara kwa Waumini. " Quran 29:44

"...Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!..." Quran 13:16

"Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba....." Zaburi 89:11-12

Hiyo quran 13:16 inatutanabaisha kuwa Mungu ameumba kila kitu, lakini tujiulize, kitu kilichoumbwa na Mungu kinaitwaje? Kwa vyovyote vile kinaitwa kiumbe. Kama ndivyo tunaweza kuwa sahihi zaidi kama tukisema kuwa Mungu ameumba viumbe vyote badala ya kusema kuwa Mungu ameumba kila kitu.

Twasema kuwa viumbe vyote vimeumbwa na Mungu, je vile ambavyo si viumbe tuna vizungumziaje? Naomba mjue Mungu ameumba viumbe vyote, lakini haimaanishi kuwa ameumba kila kitu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo Mungu hakuviumba aidha hakutaka kuviumba au ameshindwa kuviumba.

VITU VIKUU SITA AMBAVYO MUNGU HAKUVIUMBA.

1. MUNGU
Ukisoma misahafu yote mikuu miwili quran na biblia hakuna ushahidi hata mmoja unaonesha kuwa Mungu kaumba Mungu(namaanisha Mungu kujiumba).

Kubwa zaidi katika misahafu hiyo ambayo imeandikwa kwa matakwa yake MUNGU, inaonesha ukuu wa Mungu, uwezo wake, mamlaka yake, utukufu wake, usafi wake na kila aina ya sifa nzuri na tukufu, lakini hatuoni chanzo chake kikiandikwa humo na hatuoni mwisho wake ukiandikwa humo, zaidi ya vitabu hivyo kusema ufalme wa MUNGU na Nguvu zake hazina mwanzo wala mwisho.

"Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi" Ufunuo 1:8

"Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza. Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho...." Quran 28:69-70

Kwa aya hizi, na mafundisho mengine ya kinabii kama haya, yanathibitisha bila shaka kuwa ni kweli kuna mambo au vitu ambavyo Mungu hakuviumba na kwasababu hiyo vitu hivyo haviwezi kuitwa viumbe na ingawa viko. Kitu cha kwanza MUNGU, kipo na hakija umbwa.

Wanaosema kuwa MUNGU ameumba kila kitu waje hapa watuambie "MUNGU" kaumbwa na nani? Wakishindwa kututajia basi waishie kusema Mungu kaumba viumbe vyote lakini si vitu vyote.

2. KIZA
Ukisoma hiyo quran 28:69-70 na ukisoma vizuri ufunuo 1:8 utagundua mambo yote na habari zote kabla ya uwepo wa MUNGU hayajulikani na huenda anayajua Mungu mwenyewe, lakini kwetu sisi tunaona mambo hayo kwetu ni KIZA.

Kwa hivyo tunaweza kusema kabla ya Mungu hajaumba chochote alikuwako yeye na Kiza, Kiza ni mwanamke na Mungu ni mwanaume. Kwakuwa kwa kipindi hicho walikuwa wenyewe, na wanajuana wenyewe, jambo jepesi twaweza kusema hivi vitu ni ndugu. Ipo siku inshallah nitakuja kufafanua kwanini nasema Kiza mwanamke na Mungu mwanaume.

"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."
Mwanzo 1:1-4

Katika andika hilo la juu tunajifunza yafuatayo.

A. Mbingu na nchi zimeumbwa na Mungu. Maji, ardhi na vitu vya kufananayo ni sehemu ya mbingu ya nchi.

B. Mungu aliumba NURU lakini hakuumba KIZA, tunaambiwa tu Kiza kilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji lakini hatuambiwi Mungu aliumba Kiza.
Hiyo mwanzo 1:3 "Mungu akasema, iwe Nuru; ikawa Nuru"

Alijuaje kuwa Nuru imekuwa kama kabla ya Nuru hiyo kulikuwa hakuna Kiza? Je, mbona hatuoni maandiko yakionesha Mungu akisema iwe Kiza kisha kikawa Kiza?

C. Ukisoma mwanzo 1:2 tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi kisha Kiza alikaa juu ya uso wa vilindi vya maji, kwasababu hiyo, nikisema kuwa Kiza alikuwako kabla ya mbingu na nchi nitakosea? Kama alikuwako kabla ya mbigu na nchi, ama kabla ya ulimwengu, nikisema kuwa Kiza na Mungu waliishi wenyewe kabla ya ulimwengu pia nitakosea?

D. Baada ya Mungu kuumba Nuru, hapo ndipo alipofanikiwa, kumfungia KIZA, na athari za Kiza akaziita USIKU na athari za NURU akaziita MCHANA. Kwahivyo Mungu hakumuumba KIZA, ila Mungu kaumba Nuru, Mchana, na Usiku.

Kwahivyo kama tuko pamoja, utakubaliana na mimi kuwa KIZA ni moja ya kitu ambacho Mungu hakukiumba. KIZA si kiumbe, KIZA kimezuka tu kama alivyozuka Mungu mwenyewe. Tafauti kubwa kati ya MUNGU na KIZA ni kuwa Mungu kaumba na ni Mola wa viumbe vyote, lakini Kiza hakuumba kitu chochote kwa hivyo si MUUMBAJI.

Astronomy inatuambia kuwa ulimwemgu umeundwa na vitu vikuu vitatu, normal matter, dark matter na dark energy. Normal matter ndio hujumuisha zile atoms zilizo tumika kuumba Nyota,sayari, na vitu vingine.

Normal matter ni asilimia 5 tu ya ulimwengu wote, 25% ni dark energy na 70% dark matter. Hiyo dark energy na dark matter athari zake zinaonekana katika zenyewe hazionekane. Hii huenda ndio KIZA ambacho kimetajwa katika mwanzo 1:1

Astronomy pia yatuambia ulimwengu unatanuka kwa kasi, na ya kwamba unazidi kuongezeka kutokana ile motion iliyosababishwa na BING BANG, kutanuka kwake ina maanisha unazidi kumeza au ama kuingia katika sehemu mbele zaidi kutokea kule ulipo anzia(kipind cha dark age) Swali kule unapoelekea kuna nini kama si Kiza??

Astronomy pia yatuambia hakuna empty space, kama inavyo onekana, katika space waweza kuona ama kudhani hakuna maada yoyote, lakini kimsingi asilimia kubwa ya space ina dark energy na dark matter. Vitu hivi vinaashiria uwepo KIZA mbali na ulimwengu tunao ujua.

3. KIFO
Kwanza naomba tukumbuke wakati Mungu anafikiria kuumba ulimwengu tayari kulikuwako na KIZA. Ili Mungu awe kuumba ulimwengu ilikuwa lazima kwanza amuondoshe au amuue KIZA. Ili Kiza kiweze kufa shuruti pawe na "KIFO" Hata hivyo, kutokana na nguvu za Kiza, basi kikawa hakijakufa bali kilifungiwa.(Rejea mwanzo 1:3 Mungu akatenga giza na nuru)

Pili naomba mjue kuwa kiumbe hai cha kwanza kuumbwa na Mungu ni "NENO" kisha wakafuatia malaika wakubwa wanne(four Arc Angels) ambao ni Mikaeli, Raphaeli, Rucifer na Gabrieli. Hoja inakuja, Mungu alitumia kipimo gani kujua kwamba amefanikiwa kuumba kiumbe hai? Kwa vyovyote vile ili ajue kuwa amefanikiwa kuumba kiumbe hai ni lazima alinganishe uhai uliopo ndani ya kiumbe hai na mauti(KIFO). Kwa hivyo kilianza KIFO kabla ya UHAI, na bahati nzuri maandiko yanakubali kuwa Mungu kaumba uhai, lakini hayaoneshi kuwa Mungu kaumba KIFO.

Wachungaji wetu katika makanisa wanakataa katakata kuwa Mungu kaumba KIFO, wao wanasema KIFO kilisababishwa na shetani, bi maana shetani ndio kaumba KIFO. Huku ni kutokujua, lakini hakuna aliyeumba KIFO, KIFO sio kiumbe na alizuka tu kama alivyo zuka Mungu.

Kama nilivyosema ule muda Mungu anafikiria kuumba uhai, tayari kifo kilikuwako, na kwasababu hiyo, pia haijulikani kati ya Mungu na Kifo na mkubwa(kiumri).

Mungu aliumba uhai, na kwa kupitia huo uhai akaumba mwanadamu, lengo lake lilikuwa mwanadamu aishi milele, lakini kifo kikawa kikwazo katika lengo hili.

Sivyo tu, kwakuwa siku zote KIZA anataka atoke kifungoni, hivyo kila siku anapambana na Mungu kwa lengo la kutaka kumuua, na wakati huohuo Mungu naye anataka kumuua KIZA, mshindi wa pambano hili lazima amtumie "KIFO" na hapa ndipo tunapoona nafasi ya KIFO katika mahusiano ya NURU na KIZA.

Lakini Mungu anasema atakuja kumshinda KIZA na KIFO, na pindi atakapo shinda hakuna roho au mwili utakao kufa.

"na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. " Ufunuo 1:18

4. VITA na NJAA
KIZA baada ya kugundua Mungu ameumba malaika wakubwa wanne, KIZA alichukia na hapo yakazuka mapambano kati ya MUNGU na KIZA. Kwa mapambano hayo ndipo ilipozuka "VITA" mungu alichofanikiwa ni kumfungia KIZA, na funguo zake akakabidhiwa Rucifer. Mark of Darkness ndio Funguo na sehemu alofungiwa KIZA, chapa hii baadae iliitwa mark of cain.

Mnyama wa kwanza kuumbwa na Mungu kabla hata ya wanadamu ni Levithans, hawa ndio ile mijusi mikubwa na Magodizilla. hawa walikuwa na "NJAA" sana kiasi walane wenyewe kwa wenyewe, Hapa Mungu kwa kutumia jeshi lake la malaika waliwaondoa dunia na kuwafungua Purgatory. Hapa pia VITA alihitajika kufanikisha hili.

Tembo na vufaru wanapungua kwa kuuliwa na binadamu, hivi Magodizilla na Levithans waliuliwa na nani? Ikiwa wao walikuwako miaka mingi kabla ya wanadamu? Jibu jepesi ni upanga wa Malaika Mikael na jeshi lakd.

Wakati hayo yakitokea, Darkness akaigeuza ile mark kuwa laana, na laana ile ikasababisha hali ya uasi kwa mtunza funguo. Wakati Mungu anamuumba mwanadamu, na malaika kuambiwa wamsujudie, Rucifer akiwa kesha athiriwa na laana ya funguo akagoma kumsujidia adamu.

Kwa mara nyingine "VITA" ilihitajika katika kumdhibiti Rucifer na kundi lake.

6 MARADHI
mungu hakuumba maradhi, na wala si lengo mungu mwanadamu aumwe na kuteseka kwa maradhi. Ila pale mwanadamu alipoumbwa na afya bora kabisa, na maradhi yakazuka hapo hapo. Baada ya Mungu kuja kumshinda KIFO, pia atakuja kuyashinda MARADHI, na hayo yakitokea katika maisha Paradiso hakutakuwa na KIFO wala MARADHI.

MWISHO.
makala hii haina tafauti na ya juzi, ila leo baadhi ya nukta nimemua kuziongelea kwa undani zaidi ili iweze kujibu maswali na hoja zilizo jitokeza katika makala ya msingi. Hata hivyo najua siwezi kumaliza kila kitu hapa, ila mengine tutajifunza katika mjadala!

Njano5
0622845394

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom