Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 362
- 712
Miaka 7 iliyopita nipitia katika changamoto kubwa ya mahusiano yangu na Mungu.
Katika kipindi hicho chote Mungu alikuwa mwaminifu katika maisha yangu , mambo mengi ambayo hata sikuyaomba Mungu alinifanyia kwa upendo
Maisha yalikuwa mazuri katika upande wa familia, watoto, uchumi nk kwa kweli Mungu alikuwa ni mwema sana na hata leo nasema tena Mungu ni mwema.
Katika miaka hiyo yote jambo 1 ambalo nilikuwa namwomba Mungu hakuweza kunijibu, ombi hilo moja lilikuwa la muhimu sana kwangu kuliko maombi yote ambayo nimemwomba Mungu anifanyie
Ombi hilo lilianza mwaka 2019 nilianza kuomba Mungu juu ya jambo hilo, mwanzoni ili kuwa ni sehemu ya maombi yangu kwa Mungu.
Mwaka 2020 niliendelea kupeleka ombi kwa Mungu juu ya hitaji langu kwake kama kawaida pasipo kuchoka
Mwaka 2021 maombi yaliendelea na mkakati wa kufanya maombi ulibadilika
Mwaka 2022 maombi yalibadilika yakawa kilio, badala ya kuomba nikawa namlilia Mungu
Mwaka 2023 jambo lile likawa kama deni kwa Mungu, nikaanza kusoma tena biblia namkumbusha Mungu juu ya shuhuda mbalimbali alizofanya juu ya watumishi wake , maombi ya mifungo yakaanza na kwa kweli maombi yalikuwa mengi
Mwaka 2024 nikaanza kuwasilikisha na baadhi ya marafiki zangu ili tuweze kuomba kwa pamoja juu ya jambo langu,maombi ya kufunga tatu kavu na mifungo mirefu kuanza
Mwaka 2024 ndio mwaka ambao maombi ya siku 40 nilianza kuomba kwa ajili ya Mungu kunikubuka juu ya ombi langu
Mwaka 2025 nguvu za maombi zilipungua imani kwa Mungu ilipata pancha kidogo kidogo nikaona kama Mungu amenisahau lakini sikujua yale ambao wengine wanaomba usiku kucha Mungu alinipa hata bila kuomba kwa kweli sikuona wema wa Mungu katika mengi zaidi ya lile moja ambalo sikupata
Mwaka 2026 Mungu alinifuta machozi akanijaria ombi langu la miaka 7, kwa kweli siku majibu yalipopatikana nilifurahi sana lakini sio sana hile ambayo labda nikapata mwaka 1 au 2 iliyopita, nilipopata nikajikuta sehemu kubwa ya uhusiano wangu na Mungu umepungua kiu yangu ikawa sio tena kile nilichopata kiu yangu ikawa juu ya uhusiano wangu na Mungu
Mara nyingi tunapokuwa tuna uhitaji tunapokuwa tunaomba kwa ajili ya uitaji wetu na inafika mahali katika kuomba badala ya kujenga uhusiano wetu na Mungu tunajenga uhusiano wetu na vitu ambavyo Mungu anatupa
Ibrahimu alipopewa Isaka akasahau uhusiano wake na Mungu, Mungu akamwomba Isaka, sio kwamba Mungu alimtaka isaka hapana Mungu alitaka Moyo wake Ibrahimu
Ni kweli tunamwitaji Mungu sana kujibu maombi yetu, lakini katika kumsubiri Mungu tusije kutenda dhambi.
Kuna mtu amasema kama Mungu hajajibu maombi yangu basi hakuna Mungu, ile Mungu kutokujibu ombi lako hakuondoi ukuu wake wa Uungu
Kumbuka ukiona maombi yako yanachelewa ujue pia ni mpango wa Mungu, Mungu hajawai luchelewa wala kuwai siku zote yuko ontime
Mungu anajibu maombi, ila ni kwa wakati wake sio kwa wakati wako sio kwa wakati wetu Mungu ni Mungu tu na hatabakia kuwa Mungu.