Secret Star
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,861
- 2,100
Kukamilika kwa kujua nyuma au kujua Future ni jambo ambalo wanadamu sisi hatuna, nitakuambia kwanini hatuna, ila wale watu wanne walioumbwa na Mungu wao Biblia inaeleza wazi kuwa waliumbwa kwa sura na kwa mfano wa Mungu, yaani walikuwa wanaweza kila kitu, si kujua nyuma au kujua Future! Hao walikuwa wamekamilika kila sekta..Utasemaje kumuumba mwanadamu ambaye hajui mabaya ni kumuumba mtu asiyekamilika wakati mungu ndiye anayeamua kukamilika ni nini?
Sasa hivi wanadamu hatuwezi kurudi nyuma katika muda. Utasema hatujakamilika kwa sababu hatuwezi kurudi nyuma katika muda?
Uzao wa sisi tunaochat humu kwa sasa Kwa Biblia ulianzia kwenye mwanzo 2:7, ambapo pale unaona Baada ya Mungu kuwa ameshawaumba Binadamu fulani kwenye Mwanzo 1,26 anamuumba binadamu mwingine kwa udongo, pia mtu huyo anapewa kazi ya kutunza Bustani, na si kutawala kama wale wengine kule, pia mtu huyu anakuwa hajui mema na mabaya ni yapi, yaani kwa mfano mwepesi mtu huyo ambaye aliumbwa alikuwa hana tofauti na wanyama kama mbuzi au nyani unaowaona leo, Ila tunafunzwa kuwa shetani alikuja kuharibu Dunia na hivyo kuwapa siri wale waliopewa kazi ya kutunza bustani, ambapo shetani akiwafungua macho kwa kuwapa matunda ya ule, mti wakala na kufunguka hivyo binadamu hawa wakawa wameingilia mpango wa Mungu sababu kwenye mpango maalum wao ilikuwa wawe kama punda, tu au kuku.. kwa ajili ya kuufanya utawala wa wale binadamu wanne ufanyike, yaani utawale, hivyo mzee kiasili sisi haikuwa tuwe tuna maarifa kama haya! Ilikuwa tuwe sawa na mifugo tu kwa hao watawala wanne waliokuwa wamepewa mamlaka ya kutawala ulimwengu wote; sisi tukajichomeka kwenye mpango ambao kabla Mungu hakuupanga....