OK, so mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana. Mpaka hapo tayari una tatizo kubwa sana la kutatua.
Maana kama mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, na ulimwengu huu mabaya yanawezekana, ina maana mungu hakuumba ulimwengu huu?
Sasa imekuwaje mabaya yanawezekana? Ina maana kuna kitu kina uwezo kumpita mungu kilichofanya ulimwengu uwezekane kuwa na mabaya wakati mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?
Mwanadamu amewezaje kufanya mabaya katika ulimwengu ambao mungu hakuumba uwezekano wa mabaya kufanyika?
Lazima uelewe kwamba, ili binadamu afanye baya, inabidi uwezekano wa baya kufanyika uwepo.
Binadamu hawezi kufanya baya katika ulimwengu ambao uwezekano wa baya kufanyika haupo.
Kama vile ambavyo binadamu hawezi kurudi nyuma katika muda katika ulimwengu ambao uwezo wa binadamu kurudi nyuma katika muda haupo.
Sasa binadamu kawezaje kufanya mabaya katika ulimwengu ambao mungu hakuumba uwezekano wa mabaya kufanyika?
Kama mungu hakuumba binadamu kufikiri mema tu, kamuumba binadamu kuweza kufikiri na kufanya mabaya, utasemaje mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana? Unajichanganya.
Unapoongelea "akili ya kujua mema na mabaya" tayari ushaongelea ulimwengu ambao mabaya yapo. Mimi ninachouliza ni tofauti. Nauliza kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana in the first place? Katika ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, hakuna suala la kujua mema na mabaya kwa sababu mabaya hayapo. Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?
Alishindwa kuumba ulimwengu ambao una mazuri tu hauna mabaya na akampa mwanadamu uhuru wa kuchagua mazuri yapi afanye?
Mungu alishindwa kumpa mwanadamu nguvu maarifa na utashi katika ulimwengu ambao una mazuri tu na hauna mabaya?
Na kama kweli mungu anapenda mwanadamu awe na maarifa, kwa nini hakumpa mwanadamu maarifa awe kama yeye mungu?
Mungu kwa kuumba binadamu katika ulimwengu ambao mabaya yanawezekana tu na kutompa mwanadamu uwezo wa kuwa mungu tayari kashamzuia mwanadamu kuishi kwa wema 100 per cent.
Utasemaje kwamba vitu vibaya ni matokeo ya mwanadamu wakati mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kufanyika kabla mwanadamu hajaumbwa? Uwezekano wa ubaya kufanyika umekuwapo tangu mwanadamu hajaumbwa, mwanadamu hajaumbwa na uwezo kama wa mungu wa kuepuka mabaya, mwanadamu akifanya mabaya kwa sababu ulimwengu unaruhusu mabaya kufanyika kabla yeye hajaumbwa na kwa sababu yeye kaumbwa na mapungufu yanayomfanya aweze kufanya mabaya, utasemaje mabaya ni matokeo ya wanadamu wenyewe?
Ni kama umpe mtoto mchanga pikipiki halafu umtake aiendeshe resi barabarani wakati unajua kwamba hana uwezo huo, akianguka na kuumia utasema ni matokeo yake yeye mwenyewe au mipango yako?
Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao ianwezekana kwa mtu kuwa na tamaa ya kumtongoza mke wa fulani wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna tamaa ya mtu kumtongoza mke wa Fulani?
Hujajibu hili swali.
Wapi unalipata hili?
Kwa nini mungu kaumba uwezekano wa mtu kuwa na tamaa ya kumtongoza mke wa Fulani wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna tamaa ya mtu kumtongoza mke wa Fulani?
Unaweza kujibu hili swali?
Uthibitisho gani? Unaweza kuutaja? Usilazimishe mambo tu.
Hujathibitisha mungu yupo. Una otea otea tu kwa "pengine".
Unaweza kuthibitisha mungu yupo?