Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
VITU SITA AMBAVYO SI VIUMBE VYA MUNGU.
Tarehe Mar 2016 niliandika makala juu mahusiano kati Kiza, Mungu, Kifo, Vita, Njaa, na Maradhi. Makala ile ilizua mjadala mkubwa facebook na whatsapp nilipoiweka, na moja jambo kubwa lilotuvuruga ni uwezo na mamlaka ya Mungu katika uumbaji, na hasahasa ile nadharia ya kuwa MUNGU ni muumbaji wa viumbe vyote ilitumiwa sana na watu katika kuikosoa makala yangu.
Awali ya yote nakubali bila kigegezi chochote kuwa Mungu ni muumbaji wa viumbe vyote na ya kwamba ni Mola wa viumbe hivyo. Nakubali kuwa ulimwengu haukuzuka tu wenyewe katika tukio la lisilo ratibiwa. Bali yupo injinia wa Ulimwengu huu ambaye si mwingine bali ni MUNGU.
Misaahafu ya dini za Ibrahim, yaan uislamu, uyaudi na ukristo yote kwa pamoja bila kukhitililafiana inasema ulimwengu na vilivyomo ndani yake havikuzuka kwa bahati mbaya bali vimeumbwa na Mungu.
Kuna viumbe hai kama wanyama na mimea, lakini pia kuna viumbe ambavyo havina uhai kama mawe na mchanga. Vyote hivi Muumbaji wake ni Mungu.
"Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Kwa hakika katika hayo ipo Ishara kwa Waumini. " Quran 29:44
"...Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!..." Quran 13:16
"Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba....." Zaburi 89:11-12
Hiyo quran 13:16 inatutanabaisha kuwa Mungu ameumba kila kitu, lakini tujiulize, kitu kilichoumbwa na Mungu kinaitwaje? Kwa vyovyote vile kinaitwa kiumbe. Kama ndivyo tunaweza kuwa sahihi zaidi kama tukisema kuwa Mungu ameumba viumbe vyote badala ya kusema kuwa Mungu ameumba kila kitu.
Twasema kuwa viumbe vyote vimeumbwa na Mungu, je vile ambavyo si viumbe tuna vizungumziaje? Naomba mjue Mungu ameumba viumbe vyote, lakini haimaanishi kuwa ameumba kila kitu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo Mungu hakuviumba aidha hakutaka kuviumba au ameshindwa kuviumba.
VITU VIKUU SITA AMBAVYO MUNGU HAKUVIUMBA.
1. MUNGU
Ukisoma misahafu yote mikuu miwili quran na biblia hakuna ushahidi hata mmoja unaonesha kuwa Mungu kaumba Mungu(namaanisha Mungu kujiumba).
Kubwa zaidi katika misahafu hiyo ambayo imeandikwa kwa matakwa yake MUNGU, inaonesha ukuu wa Mungu, uwezo wake, mamlaka yake, utukufu wake, usafi wake na kila aina ya sifa nzuri na tukufu, lakini hatuoni chanzo chake kikiandikwa humo na hatuoni mwisho wake ukiandikwa humo, zaidi ya vitabu hivyo kusema ufalme wa MUNGU na Nguvu zake hazina mwanzo wala mwisho.
"Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi" Ufunuo 1:8
"Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza. Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho...." Quran 28:69-70
Kwa aya hizi, na mafundisho mengine ya kinabii kama haya, yanathibitisha bila shaka kuwa ni kweli kuna mambo au vitu ambavyo Mungu hakuviumba na kwasababu hiyo vitu hivyo haviwezi kuitwa viumbe na ingawa viko. Kitu cha kwanza MUNGU, kipo na hakija umbwa.
Wanaosema kuwa MUNGU ameumba kila kitu waje hapa watuambie "MUNGU" kaumbwa na nani? Wakishindwa kututajia basi waishie kusema Mungu kaumba viumbe vyote lakini si vitu vyote.
2. KIZA
Ukisoma hiyo quran 28:69-70 na ukisoma vizuri ufunuo 1:8 utagundua mambo yote na habari zote kabla ya uwepo wa MUNGU hayajulikani na huenda anayajua Mungu mwenyewe, lakini kwetu sisi tunaona mambo hayo kwetu ni KIZA.
Kwa hivyo tunaweza kusema kabla ya Mungu hajaumba chochote alikuwako yeye na Kiza, Kiza ni mwanamke na Mungu ni mwanaume. Kwakuwa kwa kipindi hicho walikuwa wenyewe, na wanajuana wenyewe, jambo jepesi twaweza kusema hivi vitu ni ndugu. Ipo siku inshallah nitakuja kufafanua kwanini nasema Kiza mwanamke na Mungu mwanaume.
"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."
Mwanzo 1:1-4
Katika andika hilo la juu tunajifunza yafuatayo.
A. Mbingu na nchi zimeumbwa na Mungu. Maji, ardhi na vitu vya kufananayo ni sehemu ya mbingu ya nchi.
B. Mungu aliumba NURU lakini hakuumba KIZA, tunaambiwa tu Kiza kilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji lakini hatuambiwi Mungu aliumba Kiza.
Hiyo mwanzo 1:3 "Mungu akasema, iwe Nuru; ikawa Nuru"
Alijuaje kuwa Nuru imekuwa kama kabla ya Nuru hiyo kulikuwa hakuna Kiza? Je, mbona hatuoni maandiko yakionesha Mungu akisema iwe Kiza kisha kikawa Kiza?
C. Ukisoma mwanzo 1:2 tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi kisha Kiza alikaa juu ya uso wa vilindi vya maji, kwasababu hiyo, nikisema kuwa Kiza alikuwako kabla ya mbingu na nchi nitakosea? Kama alikuwako kabla ya mbigu na nchi, ama kabla ya ulimwengu, nikisema kuwa Kiza na Mungu waliishi wenyewe kabla ya ulimwengu pia nitakosea?
D. Baada ya Mungu kuumba Nuru, hapo ndipo alipofanikiwa, kumfungia KIZA, na athari za Kiza akaziita USIKU na athari za NURU akaziita MCHANA. Kwahivyo Mungu hakumuumba KIZA, ila Mungu kaumba Nuru, Mchana, na Usiku.
Kwahivyo kama tuko pamoja, utakubaliana na mimi kuwa KIZA ni moja ya kitu ambacho Mungu hakukiumba. KIZA si kiumbe, KIZA kimezuka tu kama alivyozuka Mungu mwenyewe. Tafauti kubwa kati ya MUNGU na KIZA ni kuwa Mungu kaumba na ni Mola wa viumbe vyote, lakini Kiza hakuumba kitu chochote kwa hivyo si MUUMBAJI.
Astronomy inatuambia kuwa ulimwemgu umeundwa na vitu vikuu vitatu, normal matter, dark matter na dark energy. Normal matter ndio hujumuisha zile atoms zilizo tumika kuumba Nyota,sayari, na vitu vingine.
Normal matter ni asilimia 5 tu ya ulimwengu wote, 25% ni dark energy na 70% dark matter. Hiyo dark energy na dark matter athari zake zinaonekana katika zenyewe hazionekane. Hii huenda ndio KIZA ambacho kimetajwa katika mwanzo 1:1
Astronomy pia yatuambia ulimwengu unatanuka kwa kasi, na ya kwamba unazidi kuongezeka kutokana ile motion iliyosababishwa na BING BANG, kutanuka kwake ina maanisha unazidi kumeza au ama kuingia katika sehemu mbele zaidi kutokea kule ulipo anzia(kipind cha dark age) Swali kule unapoelekea kuna nini kama si Kiza??
Astronomy pia yatuambia hakuna empty space, kama inavyo onekana, katika space waweza kuona ama kudhani hakuna maada yoyote, lakini kimsingi asilimia kubwa ya space ina dark energy na dark matter. Vitu hivi vinaashiria uwepo KIZA mbali na ulimwengu tunao ujua.
3. KIFO
Kwanza naomba tukumbuke wakati Mungu anafikiria kuumba ulimwengu tayari kulikuwako na KIZA. Ili Mungu awe kuumba ulimwengu ilikuwa lazima kwanza amuondoshe au amuue KIZA. Ili Kiza kiweze kufa shuruti pawe na "KIFO" Hata hivyo, kutokana na nguvu za Kiza, basi kikawa hakijakufa bali kilifungiwa.(Rejea mwanzo 1:3 Mungu akatenga giza na nuru)
Pili naomba mjue kuwa kiumbe hai cha kwanza kuumbwa na Mungu ni "NENO" kisha wakafuatia malaika wakubwa wanne(four Arc Angels) ambao ni Mikaeli, Raphaeli, Rucifer na Gabrieli. Hoja inakuja, Mungu alitumia kipimo gani kujua kwamba amefanikiwa kuumba kiumbe hai? Kwa vyovyote vile ili ajue kuwa amefanikiwa kuumba kiumbe hai ni lazima alinganishe uhai uliopo ndani ya kiumbe hai na mauti(KIFO). Kwa hivyo kilianza KIFO kabla ya UHAI, na bahati nzuri maandiko yanakubali kuwa Mungu kaumba uhai, lakini hayaoneshi kuwa Mungu kaumba KIFO.
Wachungaji wetu katika makanisa wanakataa katakata kuwa Mungu kaumba KIFO, wao wanasema KIFO kilisababishwa na shetani, bi maana shetani ndio kaumba KIFO. Huku ni kutokujua, lakini hakuna aliyeumba KIFO, KIFO sio kiumbe na alizuka tu kama alivyo zuka Mungu.
Kama nilivyosema ule muda Mungu anafikiria kuumba uhai, tayari kifo kilikuwako, na kwasababu hiyo, pia haijulikani kati ya Mungu na Kifo na mkubwa(kiumri).
Mungu aliumba uhai, na kwa kupitia huo uhai akaumba mwanadamu, lengo lake lilikuwa mwanadamu aishi milele, lakini kifo kikawa kikwazo katika lengo hili.
Sivyo tu, kwakuwa siku zote KIZA anataka atoke kifungoni, hivyo kila siku anapambana na Mungu kwa lengo la kutaka kumuua, na wakati huohuo Mungu naye anataka kumuua KIZA, mshindi wa pambano hili lazima amtumie "KIFO" na hapa ndipo tunapoona nafasi ya KIFO katika mahusiano ya NURU na KIZA.
Lakini Mungu anasema atakuja kumshinda KIZA na KIFO, na pindi atakapo shinda hakuna roho au mwili utakao kufa.
"na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. " Ufunuo 1:18
4. VITA na NJAA
KIZA baada ya kugundua Mungu ameumba malaika wakubwa wanne, KIZA alichukia na hapo yakazuka mapambano kati ya MUNGU na KIZA. Kwa mapambano hayo ndipo ilipozuka "VITA" mungu alichofanikiwa ni kumfungia KIZA, na funguo zake akakabidhiwa Rucifer. Mark of Darkness ndio Funguo na sehemu alofungiwa KIZA, chapa hii baadae iliitwa mark of cain.
Mnyama wa kwanza kuumbwa na Mungu kabla hata ya wanadamu ni Levithans, hawa ndio ile mijusi mikubwa na Magodizilla. hawa walikuwa na "NJAA" sana kiasi walane wenyewe kwa wenyewe, Hapa Mungu kwa kutumia jeshi lake la malaika waliwaondoa dunia na kuwafungua Purgatory. Hapa pia VITA alihitajika kufanikisha hili.
Tembo na vufaru wanapungua kwa kuuliwa na binadamu, hivi Magodizilla na Levithans waliuliwa na nani? Ikiwa wao walikuwako miaka mingi kabla ya wanadamu? Jibu jepesi ni upanga wa Malaika Mikael na jeshi lakd.
Wakati hayo yakitokea, Darkness akaigeuza ile mark kuwa laana, na laana ile ikasababisha hali ya uasi kwa mtunza funguo. Wakati Mungu anamuumba mwanadamu, na malaika kuambiwa wamsujudie, Rucifer akiwa kesha athiriwa na laana ya funguo akagoma kumsujidia adamu.
Kwa mara nyingine "VITA" ilihitajika katika kumdhibiti Rucifer na kundi lake.
6 MARADHI
Mungu hakuumba maradhi, na wala si lengo mungu mwanadamu aumwe na kuteseka kwa maradhi. Ila pale mwanadamu alipoumbwa na afya bora kabisa, na maradhi yakazuka hapo hapo. Baada ya Mungu kuja kumshinda KIFO, pia atakuja kuyashinda MARADHI, na hayo yakitokea katika maisha Paradiso hakutakuwa na KIFO wala MARADHI.
MWISHO.
Makala hii haina tafauti na ya juzi, ila leo baadhi ya nukta nimemua kuziongelea kwa undani zaidi ili iweze kujibu maswali na hoja zilizo jitokeza katika makala ya msingi. Hata hivyo najua siwezi kumaliza kila kitu hapa, ila mengine tutajifunza katika mjadala!
Njano5
0622845394