Zion Daughter
JF-Expert Member
- Jul 9, 2009
- 8,921
- 4,236
Jamani si nasikia vilipigwa marufuku hivi vitabu? eti vinafundisha ujambazi?sasa Kaizer unavitakia vya nini?wakuu naombeni msaada wenu kama kuna anayejua ninakoweza kupata hivi vitabu ya Elvis Musiba, vikiwa na stellingi Willy Gamba.
Vitabu hivyo ni kama vile:
1.Kikosi cha Kisasi
2.Kufa na Kupona
3.Hofu.
4.Njama
5.Uchu
na vinginevyo. nimevisoma baadhi zamani lakini sasa hivi sina nakala tena ningependa kujua ninakoweza kuvipata.
shukrani!
...nakumbuka kipande hiki kama sikosei kwenye kufa na kupona 'nenda rudi salama umefanikiwa, kwenda na mwoneshaji wa mavazi, leo usiku toka uaduini tunamofikiri' acha kabisa novo zile.
vipi kuhusu lile kipande kwenye njama wakati yupo pale bintuman hotel jijini freetown sierra leone akiwa na mrembo veronica na kijana sharrif kisha maselina akamtumia ujumbe uliosema mama mgonjwa sana unatakiwa urudi haraka kisha willy akajua kwa ujumbe huo basi tena likizo ishaharibika bila kujua kuwa veronica na sharrif nao walikuwa ndani ya kamati ya ukombozi
acha kabisaaaaaaaa
hapo nakuunga mguuu mkuuu Hussein Chuwa anafata nyayo za akina Musiba na Kiango nimekisoma hicho kitabu kizuri sana , jamaniiiii shigongo anabore na hadithi zake zinazofanana na picha za kinigeria na kisha kujirudiarudia nilikuwa mpenzi wa hadithi zake lakini baada ya kusoma nne tu nikajua jamaaa amefulia huyuuuuu mpaka leo sijagusa hata moja maana naona uzushi tu bora niangalie 24hrs kuliko kuangalia tafsiri za movie za kinigeria
Hiki cha Hussein ni kile chenye msichana mwenye jina gumu sijui alikuwa akiitwa Tiganini sijui ? alikuwa anafanya kazi kwenye makumbusho sijui au siyo huyo? Wenzie waliuliwa walipokwenda field na yeye peke yake akabakia akiwa na mkanda unaoonyesha mauaji yalivyofanyika mle msituni? Kama ni hicho nakubaliana nanyi ni kizuri nilifanikiwa kukisoma kwa siku mbili kwani utamu wake haukuruhusu nikiweke chini kivivu!
Hivi wasanii weyu kwa nini wasiigize movies za stories kutoka kwenye hivi vitabu!
Maana story wanazo ekti ni mapenzi tuu hazina vichwa wala miguu.
Mimi wakuu natafuta vitabu vya Juma na Roza kwa ajili ya mwanangu, nilivipenda sana enzi hizo! naweza vipata wapi?
Mkuu X-P,Kuna waandishi wengine mahiri sana ambao watu wengi hawawafahamu, mfano mmoja wapo ni Mwandishi ajulikanae kwa jina la Muhamed Said Abdulla a.k.a bwana Msa (Marehemu), ana vitabu kama vile Kosa la Bwana MSA, Siri ya Sifuri, Mzimu wa Watu wa Kale, Kisiwa cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Mke Mmoja Waume Watatu na Mwana wa Yungi Hulewa. Vile vile kuna huyu ajuliukanae kwa jina la Said Ahmed Mohamed na vitabu vyake ni Kiza katika Nuru, Utengano, Asali Chungu... Bila kumsahau Mzee Shafi Adam Shafi. Na Vitabu vyake vijulikanavyo kwa majina haya: Kasri Ya Mwinyi Fuad, Kuli, Haini na Vuta N' Kuvute.
Mi nimesoma vitabu vyote vya James Hadley Chase na Erle stanley Gardner. Nimesoma pia vitabu vya Musiba. Kwa kifupi sidhani kam vitabu vya Chase vinafanana hata kidogo na vya Musiba..Sidhani kama anaiga hata kidogo, ila kuna jambo muhimu moja. Ukiwa unasoma vitabu vingi unajikuta unakuwa mkosoaji sana wa vitabu na iyo ndo njia inaweza kukufanya k......vutia msomaji
Nadhani Nick Carter alikuwa anawalenga Teenagers kwenye riwaya zake, sawa na mtunzi huyu wa Kimarekani Stephenie Meyer na vitabu vyake vya ki-vampire. Musiba ukimfananisha na watunzi aina ya kina Nick Carter utakuwa umemshushia sana hadhi yake.... Musiba yupo juu zaidi ya Nick Carter... Tatizo yupo Tanzania tu basi.Mkuu nakubaliana na wewe kwamba vitabu vya Chase hafifanani na vya Musiba.
Lakini je uliwahi kusoma vitabu vya Nick carter? Vitabu vya Musiba havina tofauti na vitabu vingi vya Carter ..... hapo alikuwa anabadilisha majina ya kizungu anaweka ya kibantu ..... !! Scene zote .. kila kitu. katika kitabu labda alikuwa anabadilisha na kuongeza vijisehemu vidogo mno ambavyo kwa uliyesoma hizo Carters unaweza ukajua kabisa ni kitu gani kitatokea kwenye chapter inayofuata.
Kwa hiyo statement yako hapo juu Mkuu sio sahihi..
Hapo nakubaliana nawe asilimia 100, ni kweli Musiba alikua aniga kutoka kwa carter. Ila unapokua unasoma vitabu vingi ni rahisi kuwa na mawazo yako na kuunganisha na hadithi ulizowai soma, kumbuka hakuna jambo lipya duniani.Mkuu nakubaliana na wewe kwamba vitabu vya Chase hafifanani na vya Musiba.
Lakini je uliwahi kusoma vitabu vya Nick carter? Vitabu vya Musiba havina tofauti na vitabu vingi vya Carter ..... hapo alikuwa anabadilisha majina ya kizungu anaweka ya kibantu ..... !! Scene zote .. kila kitu. katika kitabu labda alikuwa anabadilisha na kuongeza vijisehemu vidogo mno ambavyo kwa uliyesoma hizo Carters unaweza ukajua kabisa ni kitu gani kitatokea kwenye chapter inayofuata.
Kwa hiyo statement yako hapo juu Mkuu sio sahihi..
Mkuu unaweza kutoa mfano wa riwaya mojawapo inayo fafana na ya Nick Carter!?Hapo nakubaliana nawe asilimia 100, ni kweli Musiba alikua aniga kutoka kwa carter. Ila unapokua unasoma vitabu vingi ni rahisi kuwa na mawazo yako na kuunganisha na hadithi ulizowai soma, kumbuka hakuna jambo lipya duniani.
hivi vitabu vinauzwa na wamachinga wewe ukiwaona kule mabarabarani waulize utabahatika. mi lishakutana na mmjo sinza nikammuliza akaniambia vipo na alikuwa ananipigia simu alipovipata.wakuu naombeni msaada wenu kama kuna anayejua ninakoweza kupata hivi vitabu ya Elvis Musiba, vikiwa na stellingi Willy Gamba.
Vitabu hivyo ni kama vile:
1.Kikosi cha Kisasi
2.Kufa na Kupona
3.Hofu.
4.Njama
5.Uchu
na vinginevyo. nimevisoma baadhi zamani lakini sasa hivi sina nakala tena ningependa kujua ninakoweza kuvipata.
shukrani!