Kisa kingine kilinigusa nikiwa O level this time pale Rugambwa secondary ni kuchota maji kwenye kijito kipo kwenye mawe.Sasa hapo mkiwa zamu ya kuchota maji ya jikoni. Kaka Hansi kule jikoni anasema maji bado ongezeni tena.
Ukizingatia ziwa Victoria lipo Bukoba,ila shule maji ya tabu.
Pia vyoo vilikuwa vinajaa inabidi kuzibua.
Sitasahau kuna vyoo tulikuwa tunaviita Ihungo vilikwa vichafu.
Nikiwa O level pia nikahamia Korogwe girls huko napo nikakuta shida ya maji,kubeba ndoo kwenda kuteka maji idara ya maji.
Kuchunga ng'ombe,mchaka mchaka asubuhi. Acha kabisa.
Shamba sasa mwalimu Manento na fimbo zake,Cheka nikuue yule mwalimu anakuchekea huku anakuchapa.
Infwact shule za serikali boarding zilitupa jambajamba.
Niliapa sitakubali mwanangu asome shule ya boarding ya serikali wala ya private.
Ila tulipata ujasiri wa kupiga shule.
Inshallah Mungu akatuvusha.