Ma-TO walipofunikwa na Sylivester Mwageni (True mathematician)

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
Kuna matukio fulani hutokea kwa namna pekee ya kushangaza na mengine huwa ya kufurahisaha zaidi hasa katika jukwaa letu hili pendwa la ELIMU.

Napenda sana kuhudhuria jukwaa hili na ' ITAPENDEZA ' nikiitwa ' MASTER WA JUKWAA LA ELIMU '

Sasa leo nawakumbushia tu historia ya T.O Maarufu zaidi "GWAMAKA NGOBELO" wa MZUMBE SPECIAL SCHOOL na "JAMALI JUMA aka BABU wa FEZA BOYS au AZANIA au ukipenda ITA Azaboys " walipokutana kwa wakati tofauti na KISIKI katika somo la PURE MATHEMATICS aitwaye 'SILVESTER'

Tukubali tukatae ila kuna watu katika ULIMWENGU huu wamebarikiwa sana kuwa na akili,pamoja na hivyo akili za VICHWA hivi viwili kwa nyakati TOFAUTI walijikuta wakimpigia SALUTE Silvester wa KIBAHA kwa kusema 'Kwa Mathematics sikuwezi'.

Bila shaka humu JamiiForums wapo watu waliosoma KIBAHA au waliofanya EZERB form 6 mwaka 2012 na wakasikia JINA Silvester hivyo wanaweza kuthibitisha hiki ninachokisema hapa.

STORY INAANZIA MWAKA 2009

Tuanzie Azania High School mwaka 2009 alitokea mwanafunzi mmoja aliyeteka sana attention kielimu katika Jiji la Dar es Salaam kwa wakati huo akijulikana kama JAMALI JUMA.Wengi tuliosoma DSM miaka hiyo sio rahisi kulikumbuka JINA hilo la JAMALI JUMA ila tutamkumbuka mwanafunzi huyo huyo kwa jina la BABU.

Jamaa alifanya maajabu katika mtihani wa TAHOSA Form 4 baada ya kunyuka "A" 7 na kupata div 1.7 na kuwa "BEST STUDENT" wa DSM katika mtihani huo huku akiwaacha mbali VIPANGA wa FEDHA wakibaki wanashangaa kuwa Kijana wa AZANIA anayelipa ADA ya elfu 20 tu akionyesha maajabu mbele ya Mamilioni yaliyojaa Fedha kutokana na ADA za wanafunzi.

Jamali Juma aka BABU alikuwa very talented,na alikuwa very very very talented katika somo la MATHEMATICS.Wanafunzi wote wa AZANIA na DSM kwa ujumla waliamini kuwa sasa ENZI za Azania kutoa T.O tena zimerudi hivyo.Shule ya AZANIA ilikuwa na wakali wengi sana KIPINDI hicho ambao walifichwa ndani ya KIVULI cha JAMAL JUMA aka BABU.

Babu pamoja na kuwa alikuwa na uwezo mkubwa sana darasani ila alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafunzi wote wa AZANIA olev wanakuwa katika hali nzuri hivyo akaanza kupita darasani kuwafundisha wanafunzi mada ambazo walikuwa hawazielewi kabisa katika masomo yote kuanzia PHYSICS mpaka wale wazee wa kusoma kama wanasoma "GAZETI"(Hahahahah hili bifu nalibeba).Hakika babu alikuwa ni MFANO mzuri wa kuigwa(Wa Azania ni mashahidi).

Maisha yaliendelea mpaka matokeo ya Form 4,2009 yalipotoka ambapo T.O wetu wa DSM ahakuamini macho yake akijikuta ameangukia PUA na kuambulia DIV 1.10 kwa matokeo haya

upload_2017-12-18_18-0-54.png


Jamali Juma aka BABU akapangwa MZUMBE akasome PCM class ambalo atakuwemo T.O(hahahahah) anayeitwa GWAMAKA NJOBELO.

Story ya huyu GWAMAKA NJOBELO aliyekuwa wapili kitaifa naisummarize katika mtokeo yake haya
upload_2017-12-18_18-4-54.png


STORY YA MWAKA 2009 ikaishia hapo

Baada ya shule za Advance Kufunguliwa hatimaye SHULE YA "FEZA BOYS" ikafanikiwa kumshawishi JAMLI JUMA akajiunga FEZA na maisha ya ADVANCE yakawa na changamoto nyingi sana kwake hasa ALIPOJIKUTA kwenye KIVULI cha jamaa ZAWADI MDOE ambaye yeye hana kitu chochote anachokifiria zaidi ya KUWA T.O

===
TURUDI KIBAHA HIGH SCHOOL

Alilipoti mwanafunzi aliyekuwa na marks za kawaida tu OLEV aliyeitwa SILVESTER.Silvester alikuwa ni mwanafunzi ambaye 'ANAJUA ' mathematics kuliko mwanafunzi yeyote TANZANIA kipindi hiko,hivyo kwa kujiamini kabisa akatangaza kuwa hakuna MTU ALIYENIPITA Additional Math na Basic Math Olevel japo Sikuwa T.O ila Hakuna wa kushindana na mimi katika mtihani wa MATHEMATICS wowote.Silvester alinikuliwa akisema hata mwalimu wa KIBAHA nafahamu kabisa kuwa haniwezi math(Hahahaha).

Wanafunzi waliotoka MZUMBE na AZANIA Olev wakaenda KIBAHA wakmwambia "Sikia Silvester,wote tunajua hapa KIBAH kuwa wewe ndio MCHAWI wa namba ila kuna vichwa VIWILI huwezi shindana navyo kabisa ambao ni Jamal Juma aka BABU wa FEZA na GWAMAKA wa Mzumbe maana jamaa wakiliona tu swali wanaona mpaka mwisho wake".Silvester akawajibu simple tu naomba LIGI nao ya MATH tu niwathibitishie tu kuwa Tz Hii hakuna ZAIDI yangu katika Somo hili...Hahahah jamaa akatania kuwa "haya mambo yana wenyewe na wenyewe ndio sisi"

Haikuchukua mda mrefu hatimaye taarifa zikatua MZUMBE kwa MA-TOs kuwa kuna dharau huko KIBAHA hivyo wanahitajika KWENDA KIBAHA kuwasha MOTO.Hahahah wanafunzi wa MZUMBE hawakuwa na presha na SILVESTER maana walikuwa wanafahamu kuwa MZUMBE na KIBAHA wanafanya mtihani mmoja wa MOCK(ezeb) hivyo mwambieni ajiandae vizuri tunakuja kuwasha MOTO.

=====
Hatimaye taarifa zikatumwa kwa BABU aka MCHAWI wa MATH DSM akitokea FEZA na kuamua kuwa YUPO tayari kufanya MTIHANI na SILVESTER Jangwani Sec kwa Manyirizu kama atakuwa tayari.

Kilia jumamosi BABU akawa anaenda kujipima KWA Manyirizu kumsubili SILVESTER,na wakati huo huo SILVESTER anachati tu kwa simu yake akimsubiri BABU siku itakapo fika akaonyeshe kuwa Tz hii hakuna kama yeye katika math.

Siku ilipofika wanafunzi wa KIBAHA waliosoma na BABU Azania wakampigia simu kumwambia nasi tutakuja kufanya mtihani kwa manyilizu hivyo KIBAHA BOYS itahamia JANGWANI GIRLS.Vijana wa KIBAHA wakatimba KWA MANYIRIZU huku Babu akiwa hayupo na walipomtafuta kwenye simu hakupatikana kabisa.Hii tunaitwa "Jamaa alikimbia "..

Vijana wa KIBAHA BOYS wakafanya mtihani na kuondoka na "A" zao huku vilaza wengine wa DSM wakaambulia C na B..

Kama kawaida,week iliyofuata BABU akaripoti kituo cha mtihani JANGWANI kujipima(Hii tunaita unaangalia kwanza usalama then unaenda) na akawa kama anasukuma WALEVI baada ya SPECIAL SCHOOL NIGGAS kuondoka.

Baada ya weeks 3 babu akatoa sababu mbali mbali za msingi za kutoweza kufika siku ile kujipima hivyo akawaomba waje tena awawashie moto..

VIJANA WA KIBAHA wakwambia SILVESTER ajiaandae kesho(Ijumaa) waondoke watafikia HOSTEL za Azania na watamlipia nauli ya kwenda na kurudi na hela ya kula.Jeshi la watu 19 walitoka KIBAHA wakiongoza na SILVESTER kwenda Azania ila katika kundi hili la watu 19 atakayefanya mtihani ni mmoja tu,yaani wengine ni wapambe tu(Hahahahah wanafunzi bhana).

Baada kufika BABU na SILVESTER wakaingia CHUMBA cha mtihani huku nje vijana wa KIBAHA BOYS wanabadilishana mawazo na JANGWANI Dadaz waliokuwepo hapo(Yani vijana wakapata vitonga)..

Baada ya kutoka CHUMBA cha mtihana wote SILVESTESTER na BABU walikuwa na FURAHA kuonyesha kila mmoja anajiamini kuwa HAKUNA wa kumzuia kuwa wa kwanza.

MATOKEO YALIPOBANDIKWA

Matokeo yalionyesha kama ifuatavyo:
1.SILVESTER aliyepata 100%
2.BABU aliyepata 99% na
3.Said aka MSELEM wa Azania aliyepata 71%

Na huo ndio ukawa mwisho wa UBISHI wa Babu na SILVESTER .Kama ilivyo desturi ya MANYIRIZU ambapo MTU anayekuwa wa KWANZA atafanya mtihani ujao bure hivyo nafasi hii ikaangukia kwa SILVESTER amabaye hatokuwepo DAR hivyo akaamwambia MANYIRIZU kuwa nafasi hiyo ampe BABU na manyirizu akafanya hivyo.

VIJANA WA KIBAHA BOYS WAKAONDOKA NA USHINDI

=====
Habari zikafika MZUMBE ambapo ilikuwa ni weeks mbili kabla ya MOCK aka EZEB.Vijana wa MZUMBE wakaongeza moto zaidi kujiandaa na EZEB wakijua kuwa KUTAKUWA na SILVESTER.

MATOKEO YA EZEB YALIKUWA KAMA IFUATAVYO:

Best Student overall alitoka MZUMBE anayeitwa GWAMAKA NJOBELO akipata 1.3 PCM huku akiwa na A ZOTE PCM

NOTE:Silvester alikuwa na Div 1.5 hivyo hakuingia hata TOP 20

Waliongoza masomo PCM ni wafuatao:

1.GWAMAKA JOBELO(Physics-A)
2.GWAMAKA JOBELO(Chemistry-A)
3.SILVESTRE(Advance Math-A)

Na huo ndio ukawa Mwisho wa ubishi wa SILVESTER na GWAMAKA.Dah maisha bhana Kwa mara ya kwanza GWAMAKA AKAKILI KUWA "Simuwezi Silvester Math".Matango yote ya math kutoka mzumbe yakawa yanatatuliwa KIBAHA kwa Genius SILVESTER ambaye kwake hakuna swali linalompa changamoto kwenye TRANTA.
======

Matokeo ya mwisho kitaifa yalikuwa kama ifuatavyo:

1.Jamali Juma aliingia TOP 10 akiwa wa 4 kitaifa
upload_2017-12-18_18-51-55.png


Matokeo ya Jamali Juma
upload_2017-12-18_18-56-49.png

Ikumbukwe kuwa mwaka 2012 div 1.3 kitaifa zilikuwa 4 tu huku jamali Juma akifunga namba nne

(Huyo watatu kitaifa kutoka Minaki Katika mtihani wa MOCK EZEB alikuwa Div 1.5 huku akipata A ya phys na math na C ya Chem,matokeo ya necta alikuwa wa pili chemistry kitaifa)

2.GWAMAKA NJOBELO

Alikuwa wa 8 kitaifa baada ya kupata 1.4

Na haya ndio matokeo yake
upload_2017-12-18_18-59-23.png


3.SILVESTER MWAGENI
upload_2017-12-18_19-4-52.png



Baada kutoka kwenye mtihan wa math FORM 6,SYLVESTER Alionekana amechukia sana na alipoulizwa mtihani unauonaje akajibu "Mtihani ni mwepesi sana,sijawahi kuona mtihani mwepesi kama ule.Ni bora mtihani uwe mgumu ili tutakaopata 100% tuwe wachache kuliko mtihani ule ambao tutakaopata 100% tutakuwa wengi sana".

Na SYLVESTER hakuingia TOP 10 ila hakuna mtu aliyempita ADV MATH..Yani kwa kifupi ndiye Best Student WA ADVANCE MATH.


=====
TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO


DEADBODY
 
Hahaha
ule ubishi pale Mchikichini kwa Moody Physics kwa hawa jamaa ilikuwa hatari.

Huyo Babu na Gwamaka walikuwa wanasoma namba kwa jamaa mmoja anaitwa Log,

Ilikuwa hatari
Log boy..
Jamaa alikuwa anamkubali sana babu .
sema nae yko vizuri pure ila anabore kumdiss dis mwarami mda wote.

Boss nawe ulipita yale maeneo kumbe. .??
 
Log boy..
Jamaa alikuwa anamkubali sana babu .
sema nae yko vizuri pure ila anabore kumdiss dis mwarami mda wote.

Boss nawe ulipita yale maeneo kumbe. .??
Mimi nilikuwa Mdau sana Mchikichini. O'level nilipiga namba kwa Mtata De Mtatuzi, jamaa kanipa A ya namba O'level.

Bado sijaona jamaa anae weza shindana Namba na Mtata De Mtatuzi. Hao akina Mwarami sijui Log boy hawafui dafu kwa jamaa.

Form 4 Class of 2010.
Hatar
 
Back
Top Bottom