Nina rafiki yangu toka Kanda ya ziwa kule ambako mbunge wao wa bunge lililopita alikua anatokea upinzani. Huyu jamaa alikua anafanya kazi kwenye taasisi ya umma yenye hela nje nje na alikua ameoa toka kwao mmama mzuri lakini mweusi. Jamaa alikutana na manka fulani toka Kilimanjaro magharibi, si unajua wale wakiamua kuwa wazuri wanakua wazuri kweli.
Jamaa katupa ndoano na manka akaidaka kama vile alikua anaisubiri. Jamaa alionjeshwa vitu vitamu na adimu na mtoto mweupe (by the way weupe ndio ugonjwa wa jamaa zangu yoka Kanda ya ziwa). Jamaa kila akitoka ofisini na mark two yake, enzi hizo mark two ndio Kama harrier ya sasa hivi lazima ampitie manka wakale Bata. Kwa mkewe Tena hakumbuki kijana keshaonja mtori wenye nyama nyingi uji wa ulezi sijui mtama alikua hautaki Tena.
Kuna siku shetani hakuwa busy sana aliwatembelea, rafiki yangu na manka kwenye sehemu waliokua wanakata kiu. Shetani aliwahimiza wanywe sana na walipolewa akawaambia wasiende kwa Manka Bali waende kwa jamaa yangu Sinza. Basi waliondoka na mark two Hadi Sinza, shetani akamuelekeza jamaa jinsi ya kufungua geti, kupaki gari na kubisha hodi ili housegel afungue mlango.
Housegel akafungua mlango na kurudi kulala. Hapa ukumbuke mke wa jamaa yuko chumbani na alisikia mlango ukifunguliwa lakini aliendelea na hamsini zake. Jamaa kaingia sitin rum na manka na shetani akawaelekeza jinsi ya kukumbatiana wakiwa kwenye Kochi na Mara usingizi ukawapitia.
Mama anasubiri mume aingie chumbani, hamuoni kumbe yuko na Manka wamekumbatiana kwenye Kochi na wako usingizini. Mama akaona akakague isije ikawa kidume kaingia kwa hausegel. Aliyoyakuta hakuamini macho yake. Mume kaleta mchepuko mpaka ndani na wamekumbatiana kimahaba. Mama aliingia jikoni chap akawasha birika ya kuchemshia maji Moto. Maji yalipochemka akayatia sukari nyingi ili kuongeza joto. Kisha akayatia kwenye jagi na kuwamwagia kifuani na kutokomea kusikojulikana. Wote walizimia pale pale. Asubuhi hausegel akatoa taarifa kwa majirani na dume ambae aliumia sana aliwahishwa Muhimbili huku manka akipelekwa Mwananyamala.
Itaendelea.....